doctor Of doctors
Member
- Aug 8, 2026
- 61
- 91
Mapema leo akihojiwa na kituo cha runinga cha MS Now, mbunge wa baraza la wawakilishi kutoka huko Minneapolis, Minnesota, kaulizwa swali kuhusu mwanaume aliyeoana naye ambaye inadaiwa kuwa ni ndugu yake/ kaka yake.
ilhan kajibu “not to my knowledge”.
Anzia dakika ya 14:12 mpaka 15:00.
View: https://youtu.be/SPGxj0mhTBU?is=SGBGlYclmHJ9Dj9W
Jibu la hilo swali ni jepesi mno.
Ni kiasi cha kusema tu ndiyo au hapana.
Utashindwaje kujua kama unayeoana ni kaka yako au la?
Mimi nahisi hapo wamemshika pabaya Ilhan.
Kwenye immigration fraud Marekani, watu kuoana na ndugu zao ili wapate makaratasi ni jambo linalofanyika sana.
Uwezekano wa Ilhan na kaka yake kuoana ili kaka mtu apate makaratasi, ni mkubwa sana.
Sio marekani tu,hata Uingereza pia upo udanganyifu mwingi,wapo pia wanaotumia vyeti vya kuzaliwa sio vyao,kwa mfano kazaliwa Tanzania,anatumia cha
cha kuzaliwa cha Somalia,na tarehe ya kuzaliwa tofauti,anapata uraia na Passport ya Uingereza,hivi inakuwaje wazungu,wanadanganyika ki urahisi sana?