Hii ripoti ya CAG tutaanza kukanyagana, "Sijui tuanze kumlaumu nani?"

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
268
1,000
HII RIPOTI YA CAG TUTAANZA KUKANYAGANA, "SIJUI TUANZE KUMLAUMU NANI"?

Na Elius Ndabila
0768239284

Riporti ya mwaka huu ya CAG inaonyesha kunaubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Rushwa sasa inaonekana imeota mizizi mikuu. Waliokuwa wakikemea rushwa kwa mkono wa kulia, walikuwa wametega mkono wa kushoto kupokea rushwa.

Vitabu vya dini vinakemea namna rushwa inavyoweza kuusaliti ukweli.

Mfano mbaya zaidi wa rushwa katika Biblia ni vipande thelathini vya fedha ambazo Yuda alipokea kumsaliti Bwana Yesu. Matokeo ya moja kwa moja ya udanganyifu wa Yuda ni kwamba Yesu alikamatwa na kusulubiwa. Hatimaye, hata Yuda alitambua kuwa kukubali rushwa ilikuwa mbaya. Lakini alipojaribu kurejesha fedha kwa makuhani wakuu na wazee, walikataa, wakiita "pesa ya damu" (Mathayo 27: 3-9).

Ripoti ina madudu mengi ambayo ni hatari kwa Taifa. Mwaka jana Mhe Kessy alisema Rais aongezewe muda kwa kuwa kazi yake hakuna mtu anayeweza kufanya, Mimi niliandika tutengeneze sera ya nchi ambayo hata leo JPM akiondoka basi mambo yasikwame. Nilitoa mtazamo huo nikiamini kuwa hata JPM akiongezewa miaka 30 bado hawezi kumaliza changamoto ambazo zimeota mizizi Tanzania. Niliamini kuwa sera ya nchi ingetumika kama mwongozo wa kiongozi yeyote ambaye angepata madaraka makubwa.

Kutokana na nchi kutokuwa na sera madhubuti ndiyo maana kunakuwa na upya kwenye kila awamu. Kila kiongozi anaongoza kwa utashi anaoamini anaisaidia nchi. Ndiyo maana kuna kuwa na makosa kwenye kila awamu. Na umekuwa utamaduni wa kawaida kila serikali inapoingia madarakani kugundua makosa na kukosoa serikali zilizopita na hii ni kwa karibia Afrika nzima. Nchi hazina sera ambazo zinaweza kuweka mipaka kwenye kila utawala.

Nchi inaongozwa kwa mihili mitatu yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Kwa sheria za nchi yetu Mihili yote ina wajibu sawa ila kiutendaji kwa kwa riporti hii utagundua serikali ina nguvu kuliko mihimili mingine. Hebu jiulize Mhe Jobu Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila hofu anasimama mbele ya camera kuwa waliomshauri Rais kuachana na mradi wa Bagamoyo walimpotosha. Mhe Spika anaenda mbali kwa kusema kuwa kwa kuwa bwana mkubwa ameongea ndo inakuwa basi tena.

Anayezungumza maneno haya ni kiongozi anayesimamia mhimili wenye wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia sheria. Je, kama Bunge nalo linaogopa kuisimamia serikali kwa kuikosoa na kuishauri Bunge linabaki kuwa la kazi gani? Je, Spika baada ya kugundua kuwa maelezo ya Mhe Rais yanaviashiria vya kuwa hakuambiwa ukweli yeye na Bunge walichukua hatua gani? Je tunatenganishaje Bunge kutotimiza majukumu yake ipasavyo na haya makosa ya kiufundi ya viongozi?

Bunge ndiyo krunzi ya Wananchi kwa maana ya dhana ya kuisimamia serikali. Viongozi wakuu wa nchi hawawezi kujua kila kitu ndiyo maana lipo Bunge la kuisimamia na yapo Mahakama ya kuwachukulia hatua wale ambao hawakutimiza wajibu wao ipasavyo.

Leo hii tunasoma ripoti ya CAG ambayo inaibua maswali mengi. Bado unajiuliza hivi haya wakati yanafanyika Bunge liliona? Kama halikuona kwa nini halikuona? Ninadhani sasa ripoti hii ilifanye Bunge kuwa na macho na lionyeshe uwezo halisi wa kuisimamia serikali. Watu wote ambao wataonekana kuthibitika kuhusika kwenye upotevu huu wa fedha wachukuliwe hatua kali.

Rais Magufuli alijitahidi sana kupambana na ruswa tena kwa vitendo. Lakini inaonyesha kuwa akiwa anapambana na mapapa waliokuwa wanaonekana ni wanufaika wa rushwa, bado dagaa wengine walikuwa wakimzunguka na kutafuna fedha za miradi.

Amosi 5:12 Inasema, "Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyokubwa. Ninyi munawaonea wenye "HAKI", Mnapokea "RUSHWA" na kuwageuza watu wahitaji langoni ili wasipate "HAKI" yao. Ukweli ni kuwa rushwa ni adui wa kupindua haki, aliyestahili hupewa asicho stahili. Wahitaji hawapati haki, wasiyo wahitaji kupora haki kwa wahitaji.

Ripoti hii ya CAG si inshara njema kwa Taifa lakini pia ni ukweli kuwa Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado anayo kazi kubwa kumaliza vimelea hivi vya Rushwa.

Tafsiri halisi ya uzalendo inaanza kupauka kwa kuwa wengi wa waliokuwa wanaimba pambio za Uzalendo wanatuhumiwa na ripoti hii. Ninatambua hizi ni tuhuma na Bunge litapata nafasi pana ya kuzijadili. Lakini kama itathibitika ukweli juu ya haya ninadhani ni vema tukaangalia njia mpya ya kupambana na janga hili ambalo naweza sema virusi vyake ni hatari kuliko ugonjwa wa Corona. Haipendezi watu waliokuwa wakiimba wimbo wa Rais aongezewe muda, Rais alindwe, Rais aombewe na vitu vingine kama hivi lakini kwenye ripoti watajwe kuwa vinara wa ukwapuaji.

Bunge halikutimiza wajibu wake. Na ni wazi Bunge linaiogopa serikali kwa kuwa hata Ndugai Spika wa Bunge kwa maneno yake ya jana ya Bwana mkubwa akiongea inabidi kukaa kimya inaonyesha Bunge ni zipped. Bunge lilishindwa kutumia haki yake ya kikatiba ya kuibana serikali kwa kuhoji mapato na matumizi.

Nini maoni yangu?

Maoni yangu ni ya aina mbili.

Jambo la Kwanza Bunge livae viatu vyake ambavyo ni kwa mjibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 63(2) na (3). Ibara hii inalipa nguvu Bunge kuisimamia na kuishauri Serikali ya JMT. Ili kutimiza haya wanawajibu wa kumuuliza waziri yeyote maswali, kujadili utekelezaji wa kila wizara, kujadili mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na JMT, kutunga sheria na mwisho kujadili na kuridhia mikataba. Mijadala ya Wabunge inalindwa na Ibara ya 100 ya Katiba inayozungumzia Madaraka na Haki za Bunge.Kwa maoni mengi kati ya haya hayakufanywa ndio maana ripoti ina uozo mwingi. Bunge lirudi kwenye majukumu yake, liachane na tabia za "KUPONGEZA".

Mkaguzi ameshatimiza haki yake inayolindwa na Ibara ya 143 ya Katiba ya JMT ya 1977 pamoja na mabadiliko yake. Sasa ni haki yenu kwenda kuijadili kwa kina kwa masilahi mapana ya nchi.

Maoni yangu ya Pili, ninashauri kama Taifa tuwe na mpango wa nchi ambaye kila Rais na serikali yake anapoingia madarakani atausimamia. Kukiwa na sera kila mtu atasimama kwenye sera hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo kila Kiongozi anakiwa na vipao mbele vyake na vingine hugokana tu na mawazo yake.

Nimetumia haki yangu ya Kikatiba Ibara ya 18(1), Ibara ambayo inatoa uhuru wa kutoa "MAONI".
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,024
2,000

Bw. Ndabila
Nimekucote kwenye dhana yako hii kwa kuunga mkono hoja.
Hayati Mh.JPM alitimiza wajibu wake,
lakini Bunge na Mahakama wakiwa kama mihimili miwili ya kuisaidia Serikali na kuikosoa au kuilaumu walipwaya sana.

Spika wetu Ndungai alisaidiana na serikali kuwafurusha wakosoaji pale Bungeni.
Mahakaa nazo zilishirikiana na serikali kuwadhibiti wakosoaji kwa kuwaweka kizuizini kwa kesi za kupanga.
Mihimili hii ilipopwaya ndipo JPM alipojiona yuko Right kusimama kama ''Mungu mtu''.
Waandishi wa habari walipo pigwa stop na kufumgwa midomo, hapo ndio ukawa mwisho wa uwazi .Taifa likawa la Kidikteta kamili.

Wahalifu walipobaini kuwa matumizi ya serikali Hayapangwi bungeni, bali kwa maamuzi ya Raisi ikulu.Hazina nao walipogundua kuwa Fedha inatoka kwa amri ya raisi tuu,si kwa njia za kawaida ilizozoweleka, hapo ndio walijikita kufakamia mapesa ya umma.Ni wizi Wizi Wizi kila kona

Makosa haya hayawezi kumkwepa hayati JPM yeye binafsi na washauri wake kama alikuwa anashaurika.
lakini hayawezi kumkwepa spika na Bunge lake aidha. Jaji mkuu na mahakama zake naye pia ana wajibu wa kubeba zigo katika hili. Waziri mkuu hawezi kutoka,hasa niikumbuka masuala ya wakulima wa korosho na mbaazi wa kusini Tanzania.

Mam samia ana kazi ya kuweka mambo sawa bila ya kutazama sura za watu au lawama za wenye kulaumu.
Htokosa upinzani kwa jina la Kumuenzi JPM.Lakini ukweli hauwezi kupingika kuwa yako aeneo JPM kaenda kombo
Hasa ushirikiano wa Kimataifa, Kuwazingua wafanya biashara, na Kuifanya tanzania ni milki ya wamachinga kwa kufanya biashara hata katikati ya barabara za mjini. huku watembea kwa miguu wakipigana vikumbo na magari kwa kukosa sehemu za kutembea kwa miguu.
Taifa limekuwa la kiholela mno. Kisingizio Uzalendo
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,831
2,000
Sisi hatuna haja na sera tuna haja na Katiba mpya itakayozipa taasisi uwezo kuhakikisha wananchi wote ni sawa na hawawezi kuporwa haki zao za kimaendeleo, uhuru wa habari, kuchagua na kukusanyika
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,831
2,000
Maelezo yako ni mazuri sana kama sehemu zote zenye neno sera utaweka KATIBA MPYA.

Bunge haliwezi kuvaa viatu vyake kwa katiba hii kwa sababu wabunge wote pamoja na Spika wanaweza kupoteza nafasi zao kwa kufutwa tu uanachama na chama chao. Sasa fikiria pale amabapo pale mwenyekiti chaka ndiye Rais na anataka jambo lake lipite bungeni kama kuna mtu wa kumzuia. Rejea yaliyowakuta Hawa Ghasia, Nape na wabunge wengine wa kusini walipojaribu kuisimamia serikali kwenye sakata la Korosho dhidi ya mwenyekiti wao!
HII RIPOTI YA CAG TUTAANZA KUKANYAGANA, "SIJUI TUANZE KUMLAUMU NANI"?

Na Elius Ndabila
0768239284

Riporti ya mwaka huu ya CAG inaonyesha kunaubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Rushwa sasa inaonekana imeota mizizi mikuu. Waliokuwa wakikemea rushwa kwa mkono wa kulia, walikuwa wametega mkono wa kushoto kupokea rushwa.

Vitabu vya dini vinakemea namna rushwa inavyoweza kuusaliti ukweli.

Mfano mbaya zaidi wa rushwa katika Biblia ni vipande thelathini vya fedha ambazo Yuda alipokea kumsaliti Bwana Yesu. Matokeo ya moja kwa moja ya udanganyifu wa Yuda ni kwamba Yesu alikamatwa na kusulubiwa. Hatimaye, hata Yuda alitambua kuwa kukubali rushwa ilikuwa mbaya. Lakini alipojaribu kurejesha fedha kwa makuhani wakuu na wazee, walikataa, wakiita "pesa ya damu" (Mathayo 27: 3-9).

Ripoti ina madudu mengi ambayo ni hatari kwa Taifa. Mwaka jana Mhe Kessy alisema Rais aongezewe muda kwa kuwa kazi yake hakuna mtu anayeweza kufanya, Mimi niliandika tutengeneze sera ya nchi ambayo hata leo JPM akiondoka basi mambo yasikwame. Nilitoa mtazamo huo nikiamini kuwa hata JPM akiongezewa miaka 30 bado hawezi kumaliza changamoto ambazo zimeota mizizi Tanzania. Niliamini kuwa sera ya nchi ingetumika kama mwongozo wa kiongozi yeyote ambaye angepata madaraka makubwa.

Kutokana na nchi kutokuwa na sera madhubuti ndiyo maana kunakuwa na upya kwenye kila awamu. Kila kiongozi anaongoza kwa utashi anaoamini anaisaidia nchi. Ndiyo maana kuna kuwa na makosa kwenye kila awamu. Na umekuwa utamaduni wa kawaida kila serikali inapoingia madarakani kugundua makosa na kukosoa serikali zilizopita na hii ni kwa karibia Afrika nzima. Nchi hazina sera ambazo zinaweza kuweka mipaka kwenye kila utawala.

Nchi inaongozwa kwa mihili mitatu yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Kwa sheria za nchi yetu Mihili yote ina wajibu sawa ila kiutendaji kwa kwa riporti hii utagundua serikali ina nguvu kuliko mihimili mingine. Hebu jiulize Mhe Jobu Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila hofu anasimama mbele ya camera kuwa waliomshauri Rais kuachana na mradi wa Bagamoyo walimpotosha. Mhe Spika anaenda mbali kwa kusema kuwa kwa kuwa bwana mkubwa ameongea ndo inakuwa basi tena.

Anayezungumza maneno haya ni kiongozi anayesimamia mhimili wenye wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia sheria. Je, kama Bunge nalo linaogopa kuisimamia serikali kwa kuikosoa na kuishauri Bunge linabaki kuwa la kazi gani? Je, Spika baada ya kugundua kuwa maelezo ya Mhe Rais yanaviashiria vya kuwa hakuambiwa ukweli yeye na Bunge walichukua hatua gani? Je tunatenganishaje Bunge kutotimiza majukumu yake ipasavyo na haya makosa ya kiufundi ya viongozi?

Bunge ndiyo krunzi ya Wananchi kwa maana ya dhana ya kuisimamia serikali. Viongozi wakuu wa nchi hawawezi kujua kila kitu ndiyo maana lipo Bunge la kuisimamia na yapo Mahakama ya kuwachukulia hatua wale ambao hawakutimiza wajibu wao ipasavyo.

Leo hii tunasoma ripoti ya CAG ambayo inaibua maswali mengi. Bado unajiuliza hivi haya wakati yanafanyika Bunge liliona? Kama halikuona kwa nini halikuona? Ninadhani sasa ripoti hii ilifanye Bunge kuwa na macho na lionyeshe uwezo halisi wa kuisimamia serikali. Watu wote ambao wataonekana kuthibitika kuhusika kwenye upotevu huu wa fedha wachukuliwe hatua kali.

Rais Magufuli alijitahidi sana kupambana na ruswa tena kwa vitendo. Lakini inaonyesha kuwa akiwa anapambana na mapapa waliokuwa wanaonekana ni wanufaika wa rushwa, bado dagaa wengine walikuwa wakimzunguka na kutafuna fedha za miradi.

Amosi 5:12 Inasema, "Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyokubwa. Ninyi munawaonea wenye "HAKI", Mnapokea "RUSHWA" na kuwageuza watu wahitaji langoni ili wasipate "HAKI" yao. Ukweli ni kuwa rushwa ni adui wa kupindua haki, aliyestahili hupewa asicho stahili. Wahitaji hawapati haki, wasiyo wahitaji kupora haki kwa wahitaji.

Ripoti hii ya CAG si inshara njema kwa Taifa lakini pia ni ukweli kuwa Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado anayo kazi kubwa kumaliza vimelea hivi vya Rushwa.

Tafsiri halisi ya uzalendo inaanza kupauka kwa kuwa wengi wa waliokuwa wanaimba pambio za Uzalendo wanatuhumiwa na ripoti hii. Ninatambua hizi ni tuhuma na Bunge litapata nafasi pana ya kuzijadili. Lakini kama itathibitika ukweli juu ya haya ninadhani ni vema tukaangalia njia mpya ya kupambana na janga hili ambalo naweza sema virusi vyake ni hatari kuliko ugonjwa wa Corona. Haipendezi watu waliokuwa wakiimba wimbo wa Rais aongezewe muda, Rais alindwe, Rais aombewe na vitu vingine kama hivi lakini kwenye ripoti watajwe kuwa vinara wa ukwapuaji.

Bunge halikutimiza wajibu wake. Na ni wazi Bunge linaiogopa serikali kwa kuwa hata Ndugai Spika wa Bunge kwa maneno yake ya jana ya Bwana mkubwa akiongea inabidi kukaa kimya inaonyesha Bunge ni zipped. Bunge lilishindwa kutumia haki yake ya kikatiba ya kuibana serikali kwa kuhoji mapato na matumizi.

Nini maoni yangu?

Maoni yangu ni ya aina mbili.

Jambo la Kwanza Bunge livae viatu vyake ambavyo ni kwa mjibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 63(2) na (3). Ibara hii inalipa nguvu Bunge kuisimamia na kuishauri Serikali ya JMT. Ili kutimiza haya wanawajibu wa kumuuliza waziri yeyote maswali, kujadili utekelezaji wa kila wizara, kujadili mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na JMT, kutunga sheria na mwisho kujadili na kuridhia mikataba. Mijadala ya Wabunge inalindwa na Ibara ya 100 ya Katiba inayozungumzia Madaraka na Haki za Bunge.Kwa maoni mengi kati ya haya hayakufanywa ndio maana ripoti ina uozo mwingi. Bunge lirudi kwenye majukumu yake, liachane na tabia za "KUPONGEZA".

Mkaguzi ameshatimiza haki yake inayolindwa na Ibara ya 143 ya Katiba ya JMT ya 1977 pamoja na mabadiliko yake. Sasa ni haki yenu kwenda kuijadili kwa kina kwa masilahi mapana ya nchi.

Maoni yangu ya Pili, ninashauri kama Taifa tuwe na mpango wa nchi ambaye kila Rais na serikali yake anapoingia madarakani atausimamia. Kukiwa na sera kila mtu atasimama kwenye sera hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo kila Kiongozi anakiwa na vipao mbele vyake na vingine hugokana tu na mawazo yake.

Nimetumia haki yangu ya Kikatiba Ibara ya 18(1), Ibara ambayo inatoa uhuru wa kutoa "MAONI".
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??

*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,831
2,000
Hayo yote yataliwa kichwa kwa sababu Alipokuwa anaunua ndege bila idhini ya bunge hakujieleza , alipojenga Bwawa la Umeme bila feasibility study na Tathmini ya mazinga hakujieleza. Zaidi sana alisema yeye ukimshauri ndio unaharibu kabisa.

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,729
2,000
Hakika ujinga wa utoton unaweza kumalizika lkn ujinga wa uzeen lazma utakufa nao

Ni nyumbu tu watakaokubaliana na hilo
 
Babu Kijana

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
529
250
HII RIPOTI YA CAG TUTAANZA KUKANYAGANA, "SIJUI TUANZE KUMLAUMU NANI"?

Na Elius Ndabila
0768239284

Riporti ya mwaka huu ya CAG inaonyesha kunaubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Rushwa sasa inaonekana imeota mizizi mikuu. Waliokuwa wakikemea rushwa kwa mkono wa kulia, walikuwa wametega mkono wa kushoto kupokea rushwa.

Vitabu vya dini vinakemea namna rushwa inavyoweza kuusaliti ukweli.

Mfano mbaya zaidi wa rushwa katika Biblia ni vipande thelathini vya fedha ambazo Yuda alipokea kumsaliti Bwana Yesu. Matokeo ya moja kwa moja ya udanganyifu wa Yuda ni kwamba Yesu alikamatwa na kusulubiwa. Hatimaye, hata Yuda alitambua kuwa kukubali rushwa ilikuwa mbaya. Lakini alipojaribu kurejesha fedha kwa makuhani wakuu na wazee, walikataa, wakiita "pesa ya damu" (Mathayo 27: 3-9).

Ripoti ina madudu mengi ambayo ni hatari kwa Taifa. Mwaka jana Mhe Kessy alisema Rais aongezewe muda kwa kuwa kazi yake hakuna mtu anayeweza kufanya, Mimi niliandika tutengeneze sera ya nchi ambayo hata leo JPM akiondoka basi mambo yasikwame. Nilitoa mtazamo huo nikiamini kuwa hata JPM akiongezewa miaka 30 bado hawezi kumaliza changamoto ambazo zimeota mizizi Tanzania. Niliamini kuwa sera ya nchi ingetumika kama mwongozo wa kiongozi yeyote ambaye angepata madaraka makubwa.

Kutokana na nchi kutokuwa na sera madhubuti ndiyo maana kunakuwa na upya kwenye kila awamu. Kila kiongozi anaongoza kwa utashi anaoamini anaisaidia nchi. Ndiyo maana kuna kuwa na makosa kwenye kila awamu. Na umekuwa utamaduni wa kawaida kila serikali inapoingia madarakani kugundua makosa na kukosoa serikali zilizopita na hii ni kwa karibia Afrika nzima. Nchi hazina sera ambazo zinaweza kuweka mipaka kwenye kila utawala.

Nchi inaongozwa kwa mihili mitatu yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Kwa sheria za nchi yetu Mihili yote ina wajibu sawa ila kiutendaji kwa kwa riporti hii utagundua serikali ina nguvu kuliko mihimili mingine. Hebu jiulize Mhe Jobu Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila hofu anasimama mbele ya camera kuwa waliomshauri Rais kuachana na mradi wa Bagamoyo walimpotosha. Mhe Spika anaenda mbali kwa kusema kuwa kwa kuwa bwana mkubwa ameongea ndo inakuwa basi tena.

Anayezungumza maneno haya ni kiongozi anayesimamia mhimili wenye wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia sheria. Je, kama Bunge nalo linaogopa kuisimamia serikali kwa kuikosoa na kuishauri Bunge linabaki kuwa la kazi gani? Je, Spika baada ya kugundua kuwa maelezo ya Mhe Rais yanaviashiria vya kuwa hakuambiwa ukweli yeye na Bunge walichukua hatua gani? Je tunatenganishaje Bunge kutotimiza majukumu yake ipasavyo na haya makosa ya kiufundi ya viongozi?

Bunge ndiyo krunzi ya Wananchi kwa maana ya dhana ya kuisimamia serikali. Viongozi wakuu wa nchi hawawezi kujua kila kitu ndiyo maana lipo Bunge la kuisimamia na yapo Mahakama ya kuwachukulia hatua wale ambao hawakutimiza wajibu wao ipasavyo.

Leo hii tunasoma ripoti ya CAG ambayo inaibua maswali mengi. Bado unajiuliza hivi haya wakati yanafanyika Bunge liliona? Kama halikuona kwa nini halikuona? Ninadhani sasa ripoti hii ilifanye Bunge kuwa na macho na lionyeshe uwezo halisi wa kuisimamia serikali. Watu wote ambao wataonekana kuthibitika kuhusika kwenye upotevu huu wa fedha wachukuliwe hatua kali.

Rais Magufuli alijitahidi sana kupambana na ruswa tena kwa vitendo. Lakini inaonyesha kuwa akiwa anapambana na mapapa waliokuwa wanaonekana ni wanufaika wa rushwa, bado dagaa wengine walikuwa wakimzunguka na kutafuna fedha za miradi.

Amosi 5:12 Inasema, "Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyokubwa. Ninyi munawaonea wenye "HAKI", Mnapokea "RUSHWA" na kuwageuza watu wahitaji langoni ili wasipate "HAKI" yao. Ukweli ni kuwa rushwa ni adui wa kupindua haki, aliyestahili hupewa asicho stahili. Wahitaji hawapati haki, wasiyo wahitaji kupora haki kwa wahitaji.

Ripoti hii ya CAG si inshara njema kwa Taifa lakini pia ni ukweli kuwa Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado anayo kazi kubwa kumaliza vimelea hivi vya Rushwa.

Tafsiri halisi ya uzalendo inaanza kupauka kwa kuwa wengi wa waliokuwa wanaimba pambio za Uzalendo wanatuhumiwa na ripoti hii. Ninatambua hizi ni tuhuma na Bunge litapata nafasi pana ya kuzijadili. Lakini kama itathibitika ukweli juu ya haya ninadhani ni vema tukaangalia njia mpya ya kupambana na janga hili ambalo naweza sema virusi vyake ni hatari kuliko ugonjwa wa Corona. Haipendezi watu waliokuwa wakiimba wimbo wa Rais aongezewe muda, Rais alindwe, Rais aombewe na vitu vingine kama hivi lakini kwenye ripoti watajwe kuwa vinara wa ukwapuaji.

Bunge halikutimiza wajibu wake. Na ni wazi Bunge linaiogopa serikali kwa kuwa hata Ndugai Spika wa Bunge kwa maneno yake ya jana ya Bwana mkubwa akiongea inabidi kukaa kimya inaonyesha Bunge ni zipped. Bunge lilishindwa kutumia haki yake ya kikatiba ya kuibana serikali kwa kuhoji mapato na matumizi.

Nini maoni yangu?

Maoni yangu ni ya aina mbili.

Jambo la Kwanza Bunge livae viatu vyake ambavyo ni kwa mjibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 63(2) na (3). Ibara hii inalipa nguvu Bunge kuisimamia na kuishauri Serikali ya JMT. Ili kutimiza haya wanawajibu wa kumuuliza waziri yeyote maswali, kujadili utekelezaji wa kila wizara, kujadili mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na JMT, kutunga sheria na mwisho kujadili na kuridhia mikataba. Mijadala ya Wabunge inalindwa na Ibara ya 100 ya Katiba inayozungumzia Madaraka na Haki za Bunge.Kwa maoni mengi kati ya haya hayakufanywa ndio maana ripoti ina uozo mwingi. Bunge lirudi kwenye majukumu yake, liachane na tabia za "KUPONGEZA".

Mkaguzi ameshatimiza haki yake inayolindwa na Ibara ya 143 ya Katiba ya JMT ya 1977 pamoja na mabadiliko yake. Sasa ni haki yenu kwenda kuijadili kwa kina kwa masilahi mapana ya nchi.

Maoni yangu ya Pili, ninashauri kama Taifa tuwe na mpango wa nchi ambaye kila Rais na serikali yake anapoingia madarakani atausimamia. Kukiwa na sera kila mtu atasimama kwenye sera hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo kila Kiongozi anakiwa na vipao mbele vyake na vingine hugokana tu na mawazo yake.

Nimetumia haki yangu ya Kikatiba Ibara ya 18(1), Ibara ambayo inatoa uhuru wa kutoa "MAONI".
Magufuli hajawahi kupambana na rushwa, alipambana na watu asiowapenda na wale aliowapenda aliwaachia wakipiga madili kama kawaida. Angalia ama-DC na RC alowaachia wakidhulumu watu na hawajachukuliwa hatua yoyote. Pia sikwambii kununua wabunge na madiwani wa upinzani kwa kuwatisha au kuwapa ushawishi/rushwa, hii pia ni rushwa alioisimamia yeye
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom