Hii picha ndio tafsiri halisi ya upendo wa kiume

Afisa Tabibu

JF-Expert Member
Oct 29, 2021
484
799
Masela wameacha sofa nyumbani, wapo hospital kumfariji mchizi wao.

Hakuna shada la maua, hakuna chocolate zilizoletwa kama zawadi, wahuni wapo wao na mioyo yao tu.

Hapo zishapigwa story za mademu, ushazungumzwa utani wa mpira, na michongo kibao wanayoisikilizia.

Hapo yamezungumzwa matumaini yasiyo na dalili ya kutimia.

Hapo zipo ndoto za kutoboa maisha, hata zisizo fikirika.

Kila kinywa kina neno la ushindi, hakuna wa kutangaza majanga ya mwenzake hapo, cha siri kitabaki sirini, matusi ndio rejesta pendwa zaidi hapo.

Story kuhusu ugonjwa unaomsumbua mchizi, zimepigwa kwa kiwango kidogo sana..

Washikaji wanaumia mwenzao kulazwa lakini kuna pole chache sana, wahuni wanajali kwa vitendo.

Kuna mwana hana nauli hapo, lakini atachangiwa na kesho atafika kwao.

Kuna mchizi hajui atakula nini, lakini baadae atashiba.

Hapo wameenda kumliwaza mgonjwa, lakini kuna mtu atafarijiwa kuhusu msoto wake kuliko hata huyo aliyelazwa.

Hii picha iwekeni kwenye maktaba zenu, zisizofikiwa na Panya yeyote yule.

Mkikutana na wana ma snitch waonesheni kuwa wanaume tuna kawaida ya kulindana
588317172.jpg
 
Wanaume tuna kawaida ya kulindana.

Ujumbe mahususi Kwa jamaa Ma snitch, wapuuzi, walojaa wivu na chuki zisizokua na maana, kisa unafanya kazi Kwa kujituma, baaasi Maneno Yao yanakua mengi !!.
 
Back
Top Bottom