Hii picha inawakilisha......

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Naamini Festi Ledi wetu anatuwakilisha vyema......Kiswahili Oyeeeeeee... au unasemaje kuhusu hii picha hapa chini.

i224_FirstLady.jpg

 

Attachments

  • First Lady.jpg
    First Lady.jpg
    111.8 KB · Views: 110
Last edited by a moderator:
Ni mkutano upi huo jamani. Du mafesti ledi kibao kila lugha na rangi. Ila tu kwani ni lazima azungumze Kiingereza???? Mbona Wajapan na Wachina hamuwasemi??? They speak their language na wakilazimika kuongea kimombo ni broken na hawajali kabisa!!!!! Wanachojali ni kutokosea tu kuongea Lugha yao. Nasi kwa our dear first lady kinachojalisha ni asikosee tu Kiswahili chake, kwa maana nyingine azungumze kiswahili fasaha. Asiyeelewa Kiswahili atafute mkalimani.
 
What is the problem? Kama JK anaweza kuhutubia AUA kwa kiswazi yeye Salma atashindwa nini. After, all hawakwenda kushindana lugha. Lakini pia msisahau Salma ni mwalimu mstaafu.
 
Kiswahili oyeeee... ajili gani? ama kwa kuwa amekaa mbele?, pengine bango lake lingeandikwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" hapo ningeelewa.
 
asalamu alaykum.

ndipo hapo tunapoonekana waafrika niw atu wa ovyo kwa kushindwa kuthamini chetu sio lazima mtu ajue kiingereza ndio tumuoite msomi lugha nzuri na ya kujivunia mtu kuzungumza lugha yake ila kama akiwa anajua lugha nyengine za kigeni ndio vizuri lakini cha muhimu mtu kujisifia na kujivunia chake kwanza.

hivyo vitu walivyovaa masikioni vinasauti za lugha mbali mbali na siku hizi mikutano ya kimataifa huwa lugha nyingi zinawekwa kwa kuwa kuna wakalimali kule wanatafsiri kwa hivyo sio tatizo pengine yupo makini katika kusikiliza kinachzunguzmwa katika mkutano huo.
acheni dharau vijana
 
But the world is not allowing us to use Swahili!!, do we have to close the borders anyway??.
 
Mimi huyo mama aliye pembeni mwa "First Lady" naona kama kajichokea tu, anaonekana kama anaomba hotuba iishe aende shopping.
 
Mkuu Indume Y,

Naomba kueleshwa uhusiano wa KISWAHILI na hii picha ya 1st Lady

?

Nadhani Indume Y alitaka kuonyesha kwamba kama nchi ni moja, hakukuwa na haja ya kuwepo kwa ma-First lady wawili. Kwani Baba Enock huoni pembeni ya Festi Ledi wa sasa yupo Festi Ledi wa zamani? Maybe ndo IY antaka kuhusianisha picha hii na Kiswahli!
 
Mnajuaje kama huyo mtu aliyekuwa akizungumza alikuwa akitumia lugha ya Kiarabu au Kifaransa!.....tatizo nini haswa, sii unasikiliza kitu upate kuelewa au inapofikia kiingereza basi wewe unaelewa zaidi ya watu wote!
Wadanganyika jamani ama kweli sisi malimbukeni..
 
Mwanzilishi wa hii thread kashindwa kuielewa hiyo picha. Hii picha na lugha ya kiswahili
mbona havina uhusiano?

Iangalie tena picha vizuri.

Hata akiongea kiswahili si atakuwa anaongea lugha yake na anayoijua vizuri? hakuna ubaya hapo.
 
Nafikiri mwenye thread kuna kitu anataka tuchangie........nasikia Muungwana ana majiko ma2 ina maana wa pili hakwenda nae....au kiprotokali anafaa kusafiri na wake wangapi??
Pia wa pili anaitwaje....secondlady?
 
unasema anatuwakilisha vyema,wewe na nani?
eti anakuwakilisha vyema.unajua alichoongea huko?
wabongo bwana.ndiyo mana hata kina chenge wanaiba bila wasiwasi wowote!
 
Nafikiri wengi mna'miss' kitu fulani - msiwe na papara - study the picture and give it a long loooooong look !!:)
 
Back
Top Bottom