Kuna nchi zitakazonufaika na fursa hii ya soko wazi la China

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
21,561
Reaction score
30,195
china wameamua kuweka soko lao wazi kwa nchi za kiafrika kuingiza bidhaa zao bila ya ushuru (zero tariffs) kuanzia sasa.

Pamoja na kuwa bidhaa nyingi kutoka afrika ni mali ghafi. ikiwa ni pamoja na mazao ya kilimo, madini na bidhaa nyinginezo; badala ya kuwa mazao yaliyoongezwa thamani, hatua hii ya China itazinufaisha baadhi ya nchi zilizojiandaa vyema kutumia soko hili.
Hii itakuwa ni hatua ya mwanzo ya kupata pato na kuwezesha hatua ya kuelekea kwenye viwanda vya kuchakata bidhaa hizo.

Nina kumbukumbu ya ziara aliyofanya Samia huko China miaka miwili au mitatu iliyopita; na hasa picha iliyopigwa ya pamoja akiwa na Xi Jinping; picha niliyoisoma kwa masikitiko makubwa.
Katika maelezo ya ziara hiyo, iliripotiwa kwamba China wangeweza kununua soya yote ambayo ingeweza kuzalishwa na wakulima wa Tanzania.
Hiyo ilikuwa ni miaka miwili/mitatu iliyopita. Soya ni zao la muda mfupi sana shambani, miezi kadhaa tu.

Badala yake, Bashe, wakati huo kaibuka na mitaji kwa vijana na kuwagawia mashamba walime alizeti, (?), Nadhani!

Hii ni miaka miwili mitatu iliyopita, na matokeo yake; pengine wanayajuwa vijana walionufaika na mpango huo.

Maendeleo ya nchi hutokana na mipango inayoeleweka na kusimamiwa kwa weledi mkubwa. Chini ya utawala wa Samia Tanzania imepoteza muda ambao itaujutia sana na itakuwa kazi kubwa kuufidia.

Soko la uChina, na sisi tutanufaika nalo?
 
This world is a very interesting place. Mabepari ambao kwa kawaida ndio waumini wa free market economy sasa ndio wamekuwa protectionists, na communists, ambao kwa kawaida ni waumini wa planned economy, ndio wamekuwa practitioners wa free market economy.

Mchina anawakimbiza Wazungu mchakamchaka!
 
Mchina kawakaba kabali haswa!

Mwisho wa siku wanamalizia mahasira yao kwa viinchi kama Cuba!
 
Back
Top Bottom