Hii nimeiona Zenj tu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii nimeiona Zenj tu...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kibunango, Nov 26, 2008.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kuna mjane mmoja mwenye watoto wawili hapo kisiwani Zenj aliweza kukaa na wanaume wawili bila matatizo yoyote kwa zaidi ya miaka minne. Zaidi aliweza hata kuwafahamisha wanaume hao kuwa wanakula chungu kimoja, bila ya tatizo lolote...

  Akiwa ni mjane katika umri mdogo hii ni baada ya kutwangwa talaka na mumewe, mjane huyo kwa jina la Zuhura(sio jina lake halisi) alijikuta akifanya mapenzi na mume wa mtu kwa jina la Bakari(sio jina lake halisi). Walikutana katika moja ya baa mashuhuri hapo kisiwani na ni Zuhura ambae alianza kumchokoza Bakari, baada ya kumpa ofa ya bia kadhaa kabla ya kumwomba kukaa nae katika meza moja. Jioni hiyo ndani ya baa hiyo kulikuwa na rusha roho na kama kawaida ya wasichana/akinamama/akinadada wengi visiwani humo uitumia siku kama hiyo kurusha vijembe kwa mahasimu wao.

  Hata baada ya kwisha kwa rusha roho a Zuhura ambae alikuwa akitamba muda wote wa rusha roho, alimwomba Bakari afuatane nae usiku huo. Bakari alishindwa kufanya hivyo kwani mama watoto wake alikuwa akimsubiri nyumbani kwake. Hivyo siku hiyo ya kwanza ilikwisha kwa mapenzi mepesi kati yao, na kupanga kukutana tena siku ya pili katika baa hiyohiyo. Hivi ndivyo Zuhura alivyoweza kukutana na Bakari.

  Akiwa amezungukwa na warembo watatu, kijana Franko(sio jina lake halisi)alionekana mwenye furaha tele mbele ya wadada wale watatu. Meza yao ilikuwa imesheni aina kadhaa za bia zilizokuwa zimeshafunguliwa na zile ambazo zilikuwa zikisubiri kufunguliwa. Akina dada wale ndio waliokuwa wametala meza ya Franko na muda wote waliweza kuteka karibu kila mnywaji katika baa hiyo kwa vicheko vyao visivyokwisha. Ilikuwa ni wazi kuwa kila mtu alitamani kuwa katika meza hiyo. Pembeni ya meza ya Franko, alikuwa amekaa msichana mmoja ambaye kila mara alikuwa akimtupia macho Franko, hakuwa mwingine bali ni Zuhura.

  Kadili muda ulivyokuwa unakwenda ndio meza ya Franko ilivyozidi kupungukiwa na watu hadi akabaki msichana mmoja tu ambaye nae alionekana kuwa amelewa vya kutosha. Muda si mrefu msichana huyo wa mwisho nae alijiondokea zake na kumwacha Franko akiwa peke yake. Hali hii ilimfanya Franko kumkaribisha Zuhura katika meza yake, na bila kinyongo Zuhura alikaribia. Baada ya maongezi ya hapa na pale Franko na Zuhura walionekana kama ni watu ambao wanajuana kitambo, hii yote ilitokana na uwezo mkubwa wa Zuhura katika maongezi ambayo yalitawaliwa na kuwakandia wale wasichana watatu waliokuwa na Franko awali. Hata walipotosheka na unywaji wao Franko aliongozana na Zuhura nyumbani kwake. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi yao. Franko akiwa ni bachela na Zuhura akiwa ni mjane.

  Zuhura alipenda zaidi maisha aliyokuwa akiishi Franko, kwani aliweza kupata faragha bila tatizo kuliko kwa Bakari. Bakari akiwa ni mume wa mtu iliwalazimu kukutana katika nyumba za wageni katika faragha yao. Zaidi Bakari hakuwa mtu wa kutoka kila siku kama Franko, ambae kila siku jioni alikuwa akionekana katika baa mbalimbali. Muda ulivyozidi kwenda Bakari alijikuta akimpenda zaidi Zuhura kiasi cha kwenda kumtambulisha kwa mama yake. Hatua hii iliongeza kasi ya mapenzi yao kwani sasa waliweza kukutana kwa mama yake Bakari na kumaliza shida zao pasipo usumbufu wa kwenda kwenye nyumba za wageni. Ni katika hatua hii Zuhura alimkaribisha Bakari nyumbani kwao na ikiwa ni ruhusa kwa Bakari kwenda kwa Zuhura ambae alikuwa akiishi na baba yake.

  Kwa upande wa Franko hakuwa na shida sana na kuonana na mrembo wake Zuhura, kwani hata asipokutana nae baa, hujua kuwa Zuhura anatakwenda kulala kwake. Na iwapo inatokea tatizo la Zuhura kushindwa kwenda kulala kwa Franko, taarifa hutolewa mapema.

  Maisha haya ya Zuhura na mabwana wawili wasiojuana yalikwenda vizuri tu kwa muda mrefu. Bakari akitamba na Zuhura katika rusha roho huku Franko akitamba nae katika muziki wa dansi na madisco. Zuhura ambae alikuwa na marafiki wengi katika baa aendazo aliweza kuwaambia rafiki zake wasijaribu kamwe kutoa siri yake. Aliweza kuwanyamazisha kwa kuwapa ofa nyingi za bia. Marafiki hao kwa wakati tofauti walitambulishwa kwa Bakari na Franko.

  Walikuwa ni wahudumu wa baa walioanzisha kuvujisha siri ya Zuhura, hii ni baada ya Zuhura kufuruliza kwenda kwenye baa moja akiwa na Franko leo na kesho akiwa na Bakari. Kipindi hiki mkewe Bakari alikuwa amesafiri na Zuhura kwa mara ya kwanza aliweza kwenda kulala kwa Bakari, huku akipangua ratiba ya kulala kwa Franko kama kawaida yake. Siri hii iliwekwa wazi akiwa na Bakari ambapo walikorofishana na kila mtu kutimka kivyake usiku huo. Hii haikuishia kwa Bakari tu kwani siku iliyofuta Franko nae alifahamishwa hilo akiwa peke yake na hata Zuhura alipofika alimkuta Franko asie mjua. Hali haikuwa nzuri kabisa kwa Zuhura kuwapoteza wapenzi wake wawili kwa mpigo.

  Akitumia uwezo wake mkubwa wa kuongea, taratibu aliweza kumshawishi Bakari kuendelea na mapenzi yao. Kwa upande wa Franko aliwatumia zaidi marafiki zake wa kiume ambao walikuwa ni marafiki wa Franko vilevile kumrudisha katika himaya yake. Haikuchukua muda mrefu kufanikiwa kuwarudisha wanaume wale na kuendeleza libeneke. Na hata aliporudi mkewe Bakari tayali Zuhura alikuwa amekwisha mrejesha Bakari katika himaya yake kama hapo awali.

  Baada ya tafrani hiyo, Zuhura aliweza siku moja kuwakutanisha Bakari na Franko na kunywa nao vilivyo, siku hiyo ilikwisha kwa Zuhura kwenda kulala nyumbani kwake akiwaacha Bakari na Franko wakiendelea na vinywaji vyao kama sio maadui. Hii iliwashangaza watu wengi sana waliokuwa wanajua alichokuwa akifanya Zuhura. Gumzo la wanaume hao kukutanishwa katika meza moja pasipo kutokea aina yoyote ya ugomvi lilidumu kwa muda mrefu kwa waendaji wa baa hiyo, huku wengi kama mimi kushindwa kuelewa ni kwa namna gani aliweza kuwakutanisha pasipo aina yoyote ya ugomvi.

  Leo hii Zuhura ameolewa tena na amepata watoto wawili zaidi na bado anakutana na Bakari na Franko katika muda aupendao.
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  hadithi hii inatufundisha nini?
   
 3. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nawaaambiaga watu kwamba haya tunayoyaita mapenzi ni kielelezo cha ubinafsi wetu tu uliotukuka. Tunajisikia mno kumilikiana, ndio maana mababu waka invent hii kitu inaitwa ndoa ili kukidhi haja ya ubinafsi wetu.

  Kama mwanamke mmjoja-mwanamme mmoja ingekuwa natural, basi mungu angeweka jinsi kiasi kwamba yako wewe haingii kwa mwanamke mwingine ila yule mmoja tu. Na mwanmke yule hawezi kuingiza ya mwengine isipokuwa yako.

  Kwa hiyo ndoa sio natural, lakini mapenzi ni natural, na hayana mipaka mwanetu. Waweza penda hata mia kwa wakati mmoja. Sema kwa sababu ya ubinafsi wetu na kutaka kumilikiana tu ndio vikaja vitu kama uboifrendi, ugelifrendi, na ndoa. Hivi vyote sio natural. Na tunatumia muda mwingi kujifunza kujifanya kama vile hatujui hilo. :)
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji for the poor man, lol.
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Fissadi Jones, ulikuwepo Woodstock nini mwanangu? Au ni "Burning Man"?
   
 6. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lol

  Hata sikuwahi kuzisikia ... nimeziangalia sasa hivi nikacheka sana ...

  Hapana kabisa mtu wangu. Hizo ni fikra zangu "potofu" tu mwana ...
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Jaribu kumsoma Fisadi Jones...
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa watu filosofi ya kizuri kula na wenzako watu hawataki kuisikia chao chao...
   
 9. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  Pia ujue kuwa Ubinafsi ni Natural behaviour ya Binaadamu sote, so kama unaamini katika Nature basi usikatae UBINAFSISHAJI wa milki kama unavyoupinga hapo juu. huo ndio utu. Mwanadamu bila ubinafsi sio Mtu, angali hata akifikwa na jambo kamwe halii, MUNGU WETU, bali atalia "MUNGU WANGU" anam binafsisha hata Mungu aliye wa Wote kuwa ni wake pekee. hiyo ndio natural.
   
 10. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nina shida na hii lugha jamani! Mjane ni mtalaka ama ni mfiwa? Kama ni mtalaka ina maana wote wenye talaka ni wajane? Kiswahili hiki! Balaa
   
 11. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwetu Kigoma
  Mjane ni aliyefiwa na mwenzi (mke/mume)
  Mtalaka ni aliyetalikiwa

  Je wewe Eeka Mangi ni Mtalaka?
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...maambukizi ya ukimwi at its very best??:rolleyes:
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wenye talaka ni wajane vilevile...
   
 14. S

  Stone Town Senior Member

  #14
  Dec 1, 2008
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari za wakati huu vijana na wazee.

  hii story ya mjane na wanaume wawili nimeisoma yote bila ya kuacha mstari hata mmoja lakini nilichokiona hapa sio kigeni sana na sio kwa zenj tu kama alivyosema mwandishi suala hili ni maarufu sana kila sehemu kwa sababu kadhaa lakini moja ikiwa ni tatizo la pombe unapokunywa pombe ukabobea unaweza kufanya jambo bila ya makusudio.

  lakini jengine huyu mama ni mjane na kama tunavyofahamu hajafungwa asifanye mambo kama hayo ukitoa imani yake ya kidini aliyonayo amejiona yuko huru kufanya nalolitaka muhimu kwake ni fedha na kama tunavyojua fedha ni sabuni ya roho kwa hivyo kuwachanganya wanaume wawili kwa wakati mmoja ni jambo dogo sana kwa wanawake kwa sababu wanawake wana mbinu nyingi za namna hiyo.

  na msishangae kuwa yeye mjane ameweza kuwaweka wanaume wawili pamoja hata mke wa ndani ya nyumba anaweza kumchanganya mumewe kwa kujidai mwanamme fulani ni kaka yake kumbe jamaa anakula sahani moja mumewe. hizo ni mbinu za wanawake tu ambazo ni nyingi sana.

  suala la wivu sio sana kuja kwa kuwa mtu unayemkuta baa huwa mara nyingi anakuwa sio wako maana umemkuta katika shughuli zake hivyo hata ukitaka kum control anaweza akakutoa nishati kwa kukujibu usini control mimi kwani umenikuta na shida mimi? si kiherehere chako tu cha kunifata mimi kama unataka kuniletea ujinga wa kunionea wivu niwache maana mimi nina wapenzi kibao na ukiondoka wewe wanakuja wengine.

  wanaume muwe makini na wake zenu sisi tumejaaliwa kuna na vituko vikubwa vya udanganyifu kwa waume zetu Mungu atustiri
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nisingeshangaa sana kama Zuhura angelikuwa anatafuta pesa, kupitia kwa hao wanaume, kwani kipindi hicho alikuwa na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu. Hakuwahi kufanya kazi ya kuajiliwa, ila ni mfanyabiashara mzuri sana na wenye kujiweza na ziada kuitumia atakavyo.

  Kinachonishangaza ni kuwa yeye ndio aliyekuwa akiwafadhili hao wanaume wake na sana katika baa. Zaidi hata chakula akiwanunuliwa iwapo wapo katika hali mbaya kifedha. Kiumri alikuwa ni mdogo kwa wanaume hao...Hivyo kumweka kwenye kundi la masuga mami sio sahihi. Je cheo chake cha ujane ndio kilisababisha yote haya?

  Sijui hii ni aina gani ya mapenzi, jee inawezekana kuwa alikuwa atosheki na mwanaume mmoja? ni kitu gani kilichokuwa kinamfanya awe na hamu ya kulala na wanaume wawili katika siku moja, akipanga zamu ya mmoja mchana na mwingine usiku? Yapo mengi ya kujiuliza kuhusu tabia kama hii...
   
 16. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #16
  Dec 2, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa logic hiyo basi tunaweza kuhitimisha kwamba viumbe wote wenye uhai ni wabinafsi. Kitu ambacho kingeongeza utata katika nini tunaamnisha ubinafsi hapa. Je, ubinafsi wa wale jamaa wanaojilipua kule mashariki ya kati uko wapi? Kama ingekuwa kwambo wote ni wabinafsi naturally, je mbona wengine wako tayari kujilipua na wengine hawako tayari? Yupi kati ya hawa ni mbinafsi.

  Kama nature au nurture, whichever the case, nadhani tunatofautiana mno kwenye kiasi gani tunaendekeza ubinafsi wetu. Na ipo ndani ya uwezo wetu ku-control ubinafsi wetu, na kuchagua ni kwa kiasi gani unatawala maamuzi yetu na tabia zetu.

  Wewe na Nyerere, kwa mfano, mnaweza kuwa tofauti sana kwenye kiasi gani mnaendekeza ubinafsi wenu :). Wakati kwake yeye ilikuwa sawa tu kuondoka madarakani bila mali kedekede (hata kama alikuwa anatamani kuwa nazo), wewe ungekuwa bize kujilimbikizia kwa sababu huwezi kuu-control ubinafsi wako. Kwa hiyo watu tunatofautiana.

  Hizi ndoa unajua zilianzia wapi? Zamani tulikuwa kama kuku tu; unanyatia liye karibu na kupandia. Kama huna ubavu unatolewa nduki, kama unao ndio kama vile. Ila sasa libaba lenye mabavu anamiliki majike na kuhakikisha vidume vingine vinakaa mbali. Na hii ilisaidia sana kwenye ile kitu wengine wanaita natural selection, kuhakikisha kwamba tunakuwa na watoto wanaotoka katika mababa yenye ubavu.

  Lakini baadaye sana, binadamu katika jamii tofauti tofauti wakafanikiwa kutengeneza taratibu za jinsi gani ya kumiliki bila kupigana, maana process ya kutafuta mwenye ubavu zaidi ilikuwa inapoteza wengi. Ndio zikaja ndoa sasa, na kila jamii ikawa na jinsi yake ya kuwa-machisha na kuwafungisha ndoa. Wengine wazazi wanakubaliana, wengine unamkwiba na kuficha kwa siku kadhaa, wengine inabidi uue simba kwanza, etc.

  Na ndoa hizi zilikuwa zinamaanisha vitu tofauti-tofauti kwenye jamii tofauti-tofauti. Wengine ukishaoa waweza kuoa na mwengine, Wengine ukishaoa ndio basi tena, wengine ukishaoa ruksa kuwa na nyumba ndogo, wengine kuwa na nyumba ndogo lazima mke mkubwa aridhie, wengine mke mkubwa ndio anakutafutia nyumba ndogo, etc.

  Kwa hiyo nyie kabla hamjaambiana "sawa", hebu jaribuni kuzungumza mnakubaliana nini kwanza. Maana inawezekana mwenzako hajui kwamba nyumba ndogo marufuku.
   
 17. M

  Mama JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Ubinafsi ni tabia ya wanyama wengi. Tabia hii kibiolojia inaitwa territorial behaviour. Binadamu kama alivyo simba wanamiliki boma zao na hawapendi kuingiliwa kwenye hayo materritory yao.

  Katika bold nyekundu umesahau kuwa kuna wengine wanawake pia wana mamlaka ya kuwataliki waume zao (haki ya kuvunja ndoa pia).
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Dec 2, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Oh really??????????
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Jibu rahisi mkuu alitaka magoli ya nyavu ndogo(wajua soka wanajua)
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hapa labda kuna tofauti za kilahaja katika matumizi ya neno mjane.

  Kadiri ninavyojua mimi kiswahili cha Mrima, Mvita na kote kwengine bara mjane ni mwanamke aliyefiwa na mumewe.Mwanamke aliyeachwa haitwi mjane.

  Sina hakika kuhusu matumizi ya neno mjane katika lahaja za Unguja na kwingineko visiwani.

  Kuhusu hili swala la umewenza, kuna siku nilimsikia Erika Baduh anahojiwa kwenye redio akasema kuna kabila West Africa ambako mwanamke anaolewa na mume zaidi ya mmoja, alilitaja kabila lakini sikumbuki. I am not sure if this is verifiable or just Erikah being her magnanimous Baduist self.
   
Loading...