SI KWELI Hii ni taarifa ya CHADEMA kulaani maandamano ya Desemba 09

SI KWELI Hii ni taarifa ya CHADEMA kulaani maandamano ya Desemba 09

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
CHADEMABARUA.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikisema Chama cha Demokrasia na Meaendeleo (CHADEMA) kinauarifu umma na Jumuiya ya Kimataifa kuwa kinalaani vikali maandamano yanayoratibiwa kufanyika Desemba 9 Mwaka huu. Maandamano hayo ni kinyume na msimamo wa Chama na yanakiuka taratibu za kisheria za nchi.

Aidha taarifa hiyo inaongeza kuwa CHADEMA haitambui maandamano hayo kwa kuwa mchakato wake haujapata baraka za Uongozi wa juu wa Chama nakuwaomba wanachama na wafuasi kutoshiriki maandamano hayo.

Je, taarifa hiyo ni halisi imetolewa na CHADEMA?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijachapishwa katika ukurasa rasmi wa CHADEMA.

Aidha taarifa hiyo imetengenezwa kutoka kwenye taarifa rasmi ya CHADEMA iliyotolewa Novemba 30, ikieleza kuzuiwa kwa viongozi wa Chama hicho kuona na mwenyekiti wa Chama aliyepo gerezani, ambapo inaanza kwa kusema "Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinauarifu umma na Jumuiya ya Kimataifa kuwa" maneno haya yakitumika pia kwenye taarifa iliyotengenezwa.

Aidha katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alipotafutwa ili kuthibitisha uhalali wa barua hiyo aliikanusha akisema taarifa hiyo si ya kweli wala haijatolewa na chama hicho.​
Back
Top Bottom