Hesabu kutoku-balance ni mwiba unaowatesa watoa huduna za kifedah kwa njia ya mtandao (M-Pesa,Tigo Pesa, Airtel Money)

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Ukiachana na hasara nazo zipata ndugu yetu mfuga kuku kwenye biashara yake kutokana na uzembe wa kuto fatilia mwenendo wa biashara yake bado Tatizo la hesabu kuto ku balance ni Tatizo kwa wafanya biashara wa huduma za KIFEDHA.

Mimi ni mkongwe pia kwenye biashara hii na hili Tatizo ni janga pia kwangu Kuna wakati unakaa unawazaa Nini kimesababisha? Unakosa majibu. Bahati mbaya hatuna CCTv camera kufatilia wateja kama ulizidisha pesa wakati wa kutoa pesa kwa mteja.

Kuna siku nikabaini Tatizo la salio kuto kubalance kupitia laini yangu ya uwakala baada ya kufanya miamala, nikagundua Voda walikata salio, baaadae wakaliongeza zaidi ilikua mchana na jioni yake wakalikata salio walio ongeza ila wakakata na 2000 yangu.

Niliripotia Tatizo Hilo kupitia Vodacom WhatsApp lakini hawakunipa ufafanuzi mpaka leo, nimeweka na ushahidi wa picha hapo chini.

Nikiwa Kama mkongwe kwenye biashara hii nakiri wazi kua hili Tatizo la salio kuto ku balance na linachangiwa na vitu vingi Sana.

Moja wapo ni -

* Kuzidisha pesa wakati wa kumpa pesa mteja au kutuma pesa. na usipo kua makini katika akili yako hili litakuhusu.

* Chuma ulete naweza kukiri wazi kua hili Tatizo lipo ila moja Kati ya njia ya kulidhibiti ni kufunga hesabu mala kwa mala yaani kutwa mala tatu kama dozi ila Mimi nakiri wazi kutwa mala tatu hua nakua mzembe, hua nafunga mala moja tu kwa siku.

Wadau wanasema kua chuma ulete hachukui pesa iliyo hesabiwa yeye anadili na pesa iliyo "shaghala baghara." Aka landamlee hapo ndipo anapita nazo. Ila Sina uhakika Sana na njia hii ya udhibiti ila inasaidia.

* Wizi na udokozi wa mfanya kazi au mtu wa nje ya ofisi anaweza kuwa kibaka au mtu Aliye zoea Sana kuingia ofisini kwako .. hii inatokea na usimwamini mtu % Mia weka udhibiti wa fedha zako. Usiruhusu kila mtu mtu kuizoea ofisi yako kisa tu ni mshikaji wako.

Mimi binafsi jumapili hua sio siku rasmi ya kazi mfano Jana nimefungua saa 9 jioni nikafunga saa Moja skupiga hesabu.

Leo mchana nimefunga hesabu nimekuta loss ya 20k yaan ndani ya siku tatu nimetengeneza hasara ya 30k hapa kichwa Cha Moto sjui imepoteaje poteaje. Ila najilaumu Sana Jana kutokufunga hesabau.

Mala nyingi ninapo funga mwenzi hua sikosi hasara ya 20k,10k, 5k, ila kamisheni hunisaidia na kupaisha mtaji kila mwisho wa mwezi.

Mpaka hapa bado najifunza namna Bora ya kuendesha hii ofisi kiukweli ina changamoto.

Screenshot_20230123-175238.jpg
 
Hii biashara Mimi nimeifanya tangu 2018 mpaka leo hayo unayoyaelezea nakutana nayo mkuu , niliwahi kuwafuata Hadi wale masuper agent wakubwa nikawashirikisha , nikawauliza wanawezaje kuhimili hii changamoto , au Kama Kuna dawa tupeane, niliambiwa tu piga hesabu unapofungua na unapofunga ofisi , kingine usimwamini mtu , Lakini Kuna jamaa akaniambia hizo ofisi zao wameajiri watu kwa hiyo ikitokea loss anabebeshwa mfanyakazi , boss ye hapati hasara,.
Na wale wafanyakaz ukiwafwata wanakuambia loss zinatokea nyingi sana , sehemu kubwa ya mshahara wao huwa wanakatwa kwa ajili ya kufidia pesa iliyopotea ,

Nina mwaka mmoja Sasa hii biashara naifanya Kama biashara ya pemben mteja ukija Sina salio sihangaiki kwenda kuweka float , ukikuta Nina salio nakuhudumia usipolikuta basi ,. Nimeamua kuweka mtaji sehemu nyingine ambayo nitaweza kuisimamia vizuri ,
 
Kiukweli ni pasua kichwa japo kua ukiwa na mzunguko baadhi ya hasara hufidishiwa pia na commission.
 
Mku ondoa kwanza chumaulete, hakuna chumaulete

Pesa ya mtaji usiiguse, hata chakula toa pembeni

Mteja mwenye haraka mwache aende, kuwa makini hasa kwenye pesa kubwa.

Kamwe kamwe usitume pesa kabla hujapokea pesa.

Hii biashara inafaa zaidi penye mzunguko mkubwa wa watu

Ni biashara yenye risk kubwa usipokuwa makini.
 
Hivi kwanini kampuni zilizo nyingi ambazo zimesajiliwa bongo ni seheme ya uwizi na huwa ukiripoti ndio kwanza hawaangaiki na hili, na serikali pia kwa namna moja inashirikiana nao maana vyombo husika vipo hatua hazichukuliwi
 
Pole sana mkuu.
Ukiachia makosa ya kibinadamu ambayo yanasababisha fedha kupotea mfano. Kuzidisha hela badala ya 1000 kuwa 10000
Ukiachia kutuma hela na kisahau kuchukua hela
Ukiachia kukosea kutuma hela na ikawa imeshatolewa

Kunavisababishi vingine vinavyofanya hela kupotea ambavyo havionekan na n vya kufikirika ila madhara yake ndo kama hayo unayosema.
Kuna hiyo chuma uletee ambayo inaumiza weng katika biashara mbali mbali. Pia watu kuiba moja kwa moja ila wale watu wasionekana
 
Back
Top Bottom