Hii ni kwa akina dada tu

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,799
2,725
Jamani naomba mnipe uzoefu wenu akina dada hasa kwa wale wenye hii tabia ya kuzira kuongea na wenzi wenu na kusitisha huduma zote wakati mwingine bila taarifa. Yaani bila hata ya mhusika kujua hasa chanzo cha hivyo vikwazo vya kimahusiano.

Hivi huwa mnapata faida gani au kuna satisfaction gani mnayopata kwa kuamua kuzira kuongea, kula, kutoa huduma nyeti na wakati mwingine kupika?

Poleni kwa wale mtakaokwazika kwa hili swali.
 
Mbona kwangu mimi ni kinyume chake anazira mwanaume!!:redface:
Hata sijui wanafaidika na nini wakizira haswa maana mm mambo hayo siyawezi,kama umekerekwa unasema,mnajadiliana yanaisha Life goes on,sio watu wiki nzima wamenuna kha!!
 
Mbona kwangu mimi ni kinyume chake anazira mwanaume!!:redface:

mimi49 itabidi tuanzishe na thread kwa ajili ya wanaume wa aina hiyo. Huyo jamaa yako ana umri gani vile?
 
huwa tunaona tumewakomesha sana....na ukibembeleza basi roho kwatuu....yaani burudani....
ila ongea nae mwambie hupendi.....
 
kuzira ndio nini? ni kiswahili hiki?

Mbona akina dada wengine wameelewa. Inawezekana wewe ama huna hiyo tabia au ni mvamizi tu. Kwa ufupi neno kuzira hapa limetumika kumaanisha kususia jambo lolote. Watoto wadogo wanayo sana hii tabia ya kususia mambo hasa wanapoudhika na neno lolote. Kwa watoto neno la kimombo linalotumika kuelezea tabia hii ni "to throw tantrums" kama sikosei.
 
Wanawake ni viumbe vinavyopenda kubembelezwa kususa kwao ni ili wabembelezwe jamani.sasa utakapojifanya na ww hujui kubembeleza hapo ndo kazi itakapokuwepo ila kwa wenzangu na mm ni kujishusha tu mapemaaa.
 
ndo kudeka huko babu ....bembeleza mkuu....
imba nyimbo nzurinzuri...
peleka out..
ogesha....
mmmmmmmmmmmmmmh
 
Mbona akina dada wengine wameelewa. Inawezekana wewe ama huna hiyo tabia au ni mvamizi tu. Kwa ufupi neno kuzira hapa limetumika kumaanisha kususia jambo lolote. Watoto wadogo wanayo sana hii tabia ya kususia mambo hasa wanapoudhika na neno lolote. Kwa watoto neno la kimombo linalotumika kuelezea tabia hii ni "to throw tantrums" kama sikosei.

kususia na tantrums ni vitu viwili tofauti lakini nimewapata kumbe ni kususia thx
 
Raha yoote iko kwenye makeup! Yaani kuna saa unatamani ugomvi ili mpatane. Raha yake ukute anaejua kumbembeleza. Kama wewe hujui kubembeleza usimtese mtoto wa watu, muache aende zake.
 
nakwambia ukimpata wa kumdekea, halafu anajua kabisa anatakiwa akubembeleze na ka zawadi, uwiiiiiiiiiiiiiii! ni tamuje jamani second chance yoyote??? hamu haiishi kwenye penzi. bembeleza kaka, usiwe na roho ya kauzu! lol
 
Tata binafsi huwa sioni kama hili ni tatizo sana kwani kuzira ni tabia aliyonayo binadamu kuonyeha hajaridhika/hajafurahishwa na jambo au kitu fulani. Tofauti ni namna ya kui-express na ku-deal nayo. Na hii haiko kwenye mapenzi tu, hata madaktari walizira

Kwangu mimi njia nzuri ya kuiepusha kuzira ni ku-deal na source (mara nyingi ni maudhi), wala siyo kumkaripia eti kwa kuwa amezira ili hali ana-express dissatisfaction yake!

Oooho! kumbe uliuliza kina dada tu, samahani sikusoma vizuri nikajikuta nimeishaandika!
 
kudeka.com! Kama mwanaume hajui kubembeleza inakuwa kununiana.com! Ila kununa c vzur wadada! Tuwe wawaz kama m2 kakukera unamwambia hakuelew bora ugeuke mzungu unampa vbao vya shav vwil! Mwenyew atajbeba mbele ya safar!
 
nakwambia ukimpata wa kumdekea, halafu anajua kabisa anatakiwa akubembeleze na ka zawadi, uwiiiiiiiiiiiiiii! ni tamuje jamani second chance yoyote??? hamu haiishi kwenye penzi. bembeleza kaka, usiwe na roho ya kauzu! lol

kwa mtindo huo mtatufilisi cacico, loh!
 
kwa umri huo wa 37years ni hormonal changes anelekea kwenye menopause kaka
so takecare.
 
Back
Top Bottom