DZUDZUKU
JF-Expert Member
- Nov 8, 2012
- 3,907
- 2,092
Hii ni kama hadithi kwa wengine, lakini ni hali halisi inayowatokea walimu wenzangu, katika shule ile ya kata.
Wakati shule ikitaka kuanzisha, wanakijiji walihamishiwa mashamba yao na serikali ili kupisha ujenzi wa shule hii, baada ya hapo shule ikajengwa, na wanafunzi pamoja na walimu walipo anza kazi.
Kumbe jambo hili halikupendeza machoni pa wanakijiji hao, hapo ndio mwanzo wa mkasa ulipo anza.
Baada ya shule kuanzisha haikuchukua hata zaidi ya mwaka, mkuu wa shule aliaga dunia katika mazingira ya kutatanisha, si yeye tu mwaka huo na mwalimu wa kawaida pia alipoteza maisha.
Serikali haikuchoka, ikaleta mkuu mwingine, nae hakuchukua round, akafa, hivi sasa yupo mkuu wa shule mwingine nae mda huu, amelazwa rufaa Mbeya baada ya kutapika lita 10 za damu.
Si hayo tu, juzi juzi tu mwalimu alikuwa darasani anafundisha mara akaona mjusi umedondoka, lakini alishangazwa na kelele za wanafunzi wakidai aliedondoka sio mjusi bali ni MAMBA.
Mwalimu mwingine akiwa ametoka nyumbani kwake kuelekea shuleni, alikutana na wanafunzi na wakamwambia, mbona leo unakuja shuleni ukiwa UCHI?
Baada ya kuona visa vinazidi walimu waliamua kugoma kuingia darasani kufundisha, ndipo kikao kilipo itishwa na wanakijiji kuanza kutuhumiana, watuhumiwa wapo, bahati mbaya wanakataa kuhusika na ufedhuri huo.
DEO alifika katika shule hiyo na kuongea na walimu pamoja na kuwaomba waingie darasani huku wao wakilishughulikia jambo lao.
MAMBO HAYA YANATOKEA KATIKA KATA YA NGONGA, WILAYA YA KYELA.
Chanzo cha taarifa hii ni Kyela Fm radio.