Hili la utekelezaji wa mtaala, walimu wa darasani ndiyo wapewe semina ya moja kwa moja na si viongozi

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Hapa ndo serikali inapobugi kabisa na elimu inafeli kwa sababu inafanya vitu visivyo na tija

Nimeona semina zimeanza za utekelezaji wa mtaala mpya lakini wanaoitwa kwenye semina za moja kwa moja ni maafisa elimu wa mikoa, Wilaya, kata na wakuu wa shule na kwa nafasi za hao watu si watekelezaji wa mtaala moja kwa moja bali ni wasimamizi tu wanaacha walimu wa darasani ambao ni watu muhimu katika kutekeleza mtaala kwa asilimia.

Mwalimu wa darasani ndiye kila kitu kwenye utekelezaji wa mtaala hao viongozi ni wasimamizi tu, semina zianze na walimu wa darasani na si vinginevyo.

Wasioingia madarasani ndo wanapata semina ila wale wanaokuwa na walengwa wa mtaala (wanafunzi) na watekelezaji hawana semina, hapa serikali imechemka ile mbaya na kufeli kwa wanafunzi na elimu kunaanzia hapa.

Semina za utekelezaji wa mtaala zitolewe kwa walimu wa madarasani moja kwa moja na siyo viongozi wa elimu
 
Hela ya kuwapa walimu laki 5 haziwezi patikana.
Hela za kuwalipa watu waliokaa bunge la katiba zikapatikana na katiba haikupatikana sh laki tatu za kuwalipa walimu laki 5 zinakosa! Kumbuka elimu ndo moyo wa nchi
 
Back
Top Bottom