Hii ni kama hadithi kwa wengine, lakini ni hali halisi inayowatokea walimu wenzangu.

DZUDZUKU

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
3,907
2,091
Hii ni kama hadithi kwa wengine, lakini ni hali halisi inayowatokea walimu wenzangu, katika shule ile ya kata.

Wakati shule ikitaka kuanzisha, wanakijiji walihamishiwa mashamba yao na serikali ili kupisha ujenzi wa shule hii, baada ya hapo shule ikajengwa, na wanafunzi pamoja na walimu walipo anza kazi.

Kumbe jambo hili halikupendeza machoni pa wanakijiji hao, hapo ndio mwanzo wa mkasa ulipo anza.

Baada ya shule kuanzisha haikuchukua hata zaidi ya mwaka, mkuu wa shule aliaga dunia katika mazingira ya kutatanisha, si yeye tu mwaka huo na mwalimu wa kawaida pia alipoteza maisha.

Serikali haikuchoka, ikaleta mkuu mwingine, nae hakuchukua round, akafa, hivi sasa yupo mkuu wa shule mwingine nae mda huu, amelazwa rufaa Mbeya baada ya kutapika lita 10 za damu.

Si hayo tu, juzi juzi tu mwalimu alikuwa darasani anafundisha mara akaona mjusi umedondoka, lakini alishangazwa na kelele za wanafunzi wakidai aliedondoka sio mjusi bali ni MAMBA.

Mwalimu mwingine akiwa ametoka nyumbani kwake kuelekea shuleni, alikutana na wanafunzi na wakamwambia, mbona leo unakuja shuleni ukiwa UCHI?

Baada ya kuona visa vinazidi walimu waliamua kugoma kuingia darasani kufundisha, ndipo kikao kilipo itishwa na wanakijiji kuanza kutuhumiana, watuhumiwa wapo, bahati mbaya wanakataa kuhusika na ufedhuri huo.

DEO alifika katika shule hiyo na kuongea na walimu pamoja na kuwaomba waingie darasani huku wao wakilishughulikia jambo lao.

MAMBO HAYA YANATOKEA KATIKA KATA YA NGONGA, WILAYA YA KYELA.

Chanzo cha taarifa hii ni Kyela Fm radio.
 
Chanzo cha maswahibu hayo ni nini? Kama sikosei sehemu hiyo ya ngonga ndio kwa akina Mwakyembe and General Mwamunyange.
 
wewe

ninahadisiwa na mwalimu mkongwe shule moja hapa dar iko town na ni kongwe sihitaji jina
HIVI JUZI WANAWASACHI WATOTO BANGI MWANAFUNZI MMOJA KAKUTWA NA HIRIZI ALAFU AKAGOMA AKAWA ANATAKA ARUDISHIWE IRIDHI YAKE BASI AKAAMBIWA AKAMUITE MZAZI BASI MZAZJ AKAJA WAKACHUKUA IRIDHI YAO MPAKA SASA HUYO MTOTO YUPO

YAANI WALIMU WANAENDELEA KUFUNDISHA YEYW BADO YUPO NA NAHIS NA IRIDHI YAKE CLASS

sembuse mbeya tena mliwaamisha watu katika mashamba
 
msiende shulen mnaenda kufanya nini? ualimu siku hizi sio wito.!

Kuna kipindi wanakijiji na wanafunzi walifunga barabara ili walimu wasiende shuleni, ile kesi ilikuwa kubwa na ndio iliosababisha mkuu wa shule wa kwanza kufariki.
 
Chanzo cha maswahibu hayo ni nini? Kama sikosei sehemu hiyo ya ngonga ndio kwa akina Mwakyembe and General Mwamunyange.

Kikubwa inaonekana kama waliotoa mashamba kwaajili ya shule hawajaridhika na jambo hilo.

Ni kweli Ngonga ni kwa Mwakyembe kijimbo na Mwamunyange kiuzao-nyumbani kwake.
 
wewe

ninahadisiwa na mwalimu mkongwe shule moja hapa dar iko town na ni kongwe sihitaji jina
HIVI JUZI WANAWASACHI WATOTO BANGI MWANAFUNZI MMOJA KAKUTWA NA HIRIZI ALAFU AKAGOMA AKAWA ANATAKA ARUDISHIWE IRIDHI YAKE BASI AKAAMBIWA AKAMUITE MZAZI BASI MZAZJ AKAJA WAKACHUKUA IRIDHI YAO MPAKA SASA HUYO MTOTO YUPO

YAANI WALIMU WANAENDELEA KUFUNDISHA YEYW BADO YUPO NA NAHIS NA IRIDHI YAKE CLASS

sembuse mbeya tena mliwaamisha watu katika mashamba

Afadhali ya hao wanaomiliki hirizi na hawauwi watu, huku wanakuua kabisa.
 
Kikubwa inaonekana kama waliotoa mashamba kwaajili ya shule hawajaridhika na jambo hilo.
Ni kweli Ngonga ni kwa Mwakyembe kijimbo na Mwamunyange kiuzao-nyumbani kwake.
Haya mambo yalitokea Shauritanga huko Rombo, Wasichana wote waliokuwa Bwenini waliungua na kisa Mzee wa watu hajalipwa eneo lake.
Moto uliwaka na chanzo hakikujulikana hadi leo, maana hakukutwa na mafuta Petrol au kiberiti
ila waliozikwa mmoja alizidi
Huko Ngonga Wanayakyusa ni wasomi sana hebu waiteni wenye Ardhi wapatanishwe
 
Hii ni kama hadithi kwa wengine, lakini ni hali halisi inayowatokea walimu wenzangu, katika shule ile ya kata.

Wakati shule ikitaka kuanzisha, wanakijiji walihamishiwa mashamba yao na serikali ili kupisha ujenzi wa shule hii, baada ya hapo shule ikajengwa, na wanafunzi pamoja na walimu walipo anza kazi.

Kumbe jambo hili halikupendeza machoni pa wanakijiji hao, hapo ndio mwanzo wa mkasa ulipo anza.

Baada ya shule kuanzisha haikuchukua hata zaidi ya mwaka, mkuu wa shule aliaga dunia katika mazingira ya kutatanisha, si yeye tu mwaka huo na mwalimu wa kawaida pia alipoteza maisha.

Serikali haikuchoka, ikaleta mkuu mwingine, nae hakuchukua round, akafa, hivi sasa yupo mkuu wa shule mwingine nae mda huu, amelazwa rufaa Mbeya baada ya kutapika lita 10 za damu.

Si hayo tu, juzi juzi tu mwalimu alikuwa darasani anafundisha mara akaona mjusi umedondoka, lakini alishangazwa na kelele za wanafunzi wakidai aliedondoka sio mjusi bali ni MAMBA.

Mwalimu mwingine akiwa ametoka nyumbani kwake kuelekea shuleni, alikutana na wanafunzi na wakamwambia, mbona leo unakuja shuleni ukiwa UCHI?

Baada ya kuona visa vinazidi walimu waliamua kugoma kuingia darasani kufundisha, ndipo kikao kilipo itishwa na wanakijiji kuanza kutuhumiana, watuhumiwa wapo, bahati mbaya wanakataa kuhusika na ufedhuri huo.

DEO alifika katika shule hiyo na kuongea na walimu pamoja na kuwaomba waingie darasani huku wao wakilishughulikia jambo lao.

MAMBO HAYA YANATOKEA KATIKA KATA YA NGONGA, WILAYA YA KYELA.

Chanzo cha taarifa hii ni Kyela Fm radio.

aaah,sasa kuna haja gan ya kuingia darasan
 
Hii inatsha mkuu bora walmu wote wagome adi suluhu ifanyke kati ya serkal na wakjj kwasababu waukumiwa wasiokuwa na atia wala kujua chanzo cha tatzo hlo.serekali ifuatilie ili mapema iwezekanavyo.
 
Poleni sana aisee, Msijitumbukize kuamini mambo ya kishirikina badala yake focus kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi, hakuna limshindalo yeye.
 
dah, yaani siamini! Nilitegemea walau wachache wajitokeze kupinga au hata to question the authenticity ya hii information lakini hata mmoja!
Hivi mpaka karne hii bado kuna watu mnaamini ushirikina kiasi hiki? Kweli watanzania bado sana!
Uchawi hakuna bw, mtaendelea kudanganywa na kukosa maendeleo kwa imani za kipumbavu!!
 
Ndio maana, heading inasema " Ni kama hadithi kwa wengine........."

haya ni mambo yanayo watokea watanzania wenzio, hushangai kuona jamii yako bado haijakombolewa?

Pia, kama unajua huduma ni nini, basi ungeuliza vizuri ili uje kuhudumu maeneo haya na sio kuzungumza kwenye KEYBOARD tu hapo.

Unamaoni gani kuhusu jambo hili ndugu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom