Hii ni HATARI kwa CHADEMA!

Mzee heshima kwako.

Mkuu hili jambo limekuwa ni sehemu ya utamaduni wa CDM lakini usiogope kosoa pale unapoona kuna kasoro bila kujali kuzodolewa muhimu ujumbe ufike.

Nimekuwa nafatilia post nyingi, na pia nimejaribu kuzungumza na watu kadhaa wanaonizunguka, kuanzia ofisini mpaka mtaani.
Nilichojifunza ni kwamba, unapojaribu kukikosoa Chadema unaonekana kama umetenda dhambi.
Unapojaribu kumkosoa Mbowe, Slaa n.k unaonekana we si mzalendo wa nchi hii. Inaonekana kama wazalendo wote wanakisifia Chadema.
Chadema kama chama kinaongozwa na binadamu kama wa ccm. Wanamapungufu yao pia kama waliyonayo ccm.
Kama unaogopa kukosolewa na kurekebishwa kamwe hautojifunza.
Chadema tubadilike, tukubali kurekebishwa.
"when think alike, no one is thinking"

NB. Nipo tayari kurekebishwa.
 
Mkuu, CHADEMA hakitaki kukosolewa/kubadilika au washabiki ndani ya mitandao ambao hawataki kukubali mawazo ya watu wanaofikiri kwamba CHADEMA inahitaji mabadiliko?

Sasa mkuu, hebu tuambie, kuna watu walikuja na mapendekezi kwamba Mbowe hawezi kuwa Mwenyekitii, je, utaratiu gani utumike kumuondoa? n je aondolewe kwa sababu gani? inatosha mtu mmoja 'kufikiri' kwamba Mbowe hafai? Inatosha mnazi mmoja wa 'Zitto' kuamua kwamba Slaa hafai kuwa Katibu??

Siasa sio rahisi kama inavyoonekana mkuu.

Viongozi hao wa CDM uliowataja wanajadiliana na viongozi wenzao kila mara wanapotaka kutoa msimamo wa Chama. Ni mawazo au mapendekezo gani wewe binafsi umepata kuyatoa yakapuuzwa?

CHADEMA tunajivunia "NGUVU YA UMMA".

Hatuhitaji kukurekebisha sana ni kukujulisha kwamba, tumenyanyaswa kwa muda mrefu na CCM , tumedhalilishwa sana na CCM, tumeibiwa sana na CCM, tumefungwa sana na CCM na sasa tumepata mkombozi wa kutpeleka nchi ya ahadi TANGANYIKA. CDM ndiyo musa wetu wa kuttoa Misri na kutupeleka Nchi ya ahadi yenye Madini na ardhi yenye rutuba , nchi yenye mbuga za wanyama wa kila aina na nchi ya watu wakalimu.

nami pia natamani hivyo. Safari itakuwa nzuri sana kama tutayarekebisha mapungufu yetu mapema.
 
Ngoja nami nijaribu kuorodhesha mapungufu ya CHADEMA yetu:
-Mtandao hafifu wa kichama.
-Mashabiki wengi kuliko wanachama ambao hata kadi za kupiga kura hawana.
-Wanachama wenye jazba, hasira na munkar kupita kiasi. Hijab ya yule DC Fatma imewagharimu kura nyingi tu.
-Mawakala wa kukodi wa nini? Kura zinapigwa na wanaIgunga. CHADEMA haiwaamini hawa.
-Hawakuwaambia wanaIgunga kilichosababisha uchaguzi ule mdogo kuwa ni CCM na magamba yake.
-CHADEMA na Viongozi wake kung'ang'ania agenda zilezile kila mahala.
-CHADEMA haijajitofautisha na CCM kwa mambo mengi tu.

Good point to start with....kwa mwenye kuchanga karata vema ataweka miguu yake na kuanza mwendo wake hapo.....

Ni kweli CCM tumeichoka sana tu lakini kama CDM itashindwa kuchora mstari wa mpaka basi kuna hatari kufika mahali tutaushi ule msemo wa "Heri Zimwi likujualo maana hata likikukula haliwezi kukumaliza"

Mvua hiyoooo yaja...........
 
Hatuhitaji kukurekebisha sana ni kukujulisha kwamba, tumenyanyaswa kwa muda mrefu na CCM , tumedhalilishwa sana na CCM, tumeibiwa sana na CCM, tumefungwa sana na CCM na sasa tumepata mkombozi wa kutpeleka nchi ya ahadi TANGANYIKA. CDM ndiyo musa wetu wa kuttoa Misri na kutupeleka Nchi ya ahadi yenye Madini na ardhi yenye rutuba , nchi yenye mbuga za wanyama wa kila aina na nchi ya watu wakalimu.
Sawa kabisa mkuu.
 
Sijawahi sikia wala ona kosa la CHADEMA na nikalilinganisha na ufisadi wa MAGAMBA huwezi kosoa palipo safi utaonekana mjinga tu siku zote. huwezi fanananisha upuuzi wa CCM na Chadema kwanza angalia tu wabunge wa ccm na chadema utajua ni wapi wazalendo.
 
Nakubaliana na huyo anayesema kuwa tuwe tunaikosoa CDM. Wakikosea warekebisheni ili wafanye vizuri zaidi. Lakini anyenirudisha kuwaza kuhusu CCM, jamani aniwie radhi, hicho ni kichaka cha mafisdi, wezi wasio na uzalendo. ufisadi wa CCM ungekuwa unasaidia watanzania tungekuwa na Umeme, bei ya sukari ingeshuka, bei ya mafuta ingeshuka, tusingelazimishwa kulipa dowans, wasingetumia pesa nyingi kama walivyofanya Igunga. Tutafakari mara kadhaa. Narudia kusema "Mshipa wa aibu kwa CCM UMEKATIKA.
 
Sijawahi sikia wala ona kosa la CHADEMA na nikalilinganisha na ufisadi wa MAGAMBA huwezi kosoa palipo safi utaonekana mjinga tu siku zote. huwezi fanananisha upuuzi wa CCM na Chadema kwanza angalia tu wabunge wa ccm na chadema utajua ni wapi wazalendo.

unaposema hauwezi kosoa palipo safi unamaanisha chadema nh wasafi?
 
Hatuhitaji kukurekebisha sana ni kukujulisha kwamba, tumenyanyaswa kwa muda mrefu na CCM , tumedhalilishwa sana na CCM, tumeibiwa sana na CCM, tumefungwa sana na CCM na sasa tumepata mkombozi wa kutpeleka nchi ya ahadi TANGANYIKA. CDM ndiyo musa wetu wa kuttoa Misri na kutupeleka Nchi ya ahadi yenye Madini na ardhi yenye rutuba , nchi yenye mbuga za wanyama wa kila aina na nchi ya watu wakalimu.

Umesema ukweli japo unauma. Kwa wakati huu CDM kinaaminika zaidi kuliko CCM ambao wanategemea nguvu ya dola na wizi wa kura
 
Mpaka CCM ing'oke ndio naweza nikaanza kuwasikiliza watu kama nyie,vinginevyo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,tunanyanyasika sana na hawa wanaojiita CCM.
 
Nimekuwa nafatilia post nyingi, na pia nimejaribu kuzungumza na watu kadhaa wanaonizunguka, kuanzia ofisini mpaka mtaani.
Nilichojifunza ni kwamba, unapojaribu kukikosoa Chadema unaonekana kama umetenda dhambi.
Unapojaribu kumkosoa Mbowe, Slaa n.k unaonekana we si mzalendo wa nchi hii. Inaonekana kama wazalendo wote wanakisifia Chadema.
Chadema kama chama kinaongozwa na binadamu kama wa ccm. Wanamapungufu yao pia kama waliyonayo ccm.
Kama unaogopa kukosolewa na kurekebishwa kamwe hautojifunza.
Chadema tubadilike, tukubali kurekebishwa.
"when think alike, no one is thinking"

NB. Nipo tayari kurekebishwa.

Please nifafanulie maneno hayo mekundu!
 
Mzee heshima kwako.

Mkuu hili jambo limekuwa ni sehemu ya utamaduni wa CDM lakini usiogope kosoa pale unapoona kuna kasoro bila kujali kuzodolewa muhimu ujumbe ufike.

Kaanzeni kuikosoa CCM kwanza mkifanikiwa ndio muhamie CHADEMA,CCM imejaa vioja watu wanatukana live mpaka wabunge,wengine wanawaita wenzao the comedy,viongozi wa juu wanaviburi wengine wanadiliki kusema"mimi sio mawingu nikalete mvua mtera"wengine wanasema wenzao wanatumia masaburi(******) kufikiria na mengine mengi,kama kweli nyie ni wakweli na warekebishaji,HEBU WAREKEBISHENI KWANZA HAWA.
 
Good point to start with....kwa mwenye kuchanga karata vema ataweka miguu yake na kuanza mwendo wake hapo.....

Ni kweli CCM tumeichoka sana tu lakini kama CDM itashindwa kuchora mstari wa mpaka basi kuna hatari kufika mahali tutaushi ule msemo wa "Heri Zimwi likujualo maana hata likikukula haliwezi kukumaliza"

Mvua hiyoooo yaja...........

Mvua gani tena hiyo ndugu?
 
Hatuhitaji kukurekebisha sana ni kukujulisha kwamba, tumenyanyaswa kwa muda mrefu na CCM , tumedhalilishwa sana na CCM, tumeibiwa sana na CCM, tumefungwa sana na CCM na sasa tumepata mkombozi wa kutpeleka nchi ya ahadi TANGANYIKA.

CDM ndiyo musa wetu wa kuttoa Misri na kutupeleka Nchi ya ahadi yenye Madini na ardhi yenye rutuba , nchi yenye mbuga za wanyama wa kila aina na nchi ya watu wakalimu.

kosoa tuone utakosoa wapi.mia
 
unaposema hauwezi kosoa palipo safi unamaanisha chadema nh wasafi?

nilichokimaanisha uchafu wa CDM si kama wa CCM maana ukikosoa CDM ambayo kwa kiwango kikubwa ndicho chama pekee kinachoibua uozo wa serikali sidhani kama tutawajenga...... cha msingi sio kuwakosoa ni kutoa ushauri wapi panalega ili pajengwe..
 
Kaanzeni kuikosoa CCM kwanza mkifanikiwa ndio muhamie CHADEMA,CCM imejaa vioja watu wanatukana live mpaka wabunge,wengine wanawaita wenzao the comedy,viongozi wa juu wanaviburi wengine wanadiliki kusema"mimi sio mawingu nikalete mvua mtera"wengine wanasema wenzao wanatumia masaburi(******) kufikiria na mengine mengi,kama kweli nyie ni wakweli na warekebishaji,HEBU WAREKEBISHENI KWANZA HAWA.

mzee ushauri wako umetulia big up
 
Back
Top Bottom