Hii hapa ni tathmini fupi baada ya mikutano michache ya hadhara ya Chadema

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,723
218,285
Kwa ujumla ni kwamba sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wote wanataka waongozwe na Chadema, ukiachilia mbali watoto wa viongozi wa CCM na binamu zao na familia zao na hao wanaojiita Chawa. Kimsingi, hao wanaojiita Chawa ni koo za viongozi wa CCM, tena wale viongozi wa juu. Mimi natokea Kyela, kule hakuna Chawa wa CCM. Hii ni kwa sababu hakujawahi kuwepo viongozi wowote wa juu wa CCM. Hata watoto wa Elias Mwanjala au Harrisson Mwakyembe si Chawa wa CCM.

Wananchi wa Tanzania wamechoshwa na dhiki isiyoisha. Kote ilikopita, Chadema wananchi wanaililia. Wanataka leo kesho utawala wa kitapeli, mabavu na dhuluma uondoke haraka. Wananchi wanataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili warudi tena kupiga kura ili kuhalalisha uchaguzi. Hebu fikiria, mnaandikisha watu mil 29 lakini wanaojitokeza kupiga kura ni mil 9 tu. Lakini kwa vile mnategemea wizi wala hamjali kitu, mpinzani anapata kura mil 7.6, wa kwenu anapata chini ya kura mil 1.5 lakini anatangazwa kapata kura mil 12. Kazitoa wapi ikiwa waliojitokeza hawakuzidi 10mil?

Mpaka leo, Tume ya Uchaguzi ya Tanzania haikuweka kwenye tovuti yake matokeo ya Urais 2020. Unadhani ni kwanini?

Kwa kadiri ya macho yangu kwenye mikutano ya hadhara iliyopigwa na Chadema kanda ya Nyasa na kwingineko, yafuatayo yafanyike:

Chadema Digital iongezewe nguvu kila jimbo. Mahitaji ya watu kujiunga na Chadema ni makubwa mara 10 zaidi kuliko wakati wowote. Wengi wanaiita kadi ya Chadema kama Kadi ya Uhuru na kujitambua, kwamba ukiwa na kadi ya Chadema unaonekana unajitambua na pia unaonekana ni mpigania haki. Heshima yako kwenye jamii inaongezeka.

Yaanzishwe maduka ya Sare na Magwanda ya Chadema kila Jimbo. Mahitaji ya mavazi haya sasa yanatakiwa kwa zaidi ya mara 10 kuliko awali. Binafsi, nimelazimika kugawa zaidi ya sare zangu 7 za Chadema, yakiwemo magwanda yangu makali mawili kwa wenye uhitaji.

Mambo haya ni muhimu sana yakafanywa haraka.

JamiiForums195514995_540x540.jpg
 
Kitu ambacho ni cha ukweli kabisa kilichotokea kwenye mikutano ya CHADEMA ni viongozi waandamizi kusifu uongozi wa Mama Samia na kuwasihi ninyi wafuasi muongelee mema ya Mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM. Viongozi wenu akiwemo Mbowe na Lema wameonyesha wazi kufurahishwa na uongozi wa Mama. CHADEMA wekeni nguvu kwenye nafasi za udiwani.
 
Chawa umesoma uzi lakini?
 
Kwa ujumla ni kwamba sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wote wanataka waongozwe na Chadema , ukiachilia mbali watoto wa viongozi wa ccm na binamu zao na familia zao na hao wanaojiita Chawa , kimsingi hao wanaojiita Chawa ni koo za viongozi wa ccm , tena wale viongozi wa juu...
Inabidi tu nikupe 'like', kwa sababu ninaiamini dhamira yako na wengine ndani ya chama hicho.

Zaidi ya hapo, ninayo mashaka makubwa sana juu ya hatma ya chama chenu.

Nadhani itabidi tuweke maombi maalum kuinusuru CHADEMA.

Muda si mwingi, huenda italazimu kumpa heshima za kipekee kabisa Tundu Lissu.
 
Kitu ambacho ni cha ukweli kabisa kilichotokea kwenye mikutano ya CHADEMA ni viongozi waandamizi kusifu uongozi wa Mama Samia na kuwasihi ninyi wafuasi muongelee mema ya Mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM. Viongozi wenu akiwemo Mbowe na Lema wameonyesha wazi kufurahishwa na uongozi wa Mama. CHADEMA wekeni nguvu kwenye nafasi za udiwani.
Samia hatogombea 2025
 
Lissu yuko mbioni kurejea , kwahiyo kama unayo heshima ya kumpa tutakuandalia mkutano wa hadhara
 
Hapa hamna utafiti bali kuna unafiki. Hilo hata wewe mwenyewe rohoni na kichwani unalijua.

Sema ndo hivyo njaa haina mjanja wala baunsa. Pambana tu mkuu ili usevu tumbo lako.
hivi kuna wanaoshiba kwa kuandika JF ?
 
Kwa ujumla ni kwamba sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wote wanataka waongozwe na Chadema , ukiachilia mbali watoto wa viongozi wa ccm na binamu zao...
Nitajie IDADI ya waliowaunga na kusema tumechoka na dhiki ya Tanzania. Maana mikutano mingi mlioifanya ata Mimi nimehudhuria kikamilifu, ila wanashangaa kuona hotuba zenu Bado Zina visirani Kwa shujaa alieko Mikononi Kwa YESU mbinguniii.
 
Imeandikwa , atendaye dhambi atahukumiwa , yaani uue watu halafu eti uwe mikononi mwa Yesu !
 
Kitu ambacho ni cha ukweli kabisa kilichotokea kwenye mikutano ya CHADEMA ni viongozi waandamizi kusifu uongozi wa Mama Samia na kuwasihi ninyi wafuasi muongelee mema ya Mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM. Viongozi wenu akiwemo Mbowe na Lema wameonyesha wazi kufurahishwa na uongozi wa Mama. CHADEMA wekeni nguvu kwenye nafasi za udiwani.
Ntakutukana tusi nifungiwe Jukwaa Huru Kusini mwa Jangwa la Sahel linalo Heshimika kwa Darubini ya Dunia inayo vuta zaidi ya kilometa 3009 ...wewe ni KRESHE..mioyo ya kimaskini isiyihitaji TAFITI kuitambuwa..nnya...
 
Huo ndo mpango mzima sasa ni muda wa kujitangaza na kuwa na base imara kila mkoa na kila kanda ili kupata watu wengi.

Kuwe na siasa safi na si za kumsema marehemu ili kujenga chama safi zaidi.

Mnaanza kujitambua pia. Mtafute wastaarabu wawe wanawasemea maana watu wa kaskazini hawana ushawishi wa kuongea. Tafuteni Waswahili kama Abdu Nondo wa ACT, sasa tafuteni vijana wadogo kama yule mwenye mambo ya mipasho ndo siasa inataka.
 
Back
Top Bottom