Hii Ni CNN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii Ni CNN

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elusive, Apr 11, 2009.

 1. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa wanaofuatilia vipindi vya CNN International kwa hizi siku za karibuni wataona kuwa kila baada ya nusu saa sauti ya mtangazaji inasema 'from here and every where this is CNN' kwa lugha tofauti pamoja na jina la nchi ambayo hiyo lugha inaongewa na maandishi yakimaanisha ni CNN pamoja na lugha zinazotajwa na kiswahili nacho pia kinatumika katika tangazo hilo ambalo huanza na jina la Tanzania na taswira ya milima na nyika na maneno ya HII NI CNN ikifuatiwa na sauti ya mwandishi Isha Sesei inaongea Hii ni CNN. Tangazo hili ni la sekunde au nusu sekunde lakini nionavyo mimi ni kuwa linadhihirisha kuwa Lugha ya kiswahili ni kubwa na inaongewa na watu wengi hata wakafiria kuingiza katika hayo matangazo yao inafaa tuwapongeze kwa hilo nasi pia tujipongeze kwa kuitukuza Lugha yetu.
   
 2. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kutokana na uwazi na ukweli wa habari zao katika kujulisha ulimwengu nini kinatendeka na kinatokea katika kila nchi na kila pembe ya ulimwengu
  [ame=http://www.youtube.com/watch?v=M9ZPGLNFtQI]YouTube - Racism in Miss Tanzania?[/ame]
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kumbe huyu ndiyo SAKINA DATOO? Lohh, huwa namsoma tu huyu (kumbe ni mama).
  Babylon asante maana na sisi wa Sikonge tumemuona hatimaye.
   
 4. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu,
  Hatuna cha kujipongeza. Tanzania ni Nchi na CNN ni kampuni binafsi. Kwa ukubwa na umaarufu, nchi ni kubwa kuliko kampuni binafsi, CNN. Kwa maana hiyo, CNN inategemea kunufaika kwa kuitangaza Tanzania na Kiswahili chake, si vinginevyo.
  Hapa naliona tatizo la kutojitambua na kujiamini, si kwako tu bali hata kwa viongozi wetu. Na hii self-belittling inatokana kuwa na viongozi wenye upeo mdogo. Viongozi wasiojiamini. Hiki ni mojawapo cha chanzo cha rushwa nchini.
  Amka!
  Jiamini ndugu!
  Nchi ni kubwa kuliko kampuni.

  Unajua hoteli kubwa ya nyota 5 inayojengwa katika mbuga ya Serengeti ni mali ya nani?
  Jibu: Mabeberu wa Amerika. Hii ndiyo siri ya CNN kutangaza Tanzania, mbuga zake na Kiswahili chake. Inawatangazia Waamerika ilipowekezwa mitaji (Amerika yao nyingine/ndogo) yao na starehe zao waje kutumia. Wakimaliza kutumia pesa inarudi Amerika. Huu ndio mkakati wao.
  Mkakati wetu ni upi?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  Matumizi yoyote ya Kiswahili nje ya mipaka yetu ni ukuaji wa Lugha ya Kiswahili hata kama wafaidika wakuu sio sisi Watanzania, bali lugha yetu inakuwa.
  Niliwahi kuona tangaza la hoteli ya Zanzibar Dongwe Club Vacanze katika jarida la Kitaliano. Nilipokwenda Zanzibar, nikafunga safari mpaka hoteli hiyo. Hata kuingia getini ilikuwa shughuli, kufika reception nikaelezwa booking na malipo yote hufanywa Italy, wakanipa website ya kufanyia booking, nikakuta ni ya lugha ya Kiitaliano tuu. Safari yangu ikaishia hapo, na kulazimika kutafuta hoteli nyingine.

  Hata hivyo nikatafiti kwa wafanyakazi wenyeji, nikaelezwa, hapo waswahili hawaji na ukiwaona ni wadada tuu kwa ajili ya kuwastarehesha wataliano. Mpaka menu yao ni Kitaliano tuu. Maana yake hoteli ile ni kwa manufaa yao na lugha yao.

  Angalau siku hizi, ukipanda Swiss Air toka Tanzania au SAA, unapata na makaribisho ya Kiswahili. Ndani ya Inflight Intertainment ya Emirates kuliwahi kuwa na wimbo wa Kiswahili wa Khadija Nin "Sambolero my Son" na sasa kuna wimbo pia wa Kiswahili umeibwa West Africa. Huku kote ni kukua Kiswahili.

  Kwa CNN huo ni mwanzo mzuri, baada ya CNN Arabic, itafuatia CNN Swahili. Safari ni hatua na tumeishaanza safari ya kufikia Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kimataifa.

  Kikwete alipoitumia AU, watu wameikubali, japo karibu wakalimani wote wanatoka Kenya. Wenzetu wajanja kuna mambo waliona mbali, wanafundisha lugha zote za bara la Afrika, siye ni tumekomalia Kiingereza tuu na French kidogo.

  kati ya nchi za Afrika ya Mashariki, Tanzania ndio iliongoza kwa matumizi ya Kiswahili. Watangazaji wa mwanzo wa idhaa za Kiswahili za BBC, Voice of Amerika, Radio Japan, Deustche-Welle, All India Radio, Radio Moscow na Trans Africa, wote walitoka Tanzania, RTD. Leo Wakenya ndio wameshika Usukani, Ukiondoa Tido kuongoza BBC na Muganda VOA, sasa kote ni Wakenya. Mpaka Makao Makuu ya BBC Swahili kwa Africa ni Nairobi. Wabongo tuko wapi?. Tumelala!.
   
 6. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Ndugu,
  Huo ndio ukweli ndugu. Ni mfano halisi wa hoja yangu hapo awali. Kwamba kutangazwa CNN au majarida ya Ulaya/Amerika bila ya maandalizi ya kunufaisha wananchi ni 'good for nothing.' Na katika hili, kila mtu anapaswa kufahamu kuwa ufumbuzi wa hili 'gunia' hautokani na harakati za mtu binafsi bali wajibu wa serikali. Aidha, si kuwa Kenya ni wajanja, hapana! wanamipango yao ya uhakika. Kwa taarifa ni kwamba kwa sasa Kenya inapeleka walimu wa Kiswahili Nigeria. Hiyo yoe ni mipango ya kisera inayoongozwa na serikali yao. Serikali ya Tz bado wanasherekea ushindi wa 2005. Ushindi wa kishindo! Wakati wanamalizia mabaki ya EPA itakuwa 2015. Bagambila balinsi. Karagabao.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mnapulizwa huku mnatafunwa ,huo ni upanya kula kucha za vidole vya miguu na kumega nyama.
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunacho cha kujifunia ndugu yangu CNN Ni kampuni kubwa inatizamwa na watu wengi sana duniani ndo kusema lugha yetu imekuwa,kama ulipitia kule utakumbuka sifa mojawapo ya lugha,pili kujengwa hoteli hilo ni swala la msingi maana ajira itakuwepo na kipato cha eneo husika kitapanda,jamani tuwe tuaangalia na uwekezaji wenyewe ndo tuukosoe,ingekuwa madini ambayo tunaachiwa mashimo sawa lkn hiyo na wajenge nyingi tu,
   
 9. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Good Analysis.
   
 10. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #10
  Apr 16, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  All in all tuna cha kujivunia, TANGAZO LA KIGANDA LIPO? kwa publicity nchi huwezi kuilinganisha na CNN hata hizo tunazijijua tumezijua kwa sababu ya CNN. Cha muhimu ni kutumia fursa hii kujitayarisha ili tufaidike na hii publicuty huku tukifuatilia kwa karibu MKATABA WA UJENZI WA HIYO HOTEL tujue tunafaidika vipi.
   
Loading...