Hii ni aibu kwa Waziri Shonza kushindwa kutofautisha kati ya Ngorongoro Heroes na Serengeti boys

Akijibu swali bungeni ameipongeza Serengeti boys kwa ushindi wakati timu ya vijana iliyoshinda mechi juzi ni ya vijana ya Ngorongoro Heroes kwa kuifunga DRC.

Kama Naibu waziri hajui hata timu shiriki ni ipi je uwezo wa kusimamia timu zetu kuleta ushindi itawezekana?

Kweli hawa mawaziri wetu hawapo makini kweli kweli. Na sio kasema kwa bahati mbaya ni kuwa kaitaja Serengeti boys zaidi ya mara tatu.
Ngoja tu ajulikane kama waziri lakini kiuhalisia hata ukatibu kata ungemshinda
 
Ndio tatizo la kukabidhiwa nadaraka hili uwakomeshe watu Fulani na sio kwa ajiri kutatua changamoto zilizopo kwenye kile ulichokabidhiwa kusimamia.

Huyu Dada nna uhakika hawezi kutaja hata majina matano ya wachezaji wa taifa stars!!

Upuuzi mtupu kuna nafasi zingine za kisiasa hazistahili kuendeshwa na wanasiasa totally

.....we unawaza km mimi, umenikumbusha sammata alivyotoka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa afrika...."

lukuvi akiwa waziri wa sekta husika alitoa maboko ukumbini mpaka ukumbi mzima ukawa unacheka " eti chandimu ye anasema ndimu"
 
Ila timu zote zimeshinda heroes kampiga Congo na Serengeti anafanya vizur Burundi
 
Nyinyi wenye kujua kila kitu mna msaada kwa nchi yenu!!. Hakuna ajuaye kila kitu hata waziri Mwakyembe imembidi ajifunze mambo mengi kuhusiana na michezo pamoja na sekta nzima ya habari.

Punguzeni mbwembe za kujiona mnafahamu kila kitu. Kila mtu maishani anayo siku ya kwanza ya kujifunza kitu kipya.

Ndio maana watoto wa chekechea karibu wote hulia sana siku ya kwanza wakipelekwa shule, lakini ni hao hao ambao huufurahia urafiki mpya kutoka kwa watoto wenzao kadri siku zinavyokwenda.

unapoteuliwa kuwa waziri wa michezo inapaswa uwe na back ground ya michezo na sio uanze kujifunza ukiwa tayari wizarani, hii si sawa!!

na hya ndyo mambo yanayofanya sekta yetu ya michezo isipige hatua kwa sababu tunawapa dhamana watu ambao hawana interest kbsa na mambo ya michezo, hawana passion na hawajui changamoto zinazokabili sekta nzima coz ni outsiders. ndyo maana unaskia vilio kila sehemu kuanzia wasanii hadi wanamichezo

Mwakyembe anapiga siasa tu! coz hajui exactly kipi anatakiwa afanye ..amebaki kukabidhi bendera na kupiga porojo kila siku na hya yote yanasababishwa na kuleta siasa kila sehemu
 
km hawajui kuhusu michezo wanafanya nini wizarani? hyo kazi angepewa leodgar tenga au filbert bayi usingeskia hyo maboko ya mawaziri wetu...mwisho wa siku mi nasema " kazi ya mapishi apewe mpishi"
Tatizo lenu mnakuza vitu vidogo vidogo hulka zile zile za kupenda udaku. Timu zote mbili za vijana zimeshinda.

Na ndio jambo la muhimu, waziri kukosea ni mambo ya kawaida sana. Wanakosea mapadre na mashekhe wakiwa misikitini na makanisani sembuse hawa mawaziri.!!
 
unapoteuliwa kuwa waziri wa michezo inapaswa uwe na back ground ya michezo na sio uanze kujifunza ukiwa tayari wizarani, hii si sawa!!

na hya ndyo mambo yanayofanya sekta yetu ya michezo isipige hatua kwa sababu tunawapa dhamana watu ambao hawana interest kbsa na mambo ya michezo, hawana passion na hawajui changamoto zinazokabili sekta nzima coz ni outsiders. ndyo maana unaskia vilio kila sehemu kuanzia wasanii hadi wanamichezo

Mwakyembe anapiga siasa tu! coz hajui exactly kipi anatakiwa afanye ..amebaki kukabidhi bendera na kupiga porojo kila siku na hya yote yanasababishwa na kuleta siasa kila sehemu
Anachokifanya Mwakyembe ni kikubwa pengine kuliko uwezo wako wa kuelewa masuala mbalimbali yanayohusiana na wizara yake.
Sio kweli kwamba amebakia kukabidhi bendera, sasa hivi wanamuziki wanafaidika kuliko enzi za awamu ya nne, kwa sababu ya utetezi mkubwa wa Mwakyembe, wacheza sinema pia wanatengenezewa mazingira ya kupata wanachostahili kwa wakati.

Huko kwenye soka na michezo mingine kuna matatizo ambayo ni ya miaka na miaka, huwezi kuyamaliza kwa siku moja.

Jiulize kwanini makocha wetu wazalendo wanaishia humu humu tu, jiulize kwanini katika watu milioni 54 tunamtegemea Samatta na Msuva tu, jiulize mambo mengi na usidhani ni kazi rahisi kubadili mindsets zetu.

Jiulize kwanini mipango ya Mo Dewji inapingwa na watu ambao walipaswa kuwa wa kwanza katika kuiunga mkono.

Zama katika fikra pevu ndio utafahamu namna ya kutatua matatizo ya wizara ya Mwakyembe, kushambulia personalities hakuwezi kuja na suluhisho la aina yoyote ile.
 
we jamaa haupo update kbsa!!!

hivi unajua kwanini mchakato wa mo kupewa timu umesimama?
nikusaidie ....mchakato wa mo! kupewa timu umesimama kwa sababu serikali kwa kumtumia mwakyembe huyo huyo imeuingilia mchakato na kutaka mo apewe 49% na sio 51% alizotaka kwa hyo naweza sema mwakyembe ameuvuruga mchakato na mpk leo kuna majadiliano ya kubatilisha maamuzi ya serikali lkn serikali imetia ngumu wanaogopa mo kupata influence ya kisiasa kwa kuitumia simba km alivyofanya moise katumbi na tp mazembe
kwa hyo ukae ukijua sio wanachama wa simba wanaokwamisha huu mchakato ni mwakyembe ndyo aliyekwamisha huu mchakato baada ya kuingiza siasa na kujipendekeza kwa rais ili aonekane mchapa kazi

unadai mazingira ya wasanii kufanya kazi ni mazuri are u crazy??
wasanii karibia miaka 20 sasa wanalalamika khs uharamia wa kazi zao serikali wameshindwa kbsa kukomesha huu wizi wa kazi zao ,wamebaki kupiga porojo tu huku suluhisho la kudumu bdo kizungumkuti

labda ungeniambia amefanikiwa kuwadhibiti wasanii na kuminya uhuru wao kwa kuwakataza kuimba nyimbo za kuikosoa serikal hpo ningekuelewa! ...rejea ishu ya ney wa mitego na roma mkatoliki

sekta ya filamu ndio imekufa kbsa siku izi hatuwaoni hta akina ray na jb waki to a filamu

hya unawazungumzia kuwategemea msuva na samata hujui kuwa mifumo ya kuwapata wachezaji wazuri ni jukumu la serikali

umitashumta na umiseta ilifutwa kwa takribani miaka 10 now imerudishwa lkn inafanyika kwa staili ya bora liende kwa hyo tija hamna

viko wapi viwanja (sport centers) za kuendeleza vipaji
wako wapi walimu wa kuvitunza vipaji vyetu ?
vp khs vifaa?

na juzi kati tu tumeskia mabondia wa timu ya taifa walikuwa wanashindia uji kwenye mazoezi kabla ya kwenda kwenye jumuiya ya madola... mwakyembe sijui alikuwa wapi?

tht y nikasema mwakyembe anapiga porojo tu!
sijaona km ana mikakati yoyote ya kuhakikisha tunapiga hatua
 
Mkuu yapo mema mengi yanayoendelea, siku zote serikali zetu hufananishwa na tambara la kupigia deki.

Nimekwambia kuwa kubadili mentality ya watanzania kwenye masuala yanayotuhusu sio suala la siku moja au mbili.

Unaweza kuwalaumu mawaziri wengi tu lakini cha muhimu ni kuangalia aina ya jamii tuliyonayo.
 
Akili zenye kujielewa zilipaswa kutupeleka kwenye kuzipongeza Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes kwenye kuweza kuvuka vikwazo walivyokutana navyo.

Na sio kwenye kuangalia makosa ya naibu waziri Shonza. Wenzetu wanaishi na akili zilizo positive, sisi tunaishi na upuuzi wa kuangalia makosa madogo madogo yanayochangiwa na ubinadamu.

Aliyeturoga bado anaishi au ameshafariki dunia!!. Kwanini akili zetu hazina shukrani na siku zote zimejaa malalamiko na upuuzi wa ujuaji!!??.

Kuna kazi kubwa inafanyika mpaka vijana wetu wanaanza kutengeneza heshima kwenye soka la afrika, lakini upuuzi ndani ya vichwa vyetu unatupeleka kwenye malalamiko na dharau kwa viongozi!!.

Shame upon us.
 
Chakaza,
Mawaziri wengi na Manaibu wao katika awamu hii ni kichekesho, viroja na vihoja...!!
Kiukweli huyu Shonza hana sifa kabisa za kuwa N/Waziri. Tunajua ni kwanini alipewa Unaibu kama zawadi......baada ya kujenga hoja ya KUWAKOMOA Kina Halima Mdee na Esther Bulaya kwamba wafungiwe Vikao vya Bunge Mwaka mzima na hoja hiyo ikapita....!!!Ni uhuni mtupu.
Chakaza ndo ameboronga, Team zote zilicheza na zote zilishinda, Serengeti iliipiga Sudan goli 6 bila, na ngorongoro, iliipiga drc kwa mikwaju ya penalty 6, kwa 5.

kwa matokeo hayo Serengeti watacheza na Kenya, huku ngorongoro watakipiga na Mali.
 
Akili zenye kujielewa zilipaswa kutupeleka kwenye kuzipongeza Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes kwenye kuweza kuvuka vikwazo walivyokutana navyo.

Na sio kwenye kuangalia makosa ya naibu waziri Shonza. Wenzetu wanaishi na akili zilizo positive, sisi tunaishi na upuuzi wa kuangalia makosa madogo madogo yanayochangiwa na ubinadamu.

Aliyeturoga bado anaishi au ameshafariki dunia!!. Kwanini akili zetu hazina shukrani na siku zote zimejaa malalamiko na upuuzi wa ujuaji!!??.

Kuna kazi kubwa inafanyika mpaka vijana wetu wanaanza kutengeneza heshima kwenye soka la afrika, lakini upuuzi ndani ya vichwa vyetu unatupeleka kwenye malalamiko na dharau kwa viongozi!!.

Shame upon us.
OK, Shonza alichofanya ni kutambua timu zote mbili? Mbona unamlinda sana yeye bila kujua kuwa ndio muhusika mkuu wa wizara na anapaswa kuwa na general knowledge kuhusu wizara yake?
Huo utetezi wa eti makosa ya kibinadamu ni ujinga wa kiwango cha juu mno
 
Yote kwa yote 1.5T lazima zirudi.Pigeni porojo weeee mwisho wa siku tunataka kujua fedha zetu ziko wapi!
 
OK, Shonza alichofanya ni kutambua timu zote mbili? Mbona unamlinda sana yeye bila kujua kuwa ndio muhusika mkuu wa wizara na anapaswa kuwa na general knowledge kuhusu wizara yake?
Huo utetezi wa eti makosa ya kibinadamu ni ujinga wa kiwango cha juu mno
Watanzania tumejaa lawama na roho mbaya. Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes, zote zimeshinda, badala ya kuzipongeza timu zetu mbili wewe akili yako inakwenda kukosoa mheshimiwa naibu waziri!!, jambo ambalo ni jepesi kulinganisha na uhalisia wa mambo.

Mkuu hatuongozwi na malaika tunaongozwa na wanadamu wenye kila aina ya udhaifu. Ukitafuta udhaifu hauwezi ukaukosa. Tujikite kwenye yale ya muhimu zaidi. Namna gani timu zetu za vijana zinaweza kuwa na ushiriki wa kudumu kwenye michuano mikubwa barani Afrika.
 
Back
Top Bottom