Mkondakaiye
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 838
- 174
Serikali ya JK imekuwa ikijinadi kwa kujenga madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo hayana vifaa vya kufundishia, vitabu na walimu. Mwaka huu aibu imewakuta, wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba wamefeli sana kiasi cha kufanya ufaulu kitaifa kuwa chini ya 30%. Maafisa elimu wa mkoa wameagizwa kufanya uchaguzi wa wanafunzi hadi kufikia alama 70 kutoka alama ya mwisho kufaulu 100 kati ya 250. lengo ni kujaza madarasa ya sekondari yaliyojengwa ambayo hayana vitabu, walimu na vifaa vya kufundishia. Kazi hiyo inaanza jumatatu tarehe 17/12/2012 ili waziri wa elimu atangaze matokeo tarehe 21/12/2012
Najiuliza kama hapo mwanzo mwanafunzi aliyekuwa anapata alama ya mwisho kuchaguliwa alama 100 hakuwa na uwezo sekondari, leo mwanafunzi anaengia sekondari kwa alama 70 atamudu masomo hayo? yaani kwa wastani ana alama 14 kwa kila somo.
Serikali imeamua kutafuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuwapeleka sekondari. Hii ni aibu ya serikali ya JK.ambayo inaangalia uwingi (quantity) badala ya ubora (quality)
SERIKALI YA JK IMEVUNA ILICHOPANDA. IMEKALIA KUFANYA UFISADI NA KUSAHAU ELIMU.