Hii ni aibu kwa serikali ya JK

Hii ni aibu kwa serikali ya JK

Kilichosababisha kufeli pia inatakiwa tukumbuke wanafunzi hawa wamefanya mtihani tofauti na miaka ya nyuma kwani ndo walianzisha mfumo wa KUSHED kwa maswali ya multiple choice tu kitu ambacho ndo kinaendelea kudidimiza elimu yetu sijawahi kuona mwanafunzi anajibu mtihani wa Hesabu kwa multiple choice hawa akina Mulugo wanakotupeleka sio kwenyewe.

Kushed (kusiliba vyumba vya majibu) sio sababu ya wanafunzi kufeli kwani Dr ndalichako ni makini sana, alichukua sample ya baadhi ya wilaya walimu wakasahihisha. na baada ya zoezi hilo majibu yalikuwa sawa na mashine ilivyo sahihisha. so haya matokeo ni matunda ya ccm kutotilia maanani elimu.
 
Nape tunaomba uje utueze ni kwa nini serikali yenu imeshindwa kuinua kiwango cha elimu tz achana na porojo za kihuni eti dr slaa ana kadi ya magamba.

Kwa hili nape atasifia tu.
 
Wanawapitisha hivyo kimagumashi alafu huko mbele ndo watachaguliwa kuwa walimu,tutegemee wahitimu wa namna gani?pili watoto wanaoenda shule na bare feet,wanakaa chini,hawana vitabu huku walimu mshahara wanacheleweshwa hapo sishangai kwa matokeo ya aina hiyo
 
Serikali ya JK imekuwa ikijinadi kwa kujenga madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo hayana vifaa vya kufundishia, vitabu na walimu. Mwaka huu aibu imewakuta, wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba wamefeli sana kiasi cha kufanya ufaulu kitaifa kuwa chini ya 30%. Maafisa elimu wa mkoa wameagizwa kufanya uchaguzi wa wanafunzi hadi kufikia alama 70 kutoka alama ya mwisho kufaulu 100 kati ya 250. lengo ni kujaza madarasa ya sekondari yaliyojengwa ambayo hayana vitabu, walimu na vifaa vya kufundishia. Kazi hiyo inaanza jumatatu tarehe 17/12/2012 ili waziri wa elimu atangaze matokeo tarehe 21/12/2012

Najiuliza kama hapo mwanzo mwanafunzi aliyekuwa anapata alama ya mwisho kuchaguliwa alama 100 hakuwa na uwezo sekondari, leo mwanafunzi anaengia sekondari kwa alama 70 atamudu masomo hayo? yaani kwa wastani ana alama 14 kwa kila somo.

Serikali imeamua kutafuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuwapeleka sekondari. Hii ni aibu ya serikali ya JK.ambayo inaangalia uwingi (quantity) badala ya ubora (quality)

SERIKALI YA JK IMEVUNA ILICHOPANDA. IMEKALIA KUFANYA UFISADI NA KUSAHAU ELIMU.

Nooo! You can't be serious buddy! Hey kikwete are you there?
 
Hili si jambo la kuongelea uvunguni. Kama kuna ushahidi wa nyaraka uwekwe wazi na hatua zichukuliwe. Huu ni uuaji wa Taifa kuliko hata ule wa kuuwa binadamu. Wanaharakati, HakiElimu, n.k. livalieni njuga hili.

Huo ndio ujenzi wa Taifa la Tanzania wa Serikali ya ccm. Baada ya muda, wanaanza kusema ccm ina wazee wenye busara, CDM ina vijana vibaka wasio na mwelekeo. Huu ni uuaji wa nchi. Tatizo ni la raisi JK. Wito wangu hakuna haja ya kuwa na Raisi aina ya JK hata atoke chama gani kwa sababu aina hii imekaa ki-mambo binafsi zaidi. Habari za ustawi wa Serikali na Watanzania wote ni secondary.
 
hata tukisema hawasiki wamevaa miwani ya mbao hawaoni je inatosha kuwakabidhi jukumu la kuendesha seikali yetu:target: wananchi TUTAFAKARI WOTE KWA UMOJA WETU
 
Not that I am a "Die Hard" Kikwete fan. Nevertheless.

Kikwete anaweza kusema angalau yeye kajenga madarasa yasiyo walimu, wewe umejenga nini?

Bila kutoa orodha-idadi hapa na kuweka ankara husika kutoka si tu vitabu, bali pia vitabuluu (jua tofauti ya vitabu na vitabuluu) tunaweza kumlaumu Kikwete kwa kazi yake ya kuzidisha idadi ya Watanzania wenye access na elimu ya sekondari.

Nawewe ni GT? Sasa unamfananisha mchangiaji na kikwete kweli hii alkili au? Umempa mchangiaji U-Kikwete akakumbia ameshindwa?
 
Nawewe ni GT? Sasa unamfananisha mchangiaji na kikwete kweli hii alkili au? Umempa mchangiaji U-Kikwete akakumbia ameshindwa?

I have never claimed to be a GT in my life, whatever that is.

Kwamba nimemfananisha mchangiaji na Kikwete ni muonekano unaotokana na umasikini wa mawazo yako.

U-Kikwete ni nasaba, na hamna mtu yeyote anayeupata nje ya nasaba.
 
Kiukweli serikali ya ccm imetuchoka,hivi taifa linakwenda wapi?viongozi hawastuki kabisa.
 
Huo ni mwanzo tu kuelekea shimoni kwa watanzania ambao, nakumbuka maneno ya hayati Nyerere alisema msipoangalia waalii watakuwa wanakuja kutalii ili kuona watanzania vituko baadala ya kuja kuona wanyama wa Serengeti.

Hiv wamekazana kuanzisha mpango wa kutangaza mafanikio ya ccm kwenye redio na tv wakati elimu imedoda maendeleo gani hayo pasipo elimu? kwanza mafanikio hayatangazwi yataonekana na kila mtu atayasikia na kuyaonja, waende Rwanda kujifunza mafanikio ya kweli.
 
kiukweli inasikitisha sana utashanga watasema kiwango kimeongezeka kuficha aibu ila ipo siku mwisho wao utafika tu
 
Mnapoongelea aibu naona mnamsingizia tu JK kwa sababu kwa asili huwa haoni aibu kwa jambo lolote lile, sasa hii culture ya aibu haiwezi kuanza tu ghafla kama ngoma ya mdundiko.
 
inasikitisha na kuhuzunisha sana sijui tutapata taifa la namna gani???????????? Utasikia kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa kiwango cha juu hawashindwi hawa kuchakachua
 
Jicho langu linaona raia wamekata tamaa ktk elimu na nyanja nyengne kiasi ambach wanasubiri mbingu ishuke ili mungu awavishe taji.nawachukia wanasiasa wote wa Afrika
 
Hivi ngoma ya mdundiko bado ipo? Siku hizi nasikia taarabu tu kila kona, au wapiga ngoma kubwa wamepungua?
 
Back
Top Bottom