Hii ni aibu kwa serikali ya JK

Hii ni aibu kwa serikali ya JK

Watanzania wote tunayo sababu ya kuhoji maendeleo ya Elimu nchini mwetu tusiwaachie wanasiasa.
 
Hili si jambo la
kuongelea uvunguni. Kama kuna ushahidi wa nyaraka uwekwe wazi na hatua
zichukuliwe. Huu ni uuaji wa Taifa kuliko hata ule wa kuuwa binadamu.
Wanaharakati, HakiElimu, n.k. livalieni njuga hili.

Niseme ukweli jambo hili ni kweli kwani nimesikia Afisa elimu fulani alidokeza kwamba kama sio ujanja uliofanywa, ingekuwa hailzeki kuhuhusiana na kiwango cha kufeli
 
Sasa huo ujanja utasaidia nini kama wamefeli si wataenda seondari hata wasiojua kusoma na kuandika?
 
JK atasema ni upepo tuu utapita!
alafu mjue watoto wao hawamo umo so lazima wataligunika kiaina
 
kwenye kampeni htutaji ufauru tuna taja idadi ya walio ingia secondary watanzania wanapiga makofi na kura wanapewa.chukua hatua sasa nisisi twaweza
 
Serikali isipo jali waliomu kwac kuwalipa vizuri na marupuru,matokeo yataendelea kuwa mabaya.Walimu walimu wameisha jipanga kufundisha chini ya kiwango.Serikali chukua hatua haraka kama hamuamini subiri matokeo tya kidato cha pili na cha nne ndo mtajua umuhimu wa kumjari mwalimu.
 
Serikali ya JK imekuwa ikijinadi kwa kujenga madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo hayana vifaa vya kufundishia, vitabu na walimu. Mwaka huu aibu imewakuta, wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba wamefeli sana kiasi cha kufanya ufaulu kitaifa kuwa chini ya 30%. Maafisa elimu wa mkoa wameagizwa kufanya uchaguzi wa wanafunzi hadi kufikia alama 70 kutoka alama ya mwisho kufaulu 100 kati ya 250. lengo ni kujaza madarasa ya sekondari yaliyojengwa ambayo hayana vitabu, walimu na vifaa vya kufundishia. Kazi hiyo inaanza jumatatu tarehe 17/12/2012 ili waziri wa elimu atangaze matokeo tarehe 21/12/2012

Najiuliza kama hapo mwanzo mwanafunzi aliyekuwa anapata alama ya mwisho kuchaguliwa alama 100 hakuwa na uwezo sekondari, leo mwanafunzi anaengia sekondari kwa alama 70 atamudu masomo hayo? yaani kwa wastani ana alama 14 kwa kila somo.

Serikali imeamua kutafuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuwapeleka sekondari. Hii ni aibu ya serikali ya JK.ambayo inaangalia uwingi (quantity) badala ya ubora (quality)

SERIKALI YA JK IMEVUNA ILICHOPANDA. IMEKALIA KUFANYA UFISADI NA KUSAHAU ELIMU.

Kila jambo linafanyiwa siasa;JK aliwahi kusema hata mwananfunzi wa kidato cha pili akifeli acha aendelee eti mtihani wa form Iv ndiyo utampima,matokeo yakawa halimbaya.
JK,kuna wakati alisema wanafunzi akifeli mtihani wa darasa la nne,muache aendelee na masomo matokeo yake tuliyaona.

Tunakwepa ukweli,wanataka kuwafurahisha wananchi na wazazi kwa ujumla,lakini aibu nyingine itakuja;kidato cha nne wakifeli,watakuja na mpango wa kuunda tume kuchunguza kwa nini wanafunzi wamefeli.
 
Serikali ya JK imekuwa ikijinadi kwa kujenga madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo hayana vifaa vya kufundishia, vitabu na walimu. Mwaka huu aibu imewakuta, wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba wamefeli sana kiasi cha kufanya ufaulu kitaifa kuwa chini ya 30%. Maafisa elimu wa mkoa wameagizwa kufanya uchaguzi wa wanafunzi hadi kufikia alama 70 kutoka alama ya mwisho kufaulu 100 kati ya 250. lengo ni kujaza madarasa ya sekondari yaliyojengwa ambayo hayana vitabu, walimu na vifaa vya kufundishia. Kazi hiyo inaanza jumatatu tarehe 17/12/2012 ili waziri wa elimu atangaze matokeo tarehe 21/12/2012

Najiuliza kama hapo mwanzo mwanafunzi aliyekuwa anapata alama ya mwisho kuchaguliwa alama 100 hakuwa na uwezo sekondari, leo mwanafunzi anaengia sekondari kwa alama 70 atamudu masomo hayo? yaani kwa wastani ana alama 14 kwa kila somo.

Serikali imeamua kutafuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuwapeleka sekondari. Hii ni aibu ya serikali ya JK.ambayo inaangalia uwingi (quantity) badala ya ubora (quality)

SERIKALI YA JK IMEVUNA ILICHOPANDA. IMEKALIA KUFANYA UFISADI NA KUSAHAU ELIMU.

Mkuu nilikuwa huko hata wenye alama 70 ni wa kutafuta, yaani hali ni mbaya.
 
Nape tunaomba uje utueze ni kwa nini serikali yenu imeshindwa kuinua kiwango cha elimu tz achana na porojo za kihuni eti dr slaa ana kadi ya magamba.
 
Wanafunzi elfu kumi walio faulu mwaka Jana hawajui kusoma wala kuandika,je walio baki wana hali gani? Jk NA ccm ni janga jamani.
 
Not that I am a "Die Hard" Kikwete fan. Nevertheless.

Kikwete anaweza kusema angalau yeye kajenga madarasa yasiyo walimu, wewe umejenga nini?

Bila kutoa orodha-idadi hapa na kuweka ankara husika kutoka si tu vitabu, bali pia vitabuluu (jua tofauti ya vitabu na vitabuluu) tunaweza kumlaumu Kikwete kwa kazi yake ya kuzidisha idadi ya Watanzania wenye access na elimu ya sekondari.
 
Ndo mafanikio ambayo Lukuvi ameagiza wawe wanatangaza kwenye tv na redio!'?? Bado watakuja wapuuzi wanaofikiria kwa kutumia matumbo na kusifia serikali dhaifu hii. Nimeamini kweli ccm ni laana kwa taifa hili na tunakoelekea watatuuza wazimawazima tusipochukua hatua
 
Mie ni mwalimu wa sekondari km kulikuwa na kidato cha 2 hawajui kusoma na kuandika mwaka huu je hao ambao ndio wamefeli zaidi ila lazima waende kujaza madarasa. Hakuna mwalimu atakae poteza muda wake afundishe haya maozo. Ni janga la taifa tuamke jamani jk na watu wake wanaua elimu yetu ili tuwe taifa la wajinga wengi. Hasira sana.
 
Kama kuna kitu kinanikera kwa utendaji wa ccm ni suala la elimu. Hivi inawezekanaje elimu ambayo ndiyo inatakiwa kuwa nguzo ya kwanza ya taifa inakuwa hovyo kiasi hiki? Hatsa Kenya wenzetu hapo elimu ni bure hadi sekondari lakini ni shule za serikali ndizo zinazofanya vizuri. Mwakahuu niliangalia shule ya Maranda ambayo ni ya serikali katika wilaya ya Siaya ilifaulisha wanafunzi zaidi ya mia100 kwa daraja la kwanza. ndiyo shule iliyoongoza sekondari. unaweza kutafuta maranda kwenye google ulinganishe na shule za kwanza za Tanzania. Sisi tulioko mpakani na Kenya inatubidi tuwapeleke watoto wetu kwa ndugu zetu walio upande wa Kenya ili wapate elimu bora kwenye shule za serikali ambazo wanafundisha vizuri.
Hapa kwetu ni longolongo tu. Hivi inawezekanaje shule za serikali ambayo serikali ina uwezo na mfumo usimamizi eti ndizo ziwe shule hovyo kuliko watu binafsi? Wengine watakuambia shule ni nyingi kuliko uwezo wa serikali lakini kwanini ujenge shule nyingi kuliko uwezo wako kuzihudumia. Hii ni sawa na mtu anayezaa watoto wengi halafu wanakuwa ombaomba na machokoraa mitaani.
Jamani ccm ni janga la taifa. hawawezi kurekebisha chochote hapa kwa vichwa vilevile na udhaifu uleule. They will never change.
 
Kuna jamaa yangu, amenionyesha TSM 9 mwanafunzi kidato cha kwanza 2013 kwa jumla ya Alama 69. Amechanguliwa. Hili ni janga la kitaifa.

acha uongo amekuonyesha wapi? wakati saa hizi wanaendelea na uchaguzi kuanzia jana
 
Matumizi makubwa ya serikali kenyeutawala. maendeleo ni siasa ili wapate kura ila sio wananchi wafaidike
 
Hali hiyo ya kuchakachua matokeo ili kufurahisha Watawala ndio inayosababisha kuwa na Wanafunzi walio Sekondari ambao hawajui kusoma na kuandika. Magamba yamelewa Utawala Shime shime tuyapumzishe
 
Serikali ya JK imekuwa ikijinadi kwa kujenga madarasa mengi ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo hayana vifaa vya kufundishia, vitabu na walimu. Mwaka huu aibu imewakuta, wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba wamefeli sana kiasi cha kufanya ufaulu kitaifa kuwa chini ya 30%. Maafisa elimu wa mkoa wameagizwa kufanya uchaguzi wa wanafunzi hadi kufikia alama 70 kutoka alama ya mwisho kufaulu 100 kati ya 250. lengo ni kujaza madarasa ya sekondari yaliyojengwa ambayo hayana vitabu, walimu na vifaa vya kufundishia. Kazi hiyo inaanza jumatatu tarehe 17/12/2012 ili waziri wa elimu atangaze matokeo tarehe 21/12/2012

Najiuliza kama hapo mwanzo mwanafunzi aliyekuwa anapata alama ya mwisho kuchaguliwa alama 100 hakuwa na uwezo sekondari, leo mwanafunzi anaengia sekondari kwa alama 70 atamudu masomo hayo? yaani kwa wastani ana alama 14 kwa kila somo.

Serikali imeamua kutafuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuwapeleka sekondari. Hii ni aibu ya serikali ya JK.ambayo inaangalia uwingi (quantity) badala ya ubora (quality)

SERIKALI YA JK IMEVUNA ILICHOPANDA. IMEKALIA KUFANYA UFISADI NA KUSAHAU ELIMU.

Mchakato wa kuiua elimu upo kazini kwa muda sasa! Madarasa yasiyokuwa na vifaa; waaimu wasiokuwepo hasa shule ziizopo katika mazingira magumu; walimu semi-baked (if baked at all)...Matatizo ni mengi; mitihani ya form 2 iwepo, mara isiwepo!

Hakuna mpango unaouona wenye kutia matumaini kuwa miaka kumi ijayo wanetu watakuwa wamepewa elimu ya kuwawezesha kusimama na kupambana kupata maisha yao katika maisha ya ushindani ya Karne ya 21!

Tunaozesha vichwa vya watoto wetu tukiona!
 
Back
Top Bottom