Ndugu Zangu Watanzania;
Si jambo geni hili, labda huenda mwaka huu limeongezeka ndio maana wameamua kuliweka wazi, au kutokana na matusi yamewashitua.
hoto:
hoto: Ninayoipata hapa ni kwamba tatizo hili
limetokana na Kuvuja kwa Mitihani,
Hao Baraza wakichunguza vizuri watakuta kuwa hiyo mitihani yenye majibu ya utumbo ni lazima ilikuwa imevuja. Sasa MWanafunzi alipata paper na akalitafutia majibu kabla ya kufika chumba cha mtihani. Akiwa anajiaminisha MIA KWA MIA kufanya vizuri, anafika ndani ya chumba kufunua karatasi
anakuta SIYO PAPER ALIYOIONA KABLA!!!!!!! :lol::lol::lol:
Ndipo hapo mtu anakosa jibu na anachanganyikiwa na kufikia kufanya mambo kama hayo.
Katika hili pande zote ni za kulaumiwa (1) Wanafunzi (2) wazazi (3) Walimu (4) Baraza la Mitihani
Wazazi tunachangia kiasi kikubwa kwani tunashiriki katika kuwapa pesa ili wanunue mitihani. Ili tu mtoto afaulu na kujiona ni sifa mtaani. kumbe tunamjengea msingi mbovu na matokeo yake ni haya.
Wanafunzi wanachangia kwa uvivu wa kutojibidisha kimasomo kwa kutegemea kununua mitihani.
Waalimu wanashiriki kiasi kikubwa, kwani kuna baadhi ya shule Walimu wanawatafutia mitihani ili watotot wafaulu wengi na shule ipate sifa kwa kupata alama za juu kitaifa, kumbe tunawaharibu watoto badala ya kuwajenga.
Baraza la Mitihani kuna wafanyakazi ambao siyo waaminifu, kwani wao kwa tamaa ya pesa wanatoa mitihani na kuiuuza.
Hivyo hili tatizo tusimlaumu mtoto peke yake kwani kuna Chain ndefu iliyoshiriki katika hili. Mtoto amefika na kukuta mtihani siyo aliotegemea, Je, tunafikiri atajibu kitu gani na ikiwa alitegemea shwali la kwanza ni
Multiple Choice kumbe kufika pale anakuta
hakuna Multiple Choice kuna
ESSAY tupu mwanzo mwisho.
Kwa nini asiandike matusi yaani kumtukana aliyebadilisha mtihani!!!!!!!
Sote tujirekebishe katika nafasi zetu tulivyoshiriki kumfanya mtoto aandike utumbo huu.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!