Huyu ndio yule mwanafunzi alieandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wa form four 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndio yule mwanafunzi alieandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wa form four 2011

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by IrDA, Aug 19, 2012.

 1. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Julius-Dawson-715x600.jpg
  Unakumbuka February 8 2012 wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne? stori kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari ya bongo fleva kwenye sehemu ya kujibia maswali.

  "nashukuru sana wanaosahihisha mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea na fani yangu ya bongofleva, Majita wangu wako levo za juu na sio East Zuu, kukosa ni kawaida kwa binadamu" hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7

  kwenye swali la 11 kwenye moja ya mitihani yake aliandika mistari ya bongofleva kwamba "acha utani my girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya"

  Baada ya hayo matokeo watu wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi, Jina lake la kuzaliwa ni Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa sababu 5 za kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye mitihani yake ya kumaliza kidato cha nne.
  Amesema "1 ni kutaka kutuma ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla, sababu ya pili ni kutaka kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi maisha magumu kwa sababu tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu iliyopo ambayo ukishindwa kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna mtu anaweza akawa anashindwa kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu kingine sasa mfumo uliopo hautoi nafasi kwa wasioweza hiyo system, sababu ya tatu ni kutokana na utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa sababu sijui kama kuna mwanafunzi yeyote aliewahi kufanya mtihani wake wa mwisho alafu mtihani wake ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na wapi alipopata"
  "Sababu ya nne ni kuhusu wazazi kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo kipi wanaweza kipi hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni kwa serikali ijaribu kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo kabisa, leo hii kuna mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka mitatu na kupewa degree ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata kimoja kwamba alikua na elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia una degree wakati hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea"
  "Kwa namna moja au nyingine sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu nilichofanya watu walikichukulia tofauti sikufanikiwa ndio maana nimeamua kujitokeza kumalizia kazi ambayo niliianza kuifanya kule kwa sababu nafsi yangu ilikua inanisuta, ila kwa sasa watu watakua wameelewa na ninaweza kuwasaidia watu wengine" – Julius (Elinaja)
  Orginal source http://millardayo.com/huyu-ndio-yule-mwanafunzi-alieandika-mistari-ya-bongofleva-kwenye-mtihani-wa-form-four/
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmmh, kazi kweli kweli
   
 3. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Amefaidikaje?
   
 5. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa kadiri ya uwezo wake amejitahidi kueleza jamii sababu muhimu ila jamii yetu bado inaamini katika kile ambacho wazazi wake wanataka kwa mtoto na sicho anachoamini mtoto kuwa anaweza
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kuwa na subira ewe mwalimu mtarajiwa.
   
 7. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  mkuzu wake !
   
 8. H

  Hasson Da Melles Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  matatizo ya Kula Ugoro ndani ya Chumba Cha mtihani..
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hapa dogo ana point lakini...
   
 10. e

  enoc Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatzo huyu dogo hajui kua kila m2 anayefaulu n msanii tena kwa tz elm ye2 ya kumeza meza hiii so alchokfanya kaarbu nafac yake muhm maisha atakuja juta.
   
 11. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yaaaah maaaaaaan!!!
   
 12. pitbull

  pitbull JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  @ meles na ilo jani hapo juu linahusika kina hance hao!
   
 13. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Itachukua karne moja nzima kuelewa maana.
  Elimu ni nini?

  Bill Gate aliishia second year University.
  Mike Dell second year University.
  Steve Jobs wa Apple RIP high school.
  Larry King wa CNN high school.

  huyu anaitwa mvuta bangi.
  Huenda ni yeye anavuta kweli au sisi ndiyo wavutaji sugu.
   
 14. Geezzle

  Geezzle JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Acha jnga man!second yr na high school za hao jamaa unacompare na darasa la saba la huyo Mwanamashair,uchwara?!nmeskia nymbo zake,c mwandsh mzur na hajui 'ku-rhyme'
   
 15. A

  Awadh Mabaraza Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka yupi kat ya hao aliandika mashair kwnye mtihan? Hao tayar walishapat pa kuanzia kujeng maisha yao cyo huyo acyejua ajibu nin kwnye mtihan. Mi naona nikutojua 2 na usela mavi ndo umemtawala. Kwani ukiwa msanii una degree yako utashndw kunata na beat. Kwanz bila shule utaandka nin zaid ya ngono, pombe na supla.
  Achukue mfan wa wasanii waliotangulia ambao wana styl kali kama blu ila hawana cha kuandka. Mi naona hana jipya ni utot 2 na ujinga..
   
 16. majorbanks

  majorbanks JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Usingizi Vs Kifo
   
 17. e

  enoc Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hv ww ubongo wako n klo ngap? U r bonge la GT
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwa ninavyojua mimi, hao walikuwa na uwezo mkubwa sana huko shule, Bill Gates kwa mfano, aliandika project nzuri sana ambayo ilimfanya aache shule na kwenda kuifanya hiyo project, na imemlipa. sasa huyu hajui hata kujibu hata swali moja la f4, unategemea akiacha shule atakuwa nani? si kuvuta bangi tu?
   
 19. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  waige mifano ya wenzao akina Kofi Olomide
   
 20. m

  markj JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  point alikuwa nazo! tatizo njia aliyoitumia kufikisha point zake ni mbovu! sasa mtu anayesahihisha mtihani yeye anamuda wa kusoma majibu na kusahihisha tu, hana muda wakusoma ujumbe, na kama alitaka kufikisha uo ujumbe kwanini asinge tumia njia kibao tu sasa na watu wangepata ujumbe, adi magazeti ya udaku ya mejaaa skuizi hayana kazi! mtoto mbwiga tu huyo ye muache awafwatishe hao clouds fm ambao hawana elimu wenzake alafu aone kama ajaishia kama wakina mr blue na kuzaa na kuita watoto majina ya waimba nyimbo wenzao huku future ikiwa ina shake! hata usipokuwa na utajiri wa ajabu, ila elimu inanafasi kubwa katika mabadiliko ya kimaisha hasa kwa sasa. tatizo mishule ya kata skuizi inabeba hadi vitoto viuni mno ndo mana! je na hao waloichora wacheza mpira na michezo, walikuwa wanafikisha ujumbe wa watu wa olompic au? watoto mambwiga hawa.
   
Loading...