Baada ya kifo cha Kanumba, Bongo Movie imepoteza mvuto. Ruge kakutoka, tugemee Bongo Fleva na Clouds Media kupotea

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,460
9,394
Tunaweza kuona kama jambo la kawaida ila ukifikilia sana jinsi Ruge alivyopigania tasnia ya mziki huu, na alivyotoa ushindani gemu ilichangamka sana

Swali fikilishi ndio hilo; Ruge kaenda na bongo fleva yake kama alivyoenda Kanumba maana baada ya kifo cha Kanumba ushindani ulipungua

Kupungua kwa ushindani ndio ikawa chanzo cha kushuka kwa bongo movie

R.I.P RUGE
 
Ruge alikua na maadui wengi sana yaani kafariki still jamaa wanamkandia tu as if mchango wake kwenye sanaa haujulikani na sio sanaa tu hadi ujasiariamali, Jamaa ni Alien nadhani karudi kwako .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaweza kuona kama jambo la kawaida ila ukifikilia sana jinsi ruge alivyopigania tasnia ya mziki huu, na alivyotoa ushindani gemu ilichangamka sana, swali fikilishi ndio hilo je ruge kaenda na bongo fleva yake kama alivyoenda kanumba maana baada ya kifo cha kanumba ushindani ulipungua kupungua kwa ushindani ndio ikawa chanzo cha kushuka kwa bongo movie

R.I.P RUGE
Hizi mada nyingine za kurpu kurpu ili mradi tu uonekane na wewe umemzungumzia vizuri marehemu. Hatma ya kila mja huamuliwa na yeye mwenyewe na ndio maana linabaki jukumu la tuliosalia tukisubiri zamu zetu kujitafari kwa mifano ya waliotutangulia.

Bongo Movie ipo pale pale, madada wa kazi wanaenjoy kama zamani na masela watakula bits kama kawaida. Jifunze tu machache kati ya mengi, usitembee na tutoto tudogo wala usidhulumu majasho ya wengine.

R.I.P Ruge Mutahaba
 
.
Ukweli ni kwamba Hakuna Clouds bila Ruge ila anaweza kuwepo Ruge bila Clouds, hakukuwa na Radio yeyote yakuishinda Clouds na hata ingetokea siyo leo.

Chemistry ya Ruge na joe imeifikisha Clouds hapa ilipo lakini kwa kiasi kikubwa mtu anaefanya operational activities siyo sawa na yule ambae hagusi chochote ingawa ana umiliki wa asilimia kadhaa kwenye taasisi. Wahasibu tunajifunza kitu kinaitwa "Partnership" yaani unaingia ubia na mtu kufanya kitu na mwisho wa siku kinachopatikana mnagawana, lakini kati yenu kuna mmoja anaweza kuwa na technical skills ya kufanya hiyo biashara zaidi ya mwingine na kwa maana nyingine anakuwa muajiriwa wa hiyo partnership business yenu.

Hapa ndipo umuhimu wa Ruge unapoonekana, miaka zaidi ya 20 Clouds Radio imeendelea kuwa kinara na Super brand nchini hii ni kutokana na uwezo binafsi na ushiriki wake wa moja kwa moja wa marehemu kwani bila yeye isingefika hapa. Hakuna anaepinga Ruge alikuwa ni mtu wa tofauti sana linapokuja suala la Uongozi na ubunifu, muungano wake na Kusaga ni mfano wa mtu mwenye kifaa cha kugundua madini ardhini lakini hana dhana za kuweza kuchimba hayo madini, na hapa ndipo anapotokea mtu mwenye mashine ya kuchimba madini na hivyo kuingia ubia wenye maslahi maana mmoja ana kifaa kinachong'amua madini na mwingine ana vifaa vya kuchimba hayo madini mwisho wa siku wanapata walichokitaka na malengo yanatimia

Pamoja na uwepo wa hao wengine lakini kuna vitu wanakosa hawa wasaidizi wa Ruge ambavyo Ruge alikuwa navyo. Biashara yoyote inakuwa na Threats za ndani na Nje,Threats za ndani zinaweza dhibitiwa kwa urahisi kuliko za nje.Mfano mzuri ni Polical Threat( sijajua kiswahili fasaha ila ni kama mashambulizi ya kisiasa) hapa ndiyo utajua umuhimu wa Ruge.

Juzi tuu kukosekana kwa Ruge kumefanya Fiesta isifanyike masaa machache kabla ya Tamasha lenyewe ambalo maandalizi yake yalikamilika kwa 98% kilichobaki ni wasanii kupanda na tamasha kuanza lakini ilishidikana. Hii ni kwasababu hakuna wakuweza kukabiliana na changamoto za kisiasa ambazo Ruge aliweza kuzi handle. Mwaka juzi kulikuwa na tishio la kuizima Fiesta isizidi saa6 usiku lakini Ruge aliweza limudu vema na akatatua hilo

Tuweke uswahili pembeni tuje kwenye fair ground. ILi kampuni iweze kupiga hatua inahitaji mtu mwenye uwezo binafsi lakini mwenye maamuzi magumu na muda mwingine yenye kuumiza wengi ili kampuni isimame, ubishe usibishe huo ndiyo ukweli

Kikubwa ni kwamba pale clouds hapakuwa na "succession plan'' ya nani mwenye uwezo wa kukalia kiti baada ya Ruge na hapo ndipo tatizo linapoanza. Hata Joe hana uwezo kama Ruge, atakuwa ni boss as boss kwa ndani lakini hataweza kukabiliana na Extenal business Threats kama Ruge. Wakati Fiesta inazimwa Joe alikuwepo lakini hakuweza limudu hilo hapa ndo utajua utofauti wa Ruge na Joe

Baada ya Fiesta Kushindikana mara ya kwanza Utagundua kuna utofauti mkubwa wa Clouds ya zamani na ya sasa yaani Clouds ya sasa imepoa na inazidi kupoa siku hadi siku. Pengo la Ruge halizibiki na Hakuna atakaeweza liziba.

Clouds Radio itapoa sana lakini media nyingine haziwezi simama kama ilivyokuwa Clouds Radio otherwise zitakuwa sawa kwa maana ya clouds kuwa chini sawa na wao.

Uwezo wa Ruge ni mkubwa, amefanya mengi mazuri na kama binadamu mabaya pia haya kosekani. Huu ni msiba wa kitaifa kila mmoja kwaguswa kwa upande wake


Mbele yake, nyuma yetu. Apumzike kwa Amani mr. Rugemalila Mutahaba.

"Mwili ukikataa,Pesa haina nafasi"
IMG_20190227_082901_562.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutegemee kupata mabilionare wasanii wengi sana maana kila msanii anaeulizwa mbona haufanyi vizuri anasema Marehem Ruge anamnyonya

Dudu baya anaposti clips Za kusherehekea Kifo Cha Ruge Kwenye mitandao

Tutegemee Muda mchache Ujao Dudubaya atakuwa Billionaire kwa Kuwa anaemdhulumu kishaondoka


'... Namna ya kunisaidia kuondoka Na Dhulma Za Ruge Na Clouds sio kuniambia wananiibia bali Ni kunitaftia Mtu Au Kampuni ambayo haitoniibia ili niachane Na kina Ruge kwa Kuwa kuniambia ananiibia bila ya kunipa plan B haitonisaidia'-Mwana FA
 
Kwangu mimi bongo movie haijawahi kuwa na mvuto tokea hiyo tasnia ianze kuwapo,huyo anayesifiwa kuwa ndio gwiji(RIP) was mediocre at best,lakini hayo ni maoni yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom