Msanii wa Bongo fleva na Diwani wa kata ya Mwanga, Clayton Chipando (Baba Levo) amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela

Sage Hamisi

Member
Dec 25, 2013
6
17
Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baba Levo amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani, hukumu maalum kutoka mahakama ya Mwanzo Mwandiga.


Zaidi, soma...

Kigoma. Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumshambulia askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Akitoa hukumu hiyo leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga, Hakimu Mkazi, Florence Ikolongo amesema Baba Levo alimshambulia askari F.8350 PC Msafiri Mponela.

Hakimu Ikolongo amesema kifungo hicho ni bila faini.

Karani wa mahakama hiyo, Jackson Mrefu amesema Baba Levo ametiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002.

Kufuatia hukumu hiyo ya kesi namba 52/2019 iliyomtia hatiani Baba Levo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, katibu wa ACT mkoani Kigoma, Juma Ramadhani amesema chama hicho kinafuatilia na kitatoa tamko.

"Kama chama tumepokea taarifa ya diwani wetu kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano na tumeambiwa kwamba alichukuliwa na gari kupelekwa gerezani, tutatoa taarifa rasmi ya chama leo mchana na jamii itajua msimamo wetu,” amesema Ramadhani.

Chanzo: Mwananchi

Maoni yangu
Kuna baadhi ya uonevu huwa unaendelea barabarani jambo ambalo vijana wengi wa Kigoma wanaotafuta riziki wanakuwa na hofu sana kunako askari hao, Unaweza kupigwa fine au kuombwa rushwa kwa kutokuwa na kizima moto kwenye bajaji (Ilihali mikoa mingine ni tofauti).

Baba Levo ni mtetezi wa Bodaboda, Bajaji na wanyonge wajasiriamali katika manispaa amewapambania vya kutosha leo amepatikana na hatia kwa nia ya kuwatetea wananchi wa mji mzima, Mwanga ndipo alipozaliwa baba levo. Kamati ya Madiwani imeshakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Zaidi, soma;

baba levo.jpg
 
Ila kiukwel trafik wa Kigoma wakorof mno
Kuna siku tumepigwa tochi kaz roho tunakamatiwa uvinza wakati wazir aliagizz ni papo kwa papo...
Kuuliza wanasema hawajapokea waraka labda mkaongee na kasmanda
Nikalipa kama kawa tu kasepa


Ila baba levo kilichomponzai ni U ACT wake
Angekuwa kijani ya singefika huku
 
Hicho kifungo hakina faini mbadala....

Sasa alianzaje kupiga askari badala ya kumshitaki.
 
Tatizo anajiona bongo flava plus udiwani hivyo anaweza jichukulia sheria mkononi. Acha akale maharage ya mawese na ugali wa dona.
 
Ila kiukwel trafik wa Kigoma wakorof mno
Kuna siku tumepigwa tochi kaz roho tunakamatiwa uvinza wakati wazir aliagizz ni papo kwa papo...
Kuuliza wanasema hawajapokea waraka labda mkaongee na kasmanda
Nikalipa kama kawa tu kasepa


Ila baba levo kilichomponzai ni U ACT wake
Angekuwa kijani ya singefika huku
Kwa hiyo kijani Hua wanapiga askari
 
Kutetea bodaboda kwa kupiga askari? Labda kama kabambikiwa kesi.

Mwanawachu mwenzie aka Khamenei anasemaje?
 
Viongozi vijana wengi wana mihemko kuna mambo mengine inabidi utumie busara halafu hii kesi kama waliidharau hivi
 
safi sana huwezi kumpiga askari akiwa katika majukumu yake, asije kuingia kumi na nane za wazee tu
 
Back
Top Bottom