Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unamuongelea hasa mzazi gani? maana usije ukawajumlisha na wale wa kwetu ambao uwezo wao umeishia kutupeleka shule ya kata, mwalimu mmoja masomo yooote, hakuna kitabu cha kiada wala ziada, hakuna maabara, hakuna madawati. Report card ikija nimfanyeje mtoto sasa?Wazazi wa siku hizi hawataki kulea watoto wao! Sio wababa wala wamama, kukimbizana na starehe za mjini jumatatu hadi jumatatu!
Kila mtu anavuna alichopanda, I'm sure report cards za mtoto kama huyu zilikuwa kila temu zimeandikwa na kupelekwa kwa mzazi.
Haswa ni kuwapotezea watoto muda, sijui serikali wanaangalia wapi kwa kweli...Mkuu, tukubali tukatae, shule za kata ni janga la Taifa. Nimecheki shule za kata kutoka kwenye wilaya yangu, waliofaulu kwa kiwango cha juu wameanzia division three. Wengi wamefeli! Cha ajabu, shule nyingine katika wilaya hiyo hiyo ( za dini na zile za serikali proper) zimefanya vizuri. Nawasikitikia sana hawa vijana wanaopangiwa shule za kata. Wanapotezewa muda!!
mi nashauri huyu aoane na mwanaasha jakaya kikwete.
Mi naona ingekuwa vizuri majina yao yangewekwa hadharani...
Ndugu Zangu Watanzania;
Si jambo geni hili, labda huenda mwaka huu limeongezeka ndio maana wameamua kuliweka wazi, au kutokana na matusi yamewashitua.
hoto:hoto: Ninayoipata hapa ni kwamba tatizo hili limetokana na Kuvuja kwa Mitihani,
Hao Baraza wakichunguza vizuri watakuta kuwa hiyo mitihani yenye majibu ya utumbo ni lazima ilikuwa imevuja. Sasa MWanafunzi alipata paper na akalitafutia majibu kabla ya kufika chumba cha mtihani. Akiwa anajiaminisha MIA KWA MIA kufanya vizuri, anafika ndani ya chumba kufunua karatasi anakuta SIYO PAPER ALIYOIONA KABLA!!!!!!! :lol::lol::lol:
Ndipo hapo mtu anakosa jibu na anachanganyikiwa na kufikia kufanya mambo kama hayo.
Katika hili pande zote ni za kulaumiwa (1) Wanafunzi (2) wazazi (3) Walimu (4) Baraza la Mitihani
Wazazi tunachangia kiasi kikubwa kwani tunashiriki katika kuwapa pesa ili wanunue mitihani. Ili tu mtoto afaulu na kujiona ni sifa mtaani. kumbe tunamjengea msingi mbovu na matokeo yake ni haya.
Wanafunzi wanachangia kwa uvivu wa kutojibidisha kimasomo kwa kutegemea kununua mitihani.
Waalimu wanashiriki kiasi kikubwa, kwani kuna baadhi ya shule Walimu wanawatafutia mitihani ili watotot wafaulu wengi na shule ipate sifa kwa kupata alama za juu kitaifa, kumbe tunawaharibu watoto badala ya kuwajenga.
Baraza la Mitihani kuna wafanyakazi ambao siyo waaminifu, kwani wao kwa tamaa ya pesa wanatoa mitihani na kuiuuza.
Hivyo hili tatizo tusimlaumu mtoto peke yake kwani kuna Chain ndefu iliyoshiriki katika hili. Mtoto amefika na kukuta mtihani siyo aliotegemea, Je, tunafikiri atajibu kitu gani na ikiwa alitegemea shwali la kwanza ni Multiple Choice kumbe kufika pale anakuta hakuna Multiple Choice kuna ESSAY tupu mwanzo mwisho.
Kwa nini asiandike matusi yaani kumtukana aliyebadilisha mtihani!!!!!!!
Sote tujirekebishe katika nafasi zetu tulivyoshiriki kumfanya mtoto aandike utumbo huu.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
mtoto kapoteza four years halafu bado hajitambui tu
Studio ? ....................aaaah ! Ile Ruge katudhulumu hivi hivi tunaona !