Hii ndo mistari ya bongo fleva iliyoandikwa na mwanafunzi wakati akifanya mitihani ya kidato cha 4

Wazazi wa siku hizi hawataki kulea watoto wao! Sio wababa wala wamama, kukimbizana na starehe za mjini jumatatu hadi jumatatu!
Kila mtu anavuna alichopanda, I'm sure report cards za mtoto kama huyu zilikuwa kila temu zimeandikwa na kupelekwa kwa mzazi.

bange bana.....bange mbaya sana!!
Hao majita ndo walikuwa wanamlipia ada? Nyambaf kabisa!!
 
aisee huyu dogo kala msuba
au alikuwa anasepa kila kipindi
hakai darasani.lol
amemkatisha sana mzazi wake tamaa jamanii
ngoja nisiseme sana maana wangu
yupo njiani ,naomba mungu tu isiwe hivi
 
Katibu mtendaji mkuu wa baraza hilo Dr Joyce Ndalichako amesema mmoja kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo alifikia hatua ya kuandika mashairi ya bongo fleva baada ya kukosa cha kujibu ambapo aliandika :“nashukuru sana wote wanaosahihisha huu mtihani wangu, nitakapofeli nitaendelea na fani yangu ya bongo fleva, majita yangu yako levo za juu na sio East zuu, ukiona vyaelea ujue vimeundwa”

Joyce amesema mtahiniwa aliandika mistari katika kila sehemu alipotakiwa kujibu swali, swali la sita na la saba aliandika hiyo mistari hapo juu, swali la kumi na moja ameandika......

CHANZO <<<HAPA>>>

Matunda ya shule kukosa walimu ndiyo haya. Yatasemwa mengi lakini daima tunasikia malalamiko shule hazina walimu, na hivyo watoto wanakuwa na muda mrefu wa kutunga mashairi.
 
not real sad mwanakijiji wanavuna walichopanda pale baraza akuna uozo mkubwa wa kugawa mitihani ,,,mchezo mchafu huyo mama akiwa mmoja wao na wanawapa watu kadhaa wakitoa maelekezo kiasi kadhaa
sasa mpaka ana fika fm4 ni mkubwa ameona upumbavu wakila siku wa barza hilo akaona kwa nini asiwape mistari tu wakafie nayo mbele ya safai unafikiri huyu mtoto kufanya hivyo mwisho wa maisha..nop...
HUYO MAMA ANATAKIWA ASEMA WAZI VYANZO VYA MITIHANI KUVUJA NA KWA NINI WATU WANAKUTWA WAMEANDIKA MAJIBU YANAFANANAA KAMA SI MICHEZO MICHAFU YA WALIMU


fafanu mkuu.. Kama una siri nzito.
 
Unamuongelea hasa mzazi gani? maana usije ukawajumlisha na wale wa kwetu ambao uwezo wao umeishia kutupeleka shule ya kata, mwalimu mmoja masomo yooote, hakuna kitabu cha kiada wala ziada, hakuna maabara, hakuna madawati. Report card ikija nimfanyeje mtoto sasa?

sekta yetu ya elimu jamani inasikitisha, aseme tu yule ambaye haya madhara hayajamgusa kwa njia moja au nyengine,

Navyoandika hapa namfikiria binti ambaye yuko so eager to learn na mzazi uwezo ndo umeishia shule ya kata, kesho sitashtuka akiandika madudu zaidi ya hayo kwenye majibu yake.


true....
 
Elimu sio kwa ajili ya kila mtu,huyu wito wake uko kwenye Mic.
Tatizo yuko kwenye nchi ambayo mfumo unalazimisha kila mtu kufuata mkondo mmoja,
ndio maana wengine hata vyuoni wanakariri ili mradi tu apate cheti akatafute kazi ili aishi.

Wangekuwa wanambadala karibu nusu ya wanafunzi walioko vyuoni bongo wasingekuwepo,ila wengi wao wapo kwa sababu hakuna alternative.

Unakuta mtu anachagua course kwa kuangalia wanalipwa kiasi gani!!!
 
hii ni hasara kwa mzazi na hizi shule za kata hizi ziangaliwe sana coz nakumbuka mwaka juzi alifaulu mtoto wa ndugu yangu mmoja nilishangaa san coz alikua hajui hata kuandika jina lake lkn alifaulu unategemea huko mbele anafanya nn si ndio wanaandika bongo fleva?
 
Wazazi wa siku hizi hawataki kulea watoto wao! Sio wababa wala wamama, kukimbizana na starehe za mjini jumatatu hadi jumatatu!
Kila mtu anavuna alichopanda, I'm sure report cards za mtoto kama huyu zilikuwa kila temu zimeandikwa na kupelekwa kwa mzazi.
CHA Kushangaza mtoto anakuwa anapaka 2,5, hata zero mzazi hafuatilii... Wazazi wanafkiria kusomesha ni kulipa Ada. Mzazi kwenye masuala ya maendeleo ya mwanaye haendi Shule lakini Sijui kasikia toto lake limechapwa bakora anakuwa na povu mdomoni walimu wameyasusa manunda YENU
 
Back
Top Bottom