Hii ndiyo miradi iliyofanyika Chato

Hii ndiyo miradi iliyofanyika Chato

Mkuu kama unazo details za Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Pwani za hivi naomba.
Kwa nini za maeneo hayo.
Jaribu za maeneo yafuatayo - Chagua wilaya yoyote mkoa wa Mtwara; mkoa wa Kigoma; mkoa wa Njombe, na hata chukua wilaya yoyote ndani ya mkoa wa Geita mbali ya Chato!

Hapo utakuwa umelinganisha vizuri.
 
Hiyo Billion 127 sisi huku Dar tumefanyia project moja tu ya Mfugale.. alafu Chato wanafanyia zaidi ya miradi 7...!!!
Mnakwenda shule kupiga ushuzi siku nzima, miaka yote, shule zote ulizopitia!

Halafu unajiona umesoma, sijui unayo digrii!

Pato la Dar es Salaam ni kiasi gani?

Kuna watu wangapi?
 
Huu unaitwa ulafi na ubinafsi. Nchi kubwa hii mtu unajijazia mamiradi ya mabilioni wakati sehemu zingine watu wanakosa maji nahuduma zingine muhimu.
Hapana.

Huu ni ulimbukeni (sijui ushamba nao unakaribiana na ulimbuke?)

Yule jamaa alikuwa na tabia za kilimbuke tokea zamani. Unakumbuka zile taa za barabarani kuendeshea punda!

Angekuwa ni mtu mwenye uelewa kidogo, pesa ile aliyojengea uwanja wa ndege wa kimataifa, angetumia nusu yake kuwahimiza na kuwawezesha wananchi wa eneo lile kuanzisha kilimo au shughuli zozote za kueleweka na kuzifanya kama sehemu za mafunzo; kwa mfano, mashamba shule.

Angepeleka wasomi wa maeneo hayo kusimamia kazi na kuwaelimisha wananchi ili kufanya kilimo cha kisasa kilicho endelevu.

Chato ingepata maendeleo mazuri na ingepata uwezo wa kujenga miradi mingine ya aina hiyo ndani ya miaka michache.

Na Chato kingekuwa kitovu cha kujifunzia. Wilaya na mikoa mbalimbali wangekuwa wanakwenda Chato kujifunza kilimo au uvuvi/ufugaji bora wa samaki au mifugo.

Hata malalamiko ya upendeleo yaliyofanyika yangepungua au hata kutowepo kabisa; maana mwanzilishi angejijengea sifa kubwa, hata kama ni sehemu ndogo; lakini kwa vile ingekuwa ni kichocheo cha maendeleo na sehemu zingine, hiyo ingekuwa ni sifa kwake.

Sasa angalia aibu hii!

Hiyo 'legacy' iliyokuwa inaimbwa itapatikana kwa njia za kipuuzi kama hizi?

Inabidi nitoe mfano hapa:
Chukulia kilimo cha alizeti, kuzalisha mafuta ya kula.

Sijui; lakini nadhani alizeti inastawi vizuri sehemu nyingi wilayani Chato.

Haya, wananchi wakapewa mafunzo sahihi ya kilimo cha alizeti.

Wataalam wakawepo wa kuwaelekeza hatua zote za kilimo bora cha zao hilo.

Vifaa, mbolea na mbegu safi vyote havikosekani kwa pesa yote ile; nusu ya bajeti ya uwanja wa ndege wa Chato.

Mashine na wataalam wa kukamua mafuta wapo na maandalizi yote yamepangwa ipasavyo.

Soko la mafuta ya kula Tanzania? Congo (DRC)? Burundi? Rwanda? na kwingine kote, bado haitoshi? Miundombinu ya usambazaji bidhaa hizo hiyo pesa haikosi kuikamilisha.

Chato ikawa ndio kitovu cha uzalishaji wa mafuta ya alizeti; mashudu----ufugaji samaki, ng'ombe, kuku n.k.

Sasa sijui niseme nini, kama jina la Magufuli lisingeweza kuandikwa kwa herufi za dhahabu, sio Chato tu, hata sehemu zingine!
 
Mingi ya hii miradi imekua ya matumizi sana kipindi cha msiba na maombolezo

Hayati John Pombe Joseph Magufuli alijaaliwa na mwenyezi Mungu kujiandalia hadi mazingira ya yeye kupumzishwa kwa amani

May his soul rest in eternal peace Amen🙏
Eeeenh Heeeee!

Ni vigumu kuandika chochote juu ya 'comment' kama yako hii!

Pole sana.

Still you keep a straight face!
 
Mkuu unazingua ndo nyie nyerere hakufanya maendeleo kwao huwa mna mponda pia hamna jema acha tanzania ijengwe pole pole sehemu moja moja mwisho tutamaliza kote shida ikwapi
Hiyo ndy polepole?? Miradi yote hiyo?? Rubbish
 
Hiyo Billion 127 sisi huku Dar tumefanyia project moja tu ya Mfugale.. alafu Chato wanafanyia zaidi ya miradi 7...!!!
Chato wilaya sio au Chato mkoa kwanini unalinganisha kijiji na Jiji au mkoa?
Upo sawa kweli????
 
Back
Top Bottom