Hii ndiyo idadi ya silaha za nyuklia Urusi, hali ilivyo mataifa mengine

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
Takwimu zote za silaha za nyuklia ni makadirio lakini, kwa mujibu wa Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, Urusi ina vichwa vya nyuklia 5,977 - vifaa vinavyosababisha mlipuko wa nyuklia - ingawa hii inajumuisha takriban 1,500 ambazo zimechoka na zinatazamiwa kuvunjwa.

Kati ya 4,500 zilizosalia au zaidi, nyingi zinachukuliwa kuwa silaha za kimkakati za nyuklia - makombora ya balestiki, au makombora, ambayo yanaweza kulengwa kwa umbali mrefu. Hizi ndizo silaha ambazo kawaida huhusishwa na vita vya nyuklia.


russian_nuclear_capability_v2_640x2-nc.jpg



Je, hii inalinganishwaje na nchi nyingine?

Nchi tisa zina silaha za nyuklia: China, Ufaransa, India, Israel, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Marekani na Uingereza.
China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza pia ni miongoni mwa mataifa 191 yaliyosaini Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Chini ya makubaliano hayo, wanapaswa kupunguza akiba yao ya silaha za nyuklia na, kwa nadharia, wamejitolea kutokomeza kabisa. Na imepunguza idadi ya vichwa vya kivita vilivyohifadhiwa katika nchi hizo tangu miaka ya 1970 na 80.

India, Israel na Pakistan hazikuwahi kujiunga na NPT - na Korea Kaskazini iliondoka mwaka 2003. Israel ni nchi pekee kati ya tisa ambayo haijawahi kukiri rasmi mpango wake wa nyuklia - lakini inakubaliwa na wengi kuwa na vichwa vya nyuklia.

Ukraine haina silaha za nyuklia na, licha ya shutuma za Rais Putin, hakuna ushahidi kuwa imejaribu kuzipata.

_123457186_nuclear_warheads_by_country_inf640x2-nc.jpg


Source: bbc
 
Back
Top Bottom