Putin akubaliana na Lukashenko kupeleka silaha za nyuklia za kimkakati nchini Belarus

HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
313
20230326_05_1235461_L.jpg

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema amekubaliana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko kupelekea silaha za nyuklia za kimkakati nchini Belarus.​

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Urusi yaliyotolewa jana Jumamosi, Putin alisema Lukashenko kwa muda mrefu aliibua suala la kuweka silaha za nyuklia za kimkakati nchini mwake.

Putin alisema kwamba Marekani imekuwa ikipeleka silaha za nyuklia za kimkakati kwenye maeneo ya washirika wake mataifa ya NATO.

Aligusia kuwa Urusi na Belarus zimekubaliana kufanya hivyo hivyo, akisisitiza upelekwaji huo hautakiuka matakwa yao ya kimataifa juu ya kutosambaza silaha za nyuklia.

Putin alisema kwamba mifumo ya kimkakati ya Iskander imehamishiwa Belarus na kwamba ndege za Air Force za Belarus huenda zikatumika kurushia silaha za nyuklia.

Aliongeza kuwa Urusi inapanga kukamilisha ujenzi wa kituo cha kuhifadhia silaha za kimkakati za nyuklia nchini Belarus ifikapo Julai Mosi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom