Hii ndiyo DNA ya Kitamaduni kabisa yenye ukweli 90%

Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.
Gentamycine, hakuna ushahidi wa hilo, ni kuhisia tu! Zamani wanaume walikuwa na tatizo la vibofu vya mkojo, nimekuwa na mpaka leo wanasema ilitokana na kuzini na wanawake wengi hivyo kupata maambukizi. Lakini ukweli ni kuwa TEZI DUME problems ndiyo ilikuwa source ya hayo... science has revealed this with no boubt. Fingerprints will never match two people!
 
Duh, mwanangu nimefanana nae utafikiri mama yake ana mashine ya PHOTOCOPY tatizo hizo alama za mkononi hazifanani hata kidogo, najiskia raha tu kufanana nae sura hata kama ikitokea sio wangu[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Muda wote nilikuwa nasubiri nisikie mashangazi na wengineo kumbe alama...
Ila zipo sema bado tu hujazijua maana tangu enzi za adam mpk leo lazima kutakuwa na loophole kwa hizi scenarios, endelea kuchimba utapata tu jaribu kuwasoma hawa Anthropologist watakuwa na majibu.. sema its too risk ikiwa wazi, wewe jua tu then kausha
 
Duh, mwanangu nimefanana nae utafikiri mama yake ana mashine ya PHOTOCOPY tatizo hizo alama za mkononi hazifanani hata kidogo, najiskia raha tu kufanana nae sura hata kama ikitokea sio wangu[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Huyo atakua wangu
Gentamycine, hakuna ushahidi wa hilo, ni kuhisia tu! Zamani wanaume walikuwa na tatizo la vibofu vya mkojo, nimekuwa na mpaka leo wanasema ilitokana na kuzini na wanawake wengi hivyo kupata maambukizi. Lakini ukweli ni kuwa TEZI DUME problems ndiyo ilikuwa source ya hayo... science has revealed this with no boubt. Fingerprints will never match two people!
 
Shukuru umeitwa baba hata kama si wa mkojo wako, kuna wenzio wanatafuta mpaka wa kupewa kwa masharti kwenye vituo vya yatima
 
Hamna ukweli kwenye izo alama nimilla tu za kizamani kwa sababu walikuwa hawana vipimo vya kisasa.
 
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.
Thank you sir.
 
mkuu mavyakula tunayokula haya siku hizi mitoto inazaliwa imefanana na ma kuku ya kisasa unaweza usiambulie hata alama toto lina mwaka linapelekwa english medium schools hata kilugha cha kwao haliwez kufunzwa
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ..... Mkuu umeua vibaya sana!
 
Ukila vyakula vya asili cop huikos mkuu naamini hilo kama sio miguu bas mikono lazima tu utaambulia mwingine miguu inafanana na ya mama mikono na sura kwa baba

Toka unga wa ugali hadi maji ya kunywa vyote supamarket kwa nn usitoe kiumbe tofaut

Mwingine kaoa miaka mi nne anahangaika kupata mtoto mmoja kunywa madawaaa wee limama nalo limetoa mimba balaa
 
Mkuu GENTAMYCINE Unaifahamu hii tovuti??
Je wamekulipa kwa kunakili habari yako bila ya kukutambua kama chanzo cha habari yao??
IMG_20170226_011257_450.JPG
 
Ukishasoma basi usifanyie kazi hiki ulichokisoma Mkuu vinginevyo unaweza kuishi kwa wasiwasi ukaishia kuharibu ndoa, lakini hiyo ya vidole ni kweli kabisa tena vya miguu na mikono labda wana wengine vinafanana na vya umamani.

Mmmh mbona huyu mtoto nilienaye hapa alama zake zigzag sio Zangu, Mtatuua kwa presha asubuhi hapa Kazi hazifanyiki
 
Ivi kuna watu walikuwa na watoto wa nje ya ndoa kama mababu zetu?yaani napingana na mroa mada 100pacent maana zamani walisema usiweke mayai yote kwenye kapu mkja maana yake usizae watoto wako wote na mtu mmoja maana kama ana ugijwa wa kurith utamaliza kizazi chako.na ukichunguza sana mababu walikuwa wanawaagizia watt wao usioe au usiolewe kwa fulani maana yake ni kuwa kuna damu yake
Habari mpya kwangu....
 
unataka mtoto afanane nawe wakati wewe ni impotent ?shukuru mkeo kakuhifadhia heshima kwa kukuletea hako katoto.vinginevyo leo usingekuwa unaitwa baba juma..!
 
Mkuu GENTAMYCINE Unaifahamu hii tovuti??
Je wamekulipa kwa kunakili habari yako bila ya kukutambua kama chanzo cha habari yao?? View attachment 474608

Hapana Mkuu wala siwafahamu na ndiyo ishakula Kwangu hivyo. Halafu kuna Milofa mingi mno yenye Media na Blogs zao huwa wanachukuwa sana Mavituz yangu tena vilr vile lakini niliyehangaika kuzifukunyua na kuzileta on public nakufa tu na Umasikini wangu kudadadeki. Akhsante Mkuu kwa kunifungua na nadhani hii kitu imenipa sasa changamoto ya kuitumia hii ID yangu ambayo sasa imeshakuwa brand ya kutukuka siyo tu Tanzania bali dunini kote na hata Mbinguni ili iniletee Mapinduzi Binafsi ya Kiuchumi. Usihofu Mkuu kwa hawa Watu kuchukua Madini yangu kwani kwa Kipaji, Uwezo na Karama ya Kimungu niliyonayo huwa siishiwi Taarifa na Matukio tena makubwa hata kushinda haya na najua Watu wengi kila siku ya iendayo kwa Mungu huingia humu JF kuikodolea hii ID Brand ya GENTAMYCINE imesema au imekuja na nini.

Nakushukuru sana Mkuu wangu lukesam na ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom