Hii ndiyo DNA ya Kitamaduni kabisa yenye ukweli 90%

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.
 
Mimi na baba yangu mzazi tunafanana kop kwem, like batteries...lakini hizo alama za mikono hazifanani. Mimi na mwanangu tunafanana hizo alama za mikono lakini sura ya mtoto wangu ni mama yake hata alizaliwa na vidole 6 kama bibi yake upande wa mama.

Kuna mambo mengi sana ya kijinga yalitamkwa zamani yakiwa na lengo la kuwatisha watu wasifanye mambo fulani lakini ukiangalia uhalisia wake ni 30% - 0%.
 
Mimi na baba yangu mzazi tunafanana kop kwem, like batteries...lakini hizo alama za mikono hazifanani. Mimi na mwanangu tunafanana hizo alama za mikono lakini sura ya mtoto wangu ni mama yake hata alizaliwa na vidole 6 kama bibi yake upande wa mama.

Kuna mambo mengi sana ya kijinga yalitamkwa zamani yakiwa na lengo la kuwatisha watu wasifanye mambo fulani lakini ukiangalia uhalisia wake ni 30% - 0%.

Hata hivyo katika UZI wangu hakuna sehemu niliyoandika UNALAZIMISHWA kukikubali 100% nilichokiandika. Asante kwa kuja!
 
Hata hivyo katika UZI wangu hakuna sehemu niliyoandika UNALAZIMISHWA kukikubali 100% nilichokiandika. Asante kwa kuja!
Umeshapanic eeh! Kuna sehemu mimi nimesema umenilazimisha? Mimi nimetoa maoni yangu kuhusu huo utafiti wako ambao we unadhani ni unique.

I have a brother and two sisters. Hakuna hata mmoja wao anayefanana hizo alama na mwingine, japo wao watatu wanafanana na mama kweli kweli. Mi nakushauri, kama unataka kujifunza kitu kwa wazee wa kiswahili, basi jifunze ushirikina. Mambo ya kisayansi mapana
 
DNA ipi unayosema umeizoea au tu vile unaisikia kutajwa....!! Alama za vidole (finger print) ni kila mtu anazo zake hata kwa mapacha wafananao ziko tofauti, hiyo mbinu ipo na sana wanaangalia zile mikato/michoro kwenye kiganja (kama herufi M au N au W whatever) ila kumechi kwa mbali ni kesi chache sana.
 
DNA ipi unayosema umeizoea au tu vile unaisikia kutajwa....!! Alama za vidole (finger print) ni kila mtu anazo zake hata kwa mapacha wafananao ziko tofauti, hiyo mbinu ipo na sana wanaangalia zile mikato/michoro kwenye kiganja (kama herufi M au N au W whatever) ila kumechi kwa mbali ni kesi chache sana.
kwani huwa wanaangalia m n au w huwa ni mistari ya vidole vya mkono Fingerprint ndio tofauti na sio mikunjo mkuu..
 
Back
Top Bottom