Hii ndiyo DNA ya Kitamaduni kabisa yenye ukweli 90%

Hii ndiyo DNA ya Kitamaduni kabisa yenye ukweli 90%

Utafiti wako hauna uhalisia, "alama za mikono" hazifanani hata kwa mapacha. Siku nyingine ukitaka kujifunza njoo kwa wazee wa mikoani achana na hao wazee wa Dar, huku mikoani watakufundisha hata namna ya kutambua mwenye papuchi tamu,ndogo, kubwa nk
 
Mimi mtoto wa kwanza tunafanana sana lkn alama za viganjani hatufanani, yeye alama za N mimi M , mtoto wa pili anafanana na mama yake sura yangu hata haipo lkn alama za viganjani vinafanana,hapo naona sio kipimo halisi cha kujua biological child, ila kama baba na mama mnamakundi ya damu yanayofanana halafu mtoto kundi tofauti na lenu jua huyo mtoto ana wazazi watatu
Haya mambo ya kiganja sio ya mchezo mchezo hapa namuangalia mtoto mara tatu tatu naona mke ana Vibrate tu
 
Mimi na baba yangu mzazi tunafanana kop kwem, like batteries...lakini hizo alama za mikono hazifanani. Mimi na mwanangu tunafanana hizo alama za mikono lakini sura ya mtoto wangu ni mama yake hata alizaliwa na vidole 6 kama bibi yake upande wa mama.

Kuna mambo mengi sana ya kijinga yalitamkwa zamani yakiwa na lengo la kuwatisha watu wasifanye mambo fulani lakini ukiangalia uhalisia wake ni 30% - 0%.
Naunga mkono hoja mia kwa mia kama wabunge wa CCM bila kuweka neno LAKINI....
 
Hata hivyo katika UZI wangu hakuna sehemu niliyoandika UNALAZIMISHWA kukikubali 100% nilichokiandika. Asante kwa kuja!
asante kwa kuliweka hilo
mm na mwanangu tumepishana huyo mikato ila ni copy write
umenikumbusha enzi za Sheikh Yahaya (RIP) alivyotufundisha kutabiri viganja na alisema ni asilani haviwezi fanana na viganja vya mtu mwingine na alipendekeza kusoma kiganja cha kushoto
 
Mkemia Mkuu alisema 49% ya kesi zenye migogoro zilizopelekwa kwake kwa ajili ya kufanya vipimo vya DNA ndiyo wanaume walikuwa wamebambikwa. Siyo kweli kuwa 49% ya Watanzania wamebambikwa.
 
DNA ipi unayosema umeizoea au tu vile unaisikia kutajwa....!! Alama za vidole (finger print) ni kila mtu anazo zake hata kwa mapacha wafananao ziko tofauti, hiyo mbinu ipo na sana wanaangalia zile mikato/michoro kwenye kiganja (kama herufi M au N au W whatever) ila kumechi kwa mbali ni kesi chache sana.
HAJASEMA FINGERPRINT AMESEMA MISTARI YA KIGANJANI
 
Huu ndio upumbavu tunao ukemea kanisani.
 
Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Sasa kipimo cha nini kama hakuna action kama matokeo ni kinyume?
 
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.
Akili ya kuambiwa changanya na yako
 
Mke wa brother wangu kajifungua premature na bado yuko Muhimbili. Jamaa si kauona huu uzi, kawaganda manesi eti wamruhusu angalau kidogo amuone mtoto!! Brother hizi findings hizii, utaua watu! Hajasema ila nahisi anataka kufanya hii DNA test uliyofundisha hapa!!! Michirizi ikitofautiana tu jua kuna street child kaongezeka manake kaka yangu akili zake anazijua mwenyewe!!
 
Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Je, ina maana alama za baba kwenye mikono yake yote miwili inafanana? Je, ya mtoto nayo inafanana? Kwa maelezo yako kama mikono ya mtu mmoja haifanani hiyo mistari basi hiki kipimo ni fake kwa sababu kama mkono wangu wowote ule utafanana na wa mtoto wa kushoto basi na yangu itakuwa sawa ila nikiangalia sio sawa.

Basi finger prints zisingetumika kumtambulisha mtu au kumtofautisha mtu. Halafu genes zinabeba information ya generations nyingi zilizotangulia ukiweka na evolution sio rahisi kutumia human sense na kutumia finger and palm prints kufananisha watu.

Procedure mbali na process ya hiki kipimo ikoje? Na variables gani ambazo unaziangalia (mfano: width, length, distance between lines/ creases, number of lines/ creases)?
 
sawa mtoa mada utafiti wako ni mzuri,lkn hebu tuambie wewe ulipothibitisha ndivyo ilivyo?!!
 
Back
Top Bottom