Kwa mujibu wa kanuni za chaguzi za CCM, sifa ya elimu anayotakiwa kuwa nayo mbunge ni Elimu ya Darasa la Saba. Nadhani mjadala ukielekea huko utakuwa na tija zaidi ili kama kuna haja ya kufanya marekebisho basi hoja zijengwe in that context. Vinginevyo kwa mujibu wa kanuni za chaguzi za CCM, Mheshimiwa Azzan ni mbunge halali kwani Per kanuni za chama cha mapinduzi as of today, mgombea akiwa na kiwango cha elimu cha form four, form six, certificate, diploma, degree, n.k, hiyo inachukuliwa kama ni ziada tu na haipewi uzito na vikao vya kupitisha/kuchuja wagombea. Suala la elimu kwa sasa ni suala la wapiga kura mmoja kwa mmoja kuwa na uelewa tu kwamba je, itumike kama kigezo au lah.
Na mara nyingi ukiwa mgombea mwenye elimu kubwa, ni kawaida sana kujengewa fitina kwamba umechakachua au kampeni zako haziwatendei haki wagombea wasio na elimu, au kwamba peleka elimu yako kwingine ukajenge taifa, sio kwenye nafasi ya ubunge kwani mujibu wa kanuni ya CCM, darasa la saba linatosha, na wananchi hawana haja ya kuzingatia kiwango cha elimu kama ni kigezo cha kukuchagua kama mgombea/mbunge. Nadhani mjadala ungeelekezwa zaidi juu ya kanuni hii badala ya kumjadili Mh Azzan ambae katika mazingira haya, hana hatia na ni mwakilishi halali wa wananchi wa jimbo la Kinondoni.