Hii Ndiyo CHADEMA 1992 - 2013

Kwanza nipongeze chadema kwa kuendelea kukua kulingana na takwimu hizo ni jambo jema na lapendeza. Lakini si takwimu za kujisifia sana. Kuna mambo mengi yanapaswa yafanyike kabla ya 2015 ili kukijengea chama taswira + ambaya itakuwa endelevu kwa manufaa yake. Mathalani swala la kiuchumi haliko sawa sana chama kinatakiwa kiangalie je kinakikowapi kiuchumi...? Kuna vitegauchumi gani? kimepiga hatua gani katika kukifanya kisiwe tegemezi sana kwa wahisani?, Je idadi ya wanachama inatia moyo? Na kama inatia moyo je kuna mfumo sahihi wa kueka kumbukumbu za wanachamaa halali na waaminifu? Je uungwaji mkono wa chama maeneo mbali mbali ya nchi imeongezeka kiasi gani? Je chama kina uwezo wa kutengeneza fursa za kiuchumi ? Je chama kina Ofisi za kueleweks kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya chini ya chama ? Je chama kina demokrasia katika kuchagua uongozi na kuhakikisha kuwa uongozi huo ni endelevu kuanzia Taifa mpaka chini ?. Nazani kama cha kitazingatia hayo basi kitakuwa chama imara na chama kinachokuwa. Kinachotakiwa sasa ni kuwa cdm kinapaswa kwenda vijijini zaidi na zaidi kuelimisha watu kufungua matawi na ofisi za chama. Pili chadema kiwe makini na watu wanaohamia chadema na kuanza kutaka uongozi hapo hapo hasahasa wale wanaotoka ccm maana mamluki ndio hupitia huko. Ni imani kuwa kupitia viongozi thabiti wa chadema ....chama kitaendelea kuwa tunu kwa watanzania...
 
Msijidanganye cdm hz takwimu mnapaswa kuzitafakari kwa kina kwani ingawa chama kinaungwa mkono na watanzania wengi lkn chama kama chama bd hakija kuwa, nasema hvy kwa nn? Lazima mlinganishe toka mwaka 1992-2013 ki uchumi chama kikowapi kimepiga hatua gani , idadi ya wanachama halali na waaminifu imeongezeka kiasi gani! Uwezo wa kutengeneza fursa za kiuchumi ki chama imefikia wapi? Ofisi za kueleweks kuanzia Taifa mpaka ngazi ya chama zipo?uongozi endelevu kuanzia Taifa mpaka chini upo?. Nasema hvy maana natambuwa kuwa cdm hakijatekeleza hy ambayo ndi yanayoosha kama chama kimekuwa. .

Pengine ulikaa ukafikiri lakin hukutoka nje kuthibitisha baadh ya fikra zako, chadema kwenye uongoz haijaetereka kitaifa, kiuchumi usiongee kabisa hakuna chama TZ kinachofanya harakat kama CDM, CDM haikurupuk 1995 haikusimamisha mgombea urais kwan kilijua lazima chama kijengwe kwanza,sasa kimejengeka,karibu chadema,mbunge 1 ni zaid ya 10 wa ccm.polen ccm kwan katiba mpya itawazika rasmi 2015.
 
Yees chama kinakua sana lakini ccm haiwezi kutolewa 2015 bado itabaki. Naomba msinitukane.
 
Punguzeni uchaga chamani

AP179326965832-1280x960.jpg
 
Yees chama kinakua sana lakini ccm haiwezi kutolewa 2015 bado itabaki. Naomba msinitukane.

Swali kwa wanaCDM,mnatukanaga mambulula? Msimtukane,anahitaji ukombozi na maombi ili atokwe na shetani mwigulu
 
Hakuna dalili ya huko tunakoenda kuwa maisha ya watz yatakuwa mazuri ila dalili ni kuwa yatakuwa magumu zaidi, wenye nafasi watanemeka na wasionazo wataendelea kupigika, hali hii itakua mbaya kwa ccm na hali nzuri kwa cdm, kama ccm wanaahitaji kuwa madarakani ni vyema wabadili mwelekeo wa maisha ya mtz vinginevyo wananchi hawatakuwa upande wao bali watakuwa upande wa cdm... maisha magumu ni sera nzuri ya mpinzani ktk majukwaaa ya siasa na ni nafasi mbaya kwa ccm katika majukwaa ya siasa. ccm washukru kuwa watz ni wavumilivu ingekuwa watz ni sawa na nchi nyingine za afrika mfano kenya ccm toka 2010 wasingekuwa mjengoni. kinachonisikitisha wao wanajiona wako sawa.
 
Filipo Lubua asante sana kwa mchanganuo
nasema yes this is it.

Pamoja na changamoto mbalimbali chaa hiki kilizozipitia, bado kimeendelea kuimarika kila uchao uchwao. Kuna wale wanaobeza kuimarika kwa chama hiki, na kukifananisha na vyama vingine vya CUF na NCCR - Mageuzi, wakidhani kuwa kama ilivyokuwa kwa vyama hivyo, Chadema pia kitaporomoka. Ila watu hawa wanashindwa kuelewa kuwa Chama hiki hakijawahi kupoteza umaarufu wake, na zaidi tu kimekuwa kikiuongeza.

Swala hili linathibitishwa na idadi ya viti vya udiwani na Ubunge ambavyo chama hiki kimekuwa kikivipata katika kila uchaguzi mkuu, tangu 1995. Leo tuangalie tu takwimu fupi za udiwani na ubunge kwa Chama hiki.

Mwaka
Madiwani
Wabunge
1995
42
4
2000
75
5
2005
103
11
2010
467
49

Kwa kuzitazama takwimu hizi rahisi, utajifunza kuwa pamoja na hujuma nyingi, wizi wa kura, na fitina mbalimbali kutoka vyama vingine vya siasa (vikiwemo CCM na CUF), pamoja na serikali kutumia vyombo vya dola kujaribu kukiporomosha, bado Chadema kimekuwa kikiendelea kujinyakulia viti vingi zaidi kila kiingiapo katika uchaguzi mkuuna zaidi sana, ongezeko limekuwa likiongezeka kila uchaguzi. Mfano, mwaka 2000 chadema kiliongeza kiti kimoja tu cha ubunge na mwaka 2005 kiliongeza viti sita vya ubunge na mwaka 2010 kiliongeza viti 38 (ukiongeza na vile vya viti maalum). Kwa mantiki hiyo, chadema kimekuwa kikikubalika zaidi kila miaka isogeapo. Wale wenye ndoto kuwa kitakufa, subirini kama hamtakiona kikiingia ikulu na nyie kubaki mnabung'aabung'aa tu.

Kwa wale mpendao grafu, takwimu hizi zinaweza kuonekana kama ifuatavyo. Chadema songeni mbele, hadi mfanikiwe kulikomboa taifa hili. Matumaini ya Watanzania wengi, hasa nguvu ya taifa (vijana), yako mikononi mwenu. Imarisheni umoja, mshikamano, maelewano na mapambano. Hatimaye mtalifikisha taifa letu pale ambapo CCM wameshindwa kwa zaidi ya miaka 50 sasa (nusu karne).

View attachment 97198
 
Hakuna dalili ya huko tunakoenda kuwa maisha ya watz yatakuwa mazuri ila dalili ni kuwa yatakuwa magumu zaidi, wenye nafasi watanemeka na wasionazo wataendelea kupigika, hali hii itakua mbaya kwa ccm na hali nzuri kwa cdm, kama ccm wanaahitaji kuwa madarakani ni vyema wabadili mwelekeo wa maisha ya mtz vinginevyo wananchi hawatakuwa upande wao bali watakuwa upande wa cdm... maisha magumu ni sera nzuri ya mpinzani ktk majukwaaa ya siasa na ni nafasi mbaya kwa ccm katika majukwaa ya siasa. ccm washukru kuwa watz ni wavumilivu ingekuwa watz ni sawa na nchi nyingine za afrika mfano kenya ccm toka 2010 wasingekuwa mjengoni. kinachonisikitisha wao wanajiona wako sawa.
Kweli tupu Agwambo! ccm wakiona rushwa inatembezwa mbele ya macho yao wanalalamika na kunyamaza. ARV feki zikitengenezwa wanampa mtengenezaji cheo. Wanamtwara wakilalamika kwa nini ilani ya ccm ya 2010 haitekelezwi ccm wanawapelekea vikosi vya jeshi kuwapiga, akitokea mwanaccm kumtembeza mgonjwa wa akili kwenye kampeni kuomba kura ccm kimya kana kwamba hicho ni kitu halali.Mungu akamleta daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya moyo ili asaidie kukomboa sekta ya afya kwenye tasnia
ya matibabu ya moyo. ccm wakamnyanyasa mpaka akafariki.Daktari huyu(Ferdinand Masao) angeweza kabisa kuunda kituo
cha matibabu ya moyo kinacholingana au kuzidi appolo ya India.Daktari kafa hivihivi maccm yakimtazama! Hivi kweli huko cccm
hakuna mwenye upeo na uchungu wa nchi hii?
 
Mwamko wataupata tu manake shida hazidanganyi. Maisha yamekuwa magimu na kila mtu yukoalert kuwa tumeingia chakani. Wenyewe tutaenda kupanga mstari kupiga kura. JK kaza bolt hizohadi tunyooke!
Hivi ni kweli watu hawajitokezi kupiga kura au hawajitokezi kujiandikisha kupiga kura.....? Maana huwa kwa ukweli siziamini sana takwimu zinazotolewa kabla ya kupiga kura....tangu daftari limeanzishwa mbona hakuna updating procedures hadi ufike muda wa kupiga kura....? Mi naona tume ya uchaguzi iwe kama ya Usajili wa vizazi na vifo kila mtu akishafikisha 18 yrs akachukue kitambulisho chake....kwani kipindi hiki hatuna uchaguzi...wafanyakazi wa tume wanafanya nini...?
 
Back
Top Bottom