Hii ndio tofauti ya Vita vya Ukraine/Russia na M23/Congo au Israell/Hamas

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,373
Naangalia Clips za Huko Kivu, utagundua tofauti kubwa kati ya vita vya wazungu kwa wazungu nq vita vya Watu masikini (Waafrika) wa kipato.

Utagundua.
1: Wazungu hawaonyeshi raia wao wakilia njaa. Barkhmut (Ukraine) zilipigwa risasi na mabomu mji mzima kuliko sehemu yoyote duniani tangu nizaliwe. Mji wote kama DSM ukabaki mapagala hakuna hata mjusi, Lakini sijaona hata wakazi wa Bakhmut au Soleder wakifa kwa maelfu, wakikimbia na magodoro na ndoo za maji, wakiwa katika makambi ya wakimbizi walilia njaa. Hata kusikia Zelensky anaomba msaada wa Chakula US zaidi ya Kuomba silaha.

2: Hapa naangalia raia wa Kibumba akilia na kuilalamikia nyumba yake kubomolewa na M23 na RDF. Utaona wakazi wa Kivu wanakimbia na mabata, kuku, magodoro makuukuu, na vitu vingi duni hata hawajui wanaenda wapi. Hii Ukraine sijaona kabisa. Jamaa namuona analilia nyumba yake. Inawezekana hata ametumia miaka 30 kujenge nyumba duni kabisa, Sijawahi kuona mzungu kwenye vita ya Ukraine analilia nyumba, mifugo yake au mashamba au Kibarua alichopoteza kwa sababu ya vita.

Nishauri Rwanda Congo na wahusika wa vita hivyo, tuache kuongeza vita juu ya vita. Raia wa maeneo yetu huku bado ni masikini sana. Wanakabiliwa na uamsikini mkubwa, hii ni vita kubwa ambayo risasi na mabomu yake yanatukumba hadi sisi huku Legangabilili, Tunapambana bila mafanikio. Kukubali kutumika au kujitumia kuuana ni kuongeza umasikini wa mtu mweusi. Ni hujuma kwa harakati za mtu mweusi.

Ni hayo tu.​
 
Vita ni vita japo umaskini na hali ya Congo inasikitisha. We Kagame na Museveni, kuna siku ya hukumu ya Mungu. Utalia na kusaga meno. Acheni kuua wenzenu kisa mali za dunia zinazopita.
 
Umasikini ukijumlisha na vita huleta maumivu makali sana. Wale raia huwa nawahurumia sana nikivaa viatu vyao.
 
Eti ee!! Endelea kuyaona na kuyasikia kwa wenzetu ila omba yasikukute
Bara Lina matatizo kila angle. Zawadi pekee ambayo Mungu katupa waafrika ni UWEZO WA kuya adapt haya matatizo na kuona kama sehemu ya maisha yetu.
 
Naangalia Clips za Huko Kivu, utagundua tofauti kubwa kati ya vita vya wazungu kwa wazungu nq vita vya Watu masikini (Waafrika) wa kipato.

Utagundua.
1: Wazungu hawaonyeshi raia wao wakilia njaa. Barkhmut (Ukraine) zilipigwa risasi na mabomu mji mzima kuliko sehemu yoyote duniani tangu nizaliwe. Mji wote kama DSM ukabaki mapagala hakuna hata mjusi, Lakini sijaona hata wakazi wa Bakhmut au Soleder wakifa kwa maelfu, wakikimbia na magodoro na ndoo za maji, wakiwa katika makambi ya wakimbizi walilia njaa. Hata kusikia Zelensky anaomba msaada wa Chakula US zaidi ya Kuomba silaha.

2: Hapa naangalia raia wa Kibumba akilia na kuilalamikia nyumba yake kubomolewa na M23 na RDF. Utaona wakazi wa Kivu wanakimbia na mabata, kuku, magodoro makuukuu, na vitu vingi duni hata hawajui wanaenda wapi. Hii Ukraine sijaona kabisa. Jamaa namuona analilia nyumba yake. Inawezekana hata ametumia miaka 30 kujenge nyumba duni kabisa, Sijawahi kuona mzungu kwenye vita ya Ukraine analilia nyumba, mifugo yake au mashamba au Kibarua alichopoteza kwa sababu ya vita.

Nishauri Rwanda Congo na wahusika wa vita hivyo, tuache kuongeza vita juu ya vita. Raia wa maeneo yetu huku bado ni masikini sana. Wanakabiliwa na uamsikini mkubwa, hii ni vita kubwa ambayo risasi na mabomu yake yanatukumba hadi sisi huku Legangabilili, Tunapambana bila mafanikio. Kukubali kutumika au kujitumia kuuana ni kuongeza umasikini wa mtu mweusi. Ni hujuma kwa harakati za mtu mweusi.

Ni hayo tu.​
Mzee unatakiwa kujua hiyo Ukraine ilikuwa ni Sehem ya usoviet so inashelta kama zote kuna miji huko chini wakizama utaua wachache
 
Ni maumivu makubwa mno. Na ule mgogoro unachochewa na USA. Akimtumia Rwanda... Kuna Picha mdogo wangu alinitumia za mauaji huko. Ni za kutisha. Yaani huko ni sawa na jehanamu Kwa mateso wanayoptia
 
Back
Top Bottom