Hii ndio Tanzania yetu

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Hii ndio hali halisi ya Tanzania yetu...! Hivi hawa wananchi utawaambia kuhusu katiba mpya wakuelewe unamaanisha nini?


Tanzania yetu 2.JPG


Tanzania yetu 3.JPG


Tanzania yetu 1.JPG
 
Hapo ni wapi?? Sehemu kama hizi msimu wa masika si wa kusafiri!!
 
Hii ndio hali halisi ya Tanzania yetu...! Hivi hawa wananchi utawaambia kuhusu katiba mpya wakuelewe unamaanisha nini?

Ukiiwaambia Katiba hiyo itawabana watu wasipeane kazi kinyemela na hivyo kupelekea utendaji kazi bora watakuelewa
 
Hii ndio hali halisi ya Tanzania yetu...! Hivi hawa wananchi utawaambia kuhusu katiba mpya wakuelewe unamaanisha nini?


View attachment 22449


View attachment 22450


View attachment 22451


Huu Umasikini Utakwisha lini jamani? Tuna dhahabu tuna almasi, Tuna Madini ya kila aina tuna Gasi, Tuna Mali Asili nyingi lakini kitu kimoja tu hatuna nacho ni Viongozi wa kuipenda Nchi yetu ndio hatuna Karibu Viongozi walio Madarakani wengi wao ni Mafisadi je kweli nchi yetu itaendelea jamani Kiuchumi? nauliza hilo Swali ndugu zangu Wana Jamii Forums.
 
Hapo ni wapi?? Sehemu kama hizi msimu wa masika si wa kusafiri!!

mKUU SAfari zingine sio za kupenda/kupanga, saa zingine matatizo (Misiba, Ugonjwa) yanaweza kukufanya ufanye safari muda wowote
 
Mtoa mada hawajui watanzania, anafikiri watanzania wenye uelewa wa mambo wapo kwenye lami tu, hajui kama hata humo kwenye hayo mafuso yaliyozama kwenye matope kulikuwemo na great thinkers(mimi ni mmoja wao). Hao wanajua umuhimu wa katiba mpya kuliko hata wale ambao hawajui kama tanzania kunawilaya ambazo zinafikika kiangazi tu( tena kwa tabu).
 
Duh! Hii inanakumbusha kule Kigoma enzi zilee! Kuna eneo linaitwa kidongo chekundu barabara ya kwenda Uvinza, shughuli yake ilikuwa pevu!
 
Kwa mtu mwenye akili kwa hizo picha hutakiwi kusoma kujua kama kitu hakiko sawa - kati ya uongozi wa nchi, Katiba, etc. Wakijua kama ni wajibu wa serikali kuwapa barabara na haijawapa, lazima wajue wanahitaji mabadiliko yatakayohusisha uandikwaji wa Katiba mpya.
 
Gravel roads are very difficult to use during rain season! We are poor, in most cases we need to be granted some funds from the donors to solve our problems. For sure, development will remain to be a dream to us as long as we depend on help in order to solve very important issues !!!
 
Kinachoniudhi ni watu na taaluma zao wanoweza kutusaidia kutatua yanayotusibu lakini tunaishia kwenye siasa ambazo kikweli ni zinaishia kwenye theory na siyo practical. Kila saa mafisadi mafisadi mafisadi mafisadi, tuna rasilimali tunarasilimali. Tukiitwa kuisaidia kagoda ndiyo wa kwanza kuwasaidia kushinda kesi, kuwaandikia mikataba, kuaandikia business plan, kuwaandika magazetini kila siku kama ni sifa au kutafuta umaarufu. Jamani tuwapeleke mahakamani hawa watu, siyo kubweka tu? Ohh nimesema Jakaya mwizi kama anabisha aende mahakamani asipoenda kweli mwizi badala ya mwizi kupelekwa mahakamani tuache uhuni tuijenge hii nchi maana imeishia mikononi mwa wanasiasa na majambazi wachache wanaotumia makelele ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom