Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,217
- 1,706
UKIMJUA ANAEKUCHUKULIA MUME UTACHUKUA HATUA GANI?
Mambo ya kuchukuliana waume si mapya kabisa kuyasikia lakini likikukuta ndio utajua maumivu yake.Namna ya kukabiliana na maumivu hayo inahitajika busara ya hali ya juu kwani kama si busara unaweza kufanya lolote lile....
Kuna dada yeye alichukuliwa mume na moja ya marafiki zake yeye alichoamua ni kukusanya kikundi na kigoma cha Uruguay kwenda kumkomesha mbaya wake...
Kwanza walianzia bar wakapata kinywaji ili kujipa mzuka wa shughuli yenyewe...
Kisha wakawasili nyumbani kwa mchukua mume huyo ambako anaishi na wazazi wake na kuanza kuserebuka vigoma ambavyo vinaambatana na nyimbo za vijembe.
Wenye kazi yao shughulini ili mradi wamelipwa...
Aliyechukuliwa mume...
Wakati haya yakiendelea mlengwa hakupepo nyumbani kwao isipokuwa baba mzazi alikuwepo,ukiangalia kwenye picha utamuona kasimama mlangoni anaangalia yanayoendelea hata haelewi maskini baba wa watu.
Haya ndio mambo yaliyopo ila mimi naona ipo njia ya kudeal na mbaya wako kuliko hii.Pia kwa nini usideal na mumeo kwanza ambae amekiuka makubaliano yenu?una uhakika gani hatamgundua kimada wake mwingine?utawapigia vigoma wangapi?
Hiyo ni mitizamo yangu lakini dunia uwanja wa fujo kila mtu anacheza ngoma aitakae huwezi kumzuia mtu kufanya lake.
from Dina Marios(dm)