Hii ndio jamii ya Jamiiforums

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,215
56,855
Humu tumo mkusanyiko wa watu wengi ambao tumeunda jamii hivyo tumesadiki nadharia ya Jamii ambayo ipo katika mfumo wa forum!.
Nitaielezea kidogo jamii ya jamiiforum kwa makundi machache huku nikitoa na mifano ya baadhi ya member hao,here we go.

Wanasiasa wa jamiiforum.
Hawa huongoza katika kuchangia jukwaa la siasa nakuleta mada zenye mlengo wakisiasa,bila shaka hawa itakuwa ni watu wenye umri wa utu uzima ambao maswala ya kisiasa huyaona katika athari zaidi ya umri tofauti na wao.
Mfano Mzee Mwanakijiji.

Wana intelligence.
Tofauti nazamani vichwa katika jukwaa hili au jamii,walikuwa ni wengi hata kupelekea jukwaa la intelligence kuwa lamoto kwa mada kemkem na mijadala ambayo ilikuwa na taarifa za kina. Mfano Habibu B. Anga pamoja na Kiranga huku bila kusahau watu wa upande wapili katika mambo yakiroho Mshana Jr na Karim.

Business man.
Zaidi utawakuta jukwaa la biashara na uchumi wakijadili maswala ya biashara na uchumi.
Mada nyingi huko zimekuwa zikifundisha ama kuuliza maswali au kutoa ushauri n.k
Mfano CONTROLA.

Mapenzi na mahusiano.
Hili ndio moja ya jukwaa lenye wachangiaji wengi zaidi maana nyanja hii nafikiri humgusa kila mtu zaidi zaidi vijana ambao ndio wengi wapo katika hii forum.
Mada za kuachwa na kuacha zimejaa humu,huku visa na Mikasa vya mapenzi vikijaa humu!.. moja ya wachangiaji mahususi wakiwa ni Depal akiwawakirisha jinsia ya kike na KENZY mwenyewe akiwakilisha jinsia ya kiume.
Member wengi katika jukwaa hili utawakuta pia jukwaa la chitchat.

Wachawi wa jamiiforum.
Naomba hii sekta nisiizungumzie Sana niweke tu yule mnaemfahamu Mshana Jr 😂😂.

Madaktari wa jamiiforum.
Hawa hutusaidia katika maswala ya afya kupitia jukwaa la jf doctor. Huko utapata ushauri juu ya matatizo mbalimbali yahusuyo afya.
Mfano Mzizi mkavu na Sky Eclat.

Wasomaji tu.
Hawa zaidi huwa ni wasomaji nasio wachangiaji!,mtu yupo humu miaka nenda rudi lakini id yake bado ina komenti zero na mods nao huzidumaza id izo kwa kuziacha zisomeke "member" nawakati ni wambea walio kubuhu.😎
Hawa wanajijua hakuna cha mfano!.

Wala bata.
Hawa ndo wale member ambao kwao kunywa bia na starehe nyengine ndio kama pumzi zao za kila siku!. Hawa hata macho yao nafikiri yamekaa kilevilevi tupu..😂
Huwakuti siasani,ukiwakuta kwenye mapenzi basi jumbe zao ni fupifupi tu utakuta kaandika "Mtaachana tu!".
Mfano Evelyn Salt 🏃

Watoa likes.
Hawa huwa nawaonaga huwa hawana msimamo na wengine hawajui walifanyalo..!
Sijasema muache la hasha bali muda mwengine mwachekesha!. Unakuta mada mtu kaeleza juu ya kitu fulani so anatokea mtu anapinga hapa utakuta mtu ka like kote kwa hawa watu!.. wengine kitu hakichekeshi unakuta kalike kwa emoj ya kuchekesha!.
Let's be serious unakuta mada ya Tanzia mtu kalike hivi 🤣.
Mfano mkwepu jr na Extrovert.

Wabishi.
Hawa hata sita tag mtu maana watakuja kunibishia na hapa!. Hawa hata kama ulete uthibitisho watakubishia ilimradi ashinde yeye!.

Member wapole.
Hawa zaidi sio wachangiaji sana japo huchangia kiasi hata komenti zao huwa zinaonyesha hulka zao za upole na unyenyekevu. Mfano Me too na mkwepu jf japo huyu kukomenti huwa ni nadra.

Member waliokosa shipa la uvumilivu.
Hawa huumwaga ukweli bila kupindisha na mara nyingi huwa na dukuduku hawezi kukaa bila chochote kitu Evelyn Salt utawataja wenzako ila njooni taratibu waku..😂

List bado inaendelea...
 
Wakongwe
Hawa ndo watu waliokula chumvi katika jamiiforum.
Wengi wao naona hawana utoto na ukongwe wao huonekana pasi na shaka.
Nyani Ngabu

Vitoto vya juzijuzi.
Hawa ndo wasumbufu wa humu bado wananukia maziwa na wanastahili kuchapwa fimbo
babyfancy pamoja na Ed Kawiche. Nyie mnatakiwa mkae kwa kutulia acheni fujo vijana..😂

Wanaoteseka na mapenzi.
Sasa hawa ukikutana nao ndo wale wenye visirani maana wameshapigwa na vitu vizito kichwani!,hawa wakikuita majina mabovu vumilia tu si wao ni vitu fulanifulani vipo ndani yao..
financial services unaachaje kukaa hapa..?😂
Da'Vinci tunanena kimoyomoyo usipinge bro kaa kwa kutulia.

Member walioshindikana.
Sasa hawa Ban huwa ni vazi lao la humu!,wavunja sheria ndo hawa kanuni yao nafikiri huwa ni "sheria zipo ili zivunjwe!"
Kasomi upo au upo kwenye kifungo..? Waite na wenzako Kama wapo ndugu..😂

Moderator.
Kundi la muhimu ambalo huwezi lisahau kabisa,hawa ndo hutuhudumia humu Kama kufuta mada zetu,kutupa ban na kurekebisha mambo fulanifulani.
JamiiForums wakilisha wenzako ila punguzeni spidi kidogo.😅

Wafuatiliaji wa nje.
Hawa ndo walishagoma kujiunga katika jamii yetu ila tunatambua uwepo wenu tunachoomba tu mjiunge na mtandao wetu wa jamiiforum ili tuinue vyanyumbani pia.. NB: acheni umbea maana huko mitaani huwa tunakuta mmeyapeleka ya humu!.

Hiyo ndo list yangu ya Jamii ya jamiiforum na ningependa nitoe shukurani zangu kwa muanzilishi wetu Maxence Melo kwa kuwa na platform Kama hii ambayo tunaitumia kujadili Mambo mbalimbali.

NB:unaweza kuongeza list vile uonavyo.
 
duuuhh!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom