Otorong'ong'o
Platinum Member
- Aug 17, 2011
- 39,166
- 28,816
Naweza kuwatetea Kigoma na Rukwa, kwamba wako mbali mno na Dar.
Kuna huu mkoa jirani wa PWANI ambako ndiko mhe. Rais anatoka. Huu mkoa pamoja na rasilimali zote ilizokuwa nazo pamoja na proximity yake na Dar, ni masikini wa kutupwa kabisa. Ukifika hapo Kisarawe, Bagamoyo, Rifiji nk, kunanuka umasikini tu.
tedo,Wacha uongo wewe..Mkoa ganiupo jirani na Pwani ambao Rais anatoka....?????
Mikoa jirani na Pwani ni Dar, Moro na Tanga....
Au unamaanisha Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani..
Tabora Kigoma Rukwa Katavi Singida Lindi Mtwara Ruvuma na bado inaikumbatia ccm.Ama kweli umasikini ni mtaji wa ccm
Sijui ni vigezo gani umetumia lakini nafikiri Ruvuma na Kagera una ugomvi nao. Hawastahili kuwemo ktk kundi hili kwani wananchi wake (majority) angalau wanaweza kupata mahitaji ya msingi (Chakula, malazi, na makazi ya kuridisha, n.k ) kwa mwaka mzima bila kusumbuka sana ukilinganisha na mikoa kama vile Dodoma ambao haumo kwenye orodha yako. Nimetembelea mikoa yote mitatu na mingine ktk orodha yako kwa kweli hawastahili kuwemo hasa Kagera kuipa namba moja kwa umaskini umebugi (labda kama kuna mhaya alikutapeli kimapenzi maana kwa mambo hayo hawajambo, hasa ukiwaendea macho juu). Wanaweza pia kulipia mahitaji ya msingi kama elimu kwa watoto wao nk
1.tabora................
Nashangaa wazanzibar wanavyolalamika muungano unawanyonya au unapendelea bara,wakati hata mikoa hii mi 3 bado nayo iko nyuma kutokana na kero za muungano lakin haijawah kudai tanganyika yao.
Makazi ya kuridhisha yapi kwani hiyo mikoa iliyobaki hawana makazi ya kuridhisha labda umuulize mtoa mada katumia vigezo vipi maana hali ya mikoa hiyo kimaisha ni sawa tu. Na nilijua kusudi watu watapinga uwepo wa Kagera kwa kuwachukulia wahaya wanavyoishi nao mjini nendeni mkaishi nao kule ndo mtawajua vizuri na kama unazungumzia huduma za jamii ndo sababu hata mikoa mnayosema imeendelea nenda Arusha, Mbeya n.k kuna maeneo mengine huduma za jamii ni kitendawili huko vijijini lakini bado utakuta hicho kijiji kipo kwenye mkoa ambao makao makuu yake yanahadhi ya jiji.
usikimbie ukweli mkuu, usisifie kitu kwa kuangalia upenzi, Mtwara bado iko nyuma na wala usitishwe na hyo gas iliyopatika huko, embu cheki mfano wa dhahabu na mkoa wa shinyanga
Hakuna mji wenye sida ya maji kama Arusha,...Khaaa!!!
Sijui ni vigezo gani umetumia lakini nafikiri Ruvuma na Kagera una ugomvi nao. Hawastahili kuwemo ktk kundi hili kwani wananchi wake (majority) angalau wanaweza kupata mahitaji ya msingi (Chakula, malazi, na makazi ya kuridisha, n.k ) kwa mwaka mzima bila kusumbuka sana ukilinganisha na mikoa kama vile Dodoma ambao haumo kwenye orodha yako. Nimetembelea mikoa yote mitatu na mingine ktk orodha yako kwa kweli hawastahili kuwemo hasa Kagera kuipa namba moja kwa umaskini umebugi (labda kama kuna mhaya alikutapeli kimapenzi maana kwa mambo hayo hawajambo, hasa ukiwaendea macho juu). Wanaweza pia kulipia mahitaji ya msingi kama elimu kwa watoto wao nk
Chunguza dini iliyotamalaki huko ndo utajua..
mkuu umenichekesha ivi unafikiri mtu mmoja ndo anaweza kuleta maendeleo au unataka kuniambia kule mbeya sugu ndo amepafanya pawe vile au huijui vizuri historia ya nchi hii? toa mikakati ya kweli ci kutuletea porojo kama za wanaojiita ukawa.
Una maslahi binafsi Sizinga (Signature yako nimeiona...declare please!)....ni kweli Mtwara na Lindi zitakuwa mbali sana kiuchumi miaka ijayo kwa hii gesi asilia