Hii Mikoa Nani Kailoga?

Hii Mikoa Nani Kailoga?

Nashangaa wazanzibar wanavyolalamika muungano unawanyonya au unapendelea bara,wakati hata mikoa hii mi 3 bado nayo iko nyuma kutokana na kero za muungano lakin haijawah kudai tanganyika yao.
 
Watu tu wajitume kufanya kazi ndo tutaendelea kusini yetu. Hasa Gas ambayo imepatikana Mtwara tusiposhikana mashati kipindi hiki tutabaki hivo hivo.
 
Hili ni suala la kiimani kwa wale wanaoamini.kuna vifungo vya kiroho hivyo kimwili hatua haziwezi kupigwa.
 
Watu tu wajitume kufanya kazi ndo tutaendelea kusini yetu. Hasa Gas ambayo imepatikana Mtwara tusiposhikana mashati kipindi hiki tutabaki hivo hivo.

Eti gas!!! Katika vitu vilivyowahi kugunduliwa tanzania na kupewa hadhi ya kulikomboa taifa na umasikini basi gas ni namba nne!! Ilipogunduliwa dhahabu tulisema kwa heri umasikini, tukaja kugutushwa na almas, mara tanzanite, wimbo ni huo huo, kwa heri umasikini, ilipogundulika uranium tukashangilia kweli kweli kuwa sasa umasikini bye bye, lakini leo hata ukimuuliza mtz kama anajua kuwa hiyo kitu inachimbwa hapa atasema hajui, labda hatujajua bado tatizo la ufukara wetu, labda hata tatizo si rasilimali.
 
Mikoa masikini na isiyoendelea Tanzania hii japo kuna mingine wanatokea wapenda sifa.

1. Kagera
2. Lindi
3. Rukwa
4. Kigoma
5. Singida
6. Tabora
7. Mara
8. Ruvuma
9. Pwani
Mikoa hiyo nichoka mbaya kuliko hata huu

10. Mtwara.
 
Suala la kusema haiendelei kisa Islamic Culture na Umwinyi sio kweli maana Hata Tanga nako ni Pwani ila ni Jiji.
 
Tafadhali bwana,kagera mambo super wewe.kila kona ni lami aisee.
 
Matatizo ya watanzania yanafanana: umaskini wa kipato upo katika maeneo ya kila mkoa. Magonjwa yako katika kila mkoa Tanzania hii. Njaa iko kila mahali, vifo vya watoto na akina mama waja wazito vipo. tembea uone maisha ya watanzania.
 
Mkoa wa pwani ni masikini kuliko tunavyofikiri!! Kuna watu hata hawajui kama kuna mkoa unaoitwa pwani, ni masikini wa kila kitu kuanzia rasilimali, uwajibikaji hadi akili, hii mikoa mingine angalau watu wanajitahidi kujituma ila tu hawajapata uongozi bora, watu wa pwani hata uwagawie millioni mia mia watazimalizia kwenye ngoma na ngono tu, huu ndiyo ukweli mchungu.
 
Sielewi mwansisha mada na wachangiaji wengine wako ulimwengu huu ama ahera...Mtwara unaiweka kundi la mikoa duni ?tena kwa nyakati hizi....Hahahaaaaa, inafurahisha!! Macho na masikio ya serikali yetu hii na dunia nzima yanaelekezwa Mtwara...Ujeuri wa viongozi wengi sasahivi ni kwasababu ya Mtwara... "Mtwara Kuchele"
usikimbie ukweli mkuu, usisifie kitu kwa kuangalia upenzi, Mtwara bado iko nyuma na wala usitishwe na hyo gas iliyopatika huko, embu cheki mfano wa dhahabu na mkoa wa shinyanga
 
ongeza na Mara

Weeeeeeee, wilaya gani ? Bunda, Serengeti, Musoma, Tarime inayolisha wilaya nyingine za mkoa wa mara, labda Rorya ambayo ni wilaya mpya. Mara unaifahamu wewe au unaambiwa ? Waulize Wana Mara watakwambia kuliko kuwasemea.
 
Hapa ndio unapoonekana umuhimu wa somo la historia kwa vijana wetu.
 
Unazungumzia hapo Mtwara mjini? Nenda huko vijijini mkuu huwezi amini kama uko Tanzania.Umasikini unatisha!

Kwani unaposema Arusha ni jiji imeendelea umeenda vijijini ukajionea wamasai na wambulu wanaishije? Mwanza na Mbeya unadhani umasikini na mandhari ya jiji hata vijijini ipo? Huko mbali hata hapa Dar umeenda kule uzaramoni ukaona maisha yapoje ndugu au unamaanisha magari na foleni za hapa jijini ukadhan mkoa wote umeendelea..
 
Mkoa wa pwani ni masikini kuliko tunavyofikiri!! Kuna watu hata hawajui kama kuna mkoa unaoitwa pwani, ni masikini wa kila kitu kuanzia rasilimali, uwajibikaji hadi akili, hii mikoa mingine angalau watu wanajitahidi kujituma ila tu hawajapata uongozi bora, watu wa pwani hata uwagawie millioni mia mia watazimalizia kwenye ngoma na ngono tu, huu ndiyo ukweli mchungu.

Tatizo huu mkoa upo jirani na dar sijui ila raia wake na unamaisha duni kuliko watu wanavyo jisahaulisha hapa.
 
Back
Top Bottom