Hii Logic ipo sahihi..?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,681
106,791
Habari 👋
Wajuzi ningependa kujuzwa zaidi kuhusu hili.
It's a geometry of belief, makanisa ya kikatoliki hasa jimbo kuu la mkoa fulani hua limejengwa katikati ya mji. Yaani sehem inapoonyesa kwamba hapa ndio kati ya mji basi kanisa (Jimbo kuu) linakua limejengwa hapo. Sio kwenye clock tower or anything bali kwenye ile Quadrant inayonyesha kwamba hapa ndio kati.

Nimejaribu kuchunguza kwenye majimbo makuu niliyowahi kuhudhuria nimeona ni kwelii. Mfano, St. Joseph Cathedral Dar es salaam haipo mbali na eneo la Posta, St. Theresa Arusha halipo mbali na city center (Kroko wenyewe wanaita hivo), St Joseph Zanzibar lipo mbele kidogo tu ya Center, jimbo kuu la Shinyanga lipo mjini kati pia nimesahau eneo linaitwaje. Nk nk.

Logic ya kufanya hivyo ilikua kwamba kujenga kanisa katikati ya eneo fulani kunafanya watu wote wawe sawa mbele za Mungu.
Hivyo hivyo altar hujengwa katikati.

So kuprove kama hii theory ni kweli ningependa watu mlio maeneo mbalimbali Tz nk mniambie kama huko pia makanisa makuu ya kikatoliki yapo katikati ya mji. City center... Nachukua data kuhakikisha hii theory.

Head's Up.
Mtu ukifa unazikwa kichwa kikiwa kimeelekea mashariki(East), Kiimani mashariki inamaanisha kuchomoza (Dawn/Rising) so Watu huzikwa wakiwa wameelekea Mashariki jua linapochomoza ili roho za marehe ziweze kupata mwanga wa jua lichomozalo.

It's weird right???? Life is weird too.
Lets keep living ✌️
 
Sio kweli. Kwanini?

Sababu kuu ni kuwa cathedrals nyingi hazikuwa cathedrals yalikuwa makanisa ya kawaida mpaka hapo parokia zilipokuwa nyingi ndipo zikapanda hadhi (kuwa na center ya parokia zote)

So in the beginning the cathedral was built as a normal church.

Kuhusu hilo la kuzika niliwahi kulisikia lakini sio strict ritual. Nayajua makaburi mengi ya Catholics ambayo haya face East.
 
Sio kweli. Kwanini?

Sababu kuu ni kuwa cathedrals nyingi hazikuwa cathedrals yalikuwa makanisa ya kawaida mpaka hapo parokia zilipokuwa nyingi ndio zikapanda hadhi.
Makanisa mengi yale ya zamani hasa yapo katikati ya mji. Labda sasa hivi ndio hawazingatii jambo hili.
So in the beginning the cathedral was built as a normal church.
Mkuu my logic is pinned to the fact that haimaanishi ni kanisa kuu au kigango but Karibia kila city center kuna kanisa katoliki hata kaa halitakua cathedral. Kama nakosea ndio hapo nauliza watu waliopo sehemu mbalimbali za miji wanieleze
Kuhusu hilo la kuzika niliwahi kulisikia lakini sio strict ritual. Nayajua makaburi mengi ya Catholics ambayo haya face East.
Binafsi naamini hii kitu ni strict ritual hata kama wafanyaji wa jambo hilo hawatakua na maana hiyo niliyoeleza. Sijawahi kuona kaburi ambalo halijaelekea East kwa wakristo na kwa waislam ndio kabisa lazima kaburi lielekee Kibrah/East hata wakati wa kuchinja lazima mnyama uelekee kibra
 
Tabora jimbo kuu la kumbu kumbu ya Arch bishop Mihayo(Saint Thereza) lipo kati kati ya mji.

Kanisa kuu Katavi (Mpanda) lipo kati kati ya mji pia.

Maeneo mengine huwa napita nikipuyanga tu sijawekeza uchunguzi.

Sana nitakuwa mila nipitapo 'mkoa' nafuatilia ku prove ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia jimbo kuu la kigoma lipo city center nilikua nimesahau. Ningependa more facts ili kuhitimisha theory hii
 
Makanisa mengi yale ya zamani hasa yapo katikati ya mji. Labda sasa hivi ndio hawazingatii jambo hili.

Mkuu my logic is pinned to the fact that haimaanishi ni kanisa kuu au kigango but Karibia kila city center kuna kanisa katoliki hata kaa halitakua cathedral. Kama nakosea ndio hapo nauliza watu waliopo sehemu mbalimbali za miji wanieleze

Binafsi naamini hii kitu ni strict ritual hata kama wafanyaji wa jambo hilo hawatakua na maana hiyo niliyoeleza. Sijawahi kuona kaburi ambalo halijaelekea East kwa wakristo na kwa waislam ndio kabisa lazima kaburi lielekee Kibrah/East hata wakati wa kuchinja lazima mnyama uelekee kibra
Yeah nakubaliana na wewe kuwa city centers nyingi zina makanisa. Kwa mtizamo wangu ni kwasababu kanisa katoliki ni kanisa la zamani ambalo limesambaa duniani mianga mingi iliyopita.

Hivyo basi kutokana na kuwa miji yetu haikuwa imeendelea sana basi kanisa lazima lingejengwa hapo hapo mjini na kadiri mji unavyokuwa (kumbuka mji unakuwa kwa kutanuka 'outward' in all directions) so it's obvious kuwa baada ya miaka mingi lazima kanisa litakuwa city center.

So hapo unaweza kuona chanzo ni wakati na sio kuwa ni suala la 'lazima iwe hivyo'.

Kuhusu makaburi hebu ngoja nianze rasmi sasa kufanya uchunguzi. Nitaleta mrejesho hapa ikiwezekana na picha.
 
Yeah nakubaliana na wewe kuwa city centers nyingi zina makanisa. Kwa mtizamo wangu ni kwasababu kanisa katoliki ni kanisa la zamani ambalo limesambaa duniani mianga mingi iliyopita.
Hivyo basi kutokana na kuwa miji yetu haikuwa imeendelea sana basi kanisa lazima lingejengwa hapo hapo mjini na kadiri mji unavyokuwa (kumbuka mji unakuwa kwa kutanuka 'outward' in all directions) so it's obvious kuwa baada ya miaka mingi lazima kanisa litakuwa city center.
Paragraph hiyo inaonyesha kwamba mamluka zinazotoa takwimu kwamba sehemu hii ndio city center hua wanakadiria tu au hua wanavipimo vya kijeografia.
Ukitumia kigezo kwamba shemu zilizokua zimekua ndio zilifanywa kua city center na hivyo makanisa makuu yakajengwa hapo utakua umekosea.
Mfano..Rombo na Old moshi ndio sehemu zilizokua zimekua naa kuendelea enzi hizo. Lakini je City center ipo rombo au old moshi? Jibu ni hapana lakini pia Cathedral ipo rombo au old moshi? Jibu ni hapana pia.

Hence, kukua kwa mji haikua kigezo cha kuwekwa cathedral bali wamisionari/Jesuist walipokua wanajenga makanisa enzi hizo walikua wanajua kabisa wapi ni katikati ya mji
So hapo unaweza kuona chanzo ni wakati na sio kuwa ni suala la 'lazima iwe hhivy
Kuhusu makaburi hebu ngoja nianze rasmi sasa kufanya uchunguzi. Nitaleta mrejesho hapa ikiwezekana na picha.
Nasubiri kwakweli nijifunze kitu kipya hata kama itakua ni picha za mitandaoni kutoka nchi zingine
 
Sikiliza bwana mdogo, naamini kuna conspiracy umeigundua ila unatumia "kunafanya watu wote wawe sawa mbele za Mungu" kama scapegoat ili kuendelea kufanya utafiti na kuprove hiyo theory yako kwasababu kiukweli ukiitafakari hiyo logic yako ni very unwarranted. Therefore usikate tamaa, komaa utakuja kujua wajerumani waligundua nini kwenye ardhi yetu.
 
Thinking differently is a dooe to the creativity.. but sometimes you might lost in the dark. Jig's Up
 
Back
Top Bottom