Hii kitu ninaitamani sana

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956

Basi uichome kwa moto utie pilpili na nyanya na kitunguumaji basi raha tupu jamani nitaipata wapi hii mihogo jamani????????????
 
MziziMkavu , nipe address yako nikutumie, mambo ya kutamani si mazuri.......
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu , nipe address yako nikutumie, mambo ya kutamani si mazuri.......
Asante bibie nitakupa inshallah miaka mingi hiyo kitu sijala yapata miaka 20 sasa nipo Ughaibuni Nime i miss sana MadameX














Ulaya hii kitu ni kama dhahabu hakuna kabisa mpenzi Madam X. Udenda unanitoka hapa nilipo wachaaaaaaaaaa wabongo mnafaudu kabisa.
 
muhogo wa jang'ombe!! ladhaye chiboko, mie naula huo usiku sana, au alfajiri sana!!
 
MziziMkavu vipi kuhusu CYANIDE iliyomo humo ndani haina madhara??
Mkuu Katavi
Muhogo ni mmea wa jenasi manihot na chakula muhimu katika Afrika, Amerika Kusini na nchi za Asia Kusini. Sehemu ya kuliwa ni hasa mizizi yake minene iliyo na wanga nyingi halafu pia majani yake yenye protini na vitamini.

[h=2]Sumu ndani ya aina za muhogo[/h]
Kuna aina kadhaa za muhogo zinazotofautiana hasa katika kiwango cha sianidi (cyanid) ndani yake. Sianidi ni sumu inayoandaliwa ndani ya mmea kwa umbo la kemikali linamarin. Linamarin hubadilika kuwa sianidi.
Viwango vya sianidi vinatofautiana kati ya spishi mbalimbali za muhogo. Aina zenye kiwango kidogo sana hazina matatizo lakini kwa jumla zao linatakiwa kuandaliwa kabla ya kuliwa.
Dawa ya sianidi hupotea kwa kuacha mizizi katika maji kwa siku mbili tatu. Njia nyingine ni upishi kwa joto kali kwa mfano kukaanga katika mafuta. Njia nyingine inayotumiwa hasa Afrika ya Magharibi ni kusaga mizizi na kukoroga unga katika maji; baada ya masaa kadhaa maji hubadilishwa na uji unapikwa kuwa aina ya ugali.

 
Last edited by a moderator:
katika vyakula nivipendavyo ni mihogo na matembele........hapa mmenidondosha,mimate hiihaaa
 

Ughaibuni gani huko DHL isikokuwepo, fanya fanya uje uamkie kidogo home na upunguze hamu ya mhogo pia.
 
Mkuu, Hii sasa ni kutiana hamu kwa kitu ambacho mtu huwezi kukipata, na hata ukikipata si quality ile uliyozoea. Mzizi ukiwa Mkavu bado hauishi utamu.....Ninauambulia nikienda vijijini hasa kule Tzaneen na Mapetla.
 
Ehee bwana dahh! umenikumbusha mbali sana,kuna jamaa bubu alikuwa akiikaanga pale daraja la mto themi arusha ilipokuwa matongee club sasa hivi nasikia nssf wamshusha mjengo, yaani ukipiga ki2 cha parachichi ni balaa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…