Hii kitu iko hivo kwenu pia?

Hii kitu iko hivo kwenu pia?

jogijo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
262
Reaction score
509
Wapendwa habari, nimeoa na bahati nzuri mke ni mjamzito kwa sasa, tatizo ni kuwa toka kawa mjamzito amekuwa kila akiingia jikoni anatapika, hivo ikabidi nimuweke sub, kidume nikaanza kuingia jikoni, kila nikitoka kazini, sasa hii hali imenipa taabu maana naona wakati mwingine ananiigizia, sisi wasukuma kwetu mwanaume haingii jikoni hata iweje, lakini kwa upendo nimeona nimsaidie maana namuonea huruma kule kutapika kila akiwa jikoni. na wakati mwingine hata mm nikiwa napika na yeye akaja jikoni akitoka basi anaenda kutapika, au ukipika chakula namna ambayo yeye hajapenda atakua ukitoe mezani..
yaani hata nyama akiiona anakwambia toa kanipikie dagaa, asee napata tabu sana, wanaume wenzangu njooni hapa mseme ukweli kwenu hua ikoje hii kitu?
Nimemwambia ajiandae tukamsalimie mama mzazi nyumbani ili nikaone atakavokua akiwa nyumbani akiendelea na tabia hio basi nitaona haniigizii..
thou nikiri nampenda sana na siwez ajiri house girl at this moment na wala akijifungua sitaki house girl kwangu.
 
Ndo iko hivyo mkuu!
Vumilia kidogo tuu miezi tisa sio mingi!

Akijifungua itabidi uombe likizo bila malipo, sio kwa misimamo hiyo!
 
Vp kufua, kuosha vyombo, usafi kwa ujumla anafanya nani?
 
Huzijui mimba ww, kuna wengine hapa hata mood ya kuongea na Mr ilikuwa haipo.
Unakuwa km umepata ububu fln hv, kooni unakabwa kbs
 
k
Vp kufua, kuosha vyombo, usafi kwa ujumla anafanya nani?
kuosha vyombo anaosha akimaliza anatapika, hio hainiumizi kama kutapika kabla ya kula, vyombo huoshwa baadae sana angalau chakula kikishameng'enywa
 
Wapendwa habari, nimeoa na bahati nzuri mke ni mjamzito kwa sasa, tatizo ni kuwa toka kawa mjamzito amekuwa kila akiingia jikoni anatapika, hivo ikabidi nimuweke sub, kidume nikaanza kuingia jikoni, kila nikitoka kazini, sasa hii hali imenipa taabu maana naona wakati mwingine ananiigizia, sisi wasukuma kwetu mwanaume haingii jikoni hata iweje, lakini kwa upendo nimeona nimsaidie maana namuonea huruma kule kutapika kila akiwa jikoni. na wakati mwingine hata mm nikiwa napika na yeye akaja jikoni akitoka basi anaenda kutapika, au ukipika chakula namna ambayo yeye hajapenda atakua ukitoe mezani..
yaani hata nyama akiiona anakwambia toa kanipikie dagaa, asee napata tabu sana, wanaume wenzangu njooni hapa mseme ukweli kwenu hua ikoje hii kitu?
Nimemwambia ajiandae tukamsalimie mama mzazi nyumbani ili nikaone atakavokua akiwa nyumbani akiendelea na tabia hio basi nitaona haniigizii..
thou nikiri nampenda sana na siwez ajiri house girl at this moment na wala akijifungua sitaki house girl kwangu.
Hili swala ni wanawake wa kibongo tu?
 
sio kubadilika jinsia but nachoka
Km ulikuwa hujui uchovu wa mimba ni mara 10 ya uchovu wako huo wa kawaida.
Na jinsi mtu unavyokuwa na malaria ile hali ya mate machungu, kichefuchefu, hamu ya kula hakuna basi ujue na kwenye mimba ndio hivyo hivyo.
Tena bora malaria utameza dawa utapona, lkn mimba haina kumeza dawa. Ni kupambana tu hali yako.
 
Wanatusumbua sababu tumewadekeza kwa hilo yaani unalala usiku mtu anakuamsha ukamtafutie embe so uzwazwa
ndio maana sielewi hii kitu naogopa kutenda ubaya nisijeonekana namuonea
 
Sidhani kama anaweza kuwa ana-fake kutapika kila wakati mkuu!
 
MWANAMKE akiwa na mimba mi huskia;"mimba yangu imekataa harufu ya kitunguu, ooh mara imekataa pilau, Mara sitaki kumwona yule oo mimba yangu imekataa nyama, ooooo ooooo blah blah blah.... "
Swali langu ni, mbona sijawahi skia mimba IMEKATAA PESA??? 😂😂😂😂😂😂😂
 
Beki tatu akipata mimba au mtu akiyepatia mimba kwao huwa hawasumbui
 
Sidhani kama anaweza kuwa ana-fake kutapika kila wakati mkuu!
Mkuu co rahis kutapika lkn kuna kitu najiuliza mbona akiwa hana mume wala mama wa kumdekeza anakuwa mzima kabisa hana kuumwa wala nini
 
Anadeka huyo kwa sababu ni mimba ya kwanza na anakupima msimamo wako,ingawa mimba huwa zinasumbua lakini inategemea mtu na mtu anaichukuliaje.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom