Mabinti jifunzeni siri hii nanyi mtafanikiwa sana

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,650
Wakuu, Amani kwenu nyote.
Iko siri kubwa ya maisha ambayo kwa kiasi kikubwa huamua hatma ya mtoto wa kike. Ili kuifahamu tumtazame kwanza kijana mume:

Mwanamume
Kijana mume huanzia chini katika thamani ya maisha ndipo anapanda juu. Sababu kubwa ni kuwa mwanamume huzaliwa akiwa HANA KUSUDI moyoni mwake, ndio maana ni wajibu wake kulitafuta kusudi la yeye kuzaliwa. Hapa ndipo ilipo siri ya kufanikiwa kijana kwa sababu kama akizingatia sauti ya ndani kumwonyesha ni ipi njia aifuate, hufanya mambo yaliyo "damuni." Bahati mbaya vijana wengi wanaishi kwa kutumikia kusudi la wengine, hawaishi kwa kusudi lao wenyewe. Tumegeuka kizazi cha "misukule" tukiamliwa tuweje, tuhusianaje, tuishije.

Turudi kwenye mada: kijana akizaliwa huwa hana kitu, anaanza kitafuta. Katika kipindi hiki ndipo hukutana na kauli kama "sio type yangu" kutoka kwa binti ambaye wako rika moja. Ni kipindi ambacho kinaweka wazi jinsi mwanamke alivyowekewa kusudi lake bila kujua.

Kijana afikapo umri wa miaka 25 na kuendelea huwa amajiwekea lengo na mafanikio yameanza kumjia. Hapo hugeuka "hot cake" kwa mabinti ambao hapo awali walimwona kuwa si kitu. Sasa kadri kijana anavyozidi kufanikiwa ndivyo anavyozidi kujiweka sokoni. Umri hauna maana tena kwani ni namba tu, sura wala sio habari tena kwani mwanamume ana sura moja tu, mafanikio. Hata akitimia mika 40, mwanamume ataendelea kuitwa "baby" sio kwa sababu kweli ni kijana bali kwa sababu umri wake hupimwa kwa mafanikio yake.

Mwanamke
Binti anapovunja ungo tu, vichuchu vikamsimama, hipsi zikaji-align vema na matako, miguu ikachongoka nk moja kwa moja huanzia juu katika thamani. Binti huanzia juu kwa maana kwamba ndicho kipindi ambacho uzuri wake halisi huthibitika mbele ya jamii. Ni kipindi ambacho hata wazazi walio wagonjwa wa akili hushindwa kujizuia na kuwalala watoto wao wa kuwazaa. Ni kipindi ambacho hata kama binti atavaa kinguo cha kushindia tu wanaume wakware hupata taabu kwa sababu uzuri huficha mavazi.

Sasa kipindi hiki ndicho jehanamu ya binti. Kwa sababu ya umaarufu feki utokanao na jamii iliyoharibika akili kumweka juu binti huyu, mabinti wengi wamepoteza mwelekeo. Nimesema tangu mwanzo binti analo kusudi la kuzaliwa kwake, God given. Kusudi la mwanamke ni kuzaa na kulea. Mwanamke hana haja ya kutafuta kusudi la kuwepo kwake kwani lipo tayari tangu kuumbwa kwake. Ni jukumu la mwanamume kujibidiisha kutambua Kusudi lake.

Nilishangaa kusikia yuko mwanamke mashuhuri amemwacha mumewe ili akatumikie kusudi aliloitiwa!! Hiyo ni roho ya ukahaba.

Sasa mwanamke huanzia juu, lakini afikapo miaka 30 tayari taa nyekundu huwaka. Thamani yake hushuka kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba anaanza kuhangaika kurekebisha sura kwa namna mbalimbali. Anatafuta kukubalika kwamba bado yuko juu, lakini jamii tayari inao vibinti vichanga vilivyoingia hapo kuziba pengo.

Ni kipindi hiki mwanamke huyu ambaye graph yake inashuka hukutana na mwanamume ambaye graph yake inapanda sokoni. Lakini ajabu ni kuwa mwanamume huyu hataki tena kumtazama mwanamke huyu anayemhesabu kuwa "ametumika" na ni mzee. Kijana tayari ana mafanikio ya kuweza kumwingiza sokoni kujitwalia kibinti kibichi, kwa nini ahangaike na mwanamke anayetoka sokoni? Mwanamke akivuka miaka 35 huwa "game over" na hapo huwa radhi hata kuolewa na house boy alimradi aitwe mke. Mwanamume hata akipindukia miaka 45 huwa "game on" mradi ana mafanikio ya kuonyesha sokoni.

Hii inajibu swali muhimu maishani:kwa nini mabinti wanapenda kutoka na watu wazima? Sababu ni moja tu, jamii inamweka juu, binti hujawa na kiburi na kujisahau na hivyo kuutumia ujana wake kuwastarehesha "wazee" kwa sababu tayari wana mafanikio. Hawa ni wazee ambao tayari wana malengo yao na wamesha jipanga kuwa na familia bora, bali huvitumia vibinti hivi ama kwa kujistarehesha, ama kwa matambiko!! Maisha yana siri nzito!!

Sasa binti aweje? Ni vema sana kwa binti kuishi misha ya hofu ya Mungu. Neno hili laweza kuonekana ni upuuzi, lakini mwishowe hudhihirisha ukweli wake. Mwanamke mwenye hofu ya Mungu hawezi kamwe kuenenda na mfumo wa jamii. Atatambua kuwa yeye ni binti tu japo jamii itajaribu kumwaminisha kuwa anaimiliki dunia tangu kuzaliwa kwake. Jamii itajaribu kumjaza ujinga kuwa yeye ni zaidi ya wanawake wengine wote, asijue hata hao anaowadharau siku moja walikuwa juu hata zaidi yake.

Ndiposa ni vema kuchunga unapata wapi mambo unayoulisha moyo wako. Binti kujikita kutazama channel za ngono kwenye TV zilizopoteza mwelekeo ni kosa ambalo utakuja lijutia baadaye. Tasnia kama bongo movie ni tasnia ya ngono na ubunifu ni zero. Kama unabisha tazama mabinti waigizaji maisha yao, kwa kiasi kikubwa utakuta maajabu. Sasa hawa ndio wanaotoa mafunzo kwa mabinti waishije!! Ziko channel nyingi tu ambazo zinaingia kwenye kundi la ngono lakini si vema nizitaje hapa kwa sababu za kibiashara, wana kundi la wajinga ambao huwapatia mapato yao. Mind game.

Jambo la kukumbuka daima:
Binti huanza kwa thamani ya juu maishani na thamani yake hutoweka ghafla, wakati kijana mume huanza chini na kupanda taratibu katika thamani. Ndio maana nimeona nikazie kwa watoto wa kike. Wanateswa sana siku za usoni kwa makosa ya ujanani. Maisha ni katili na mara nyingi hawapati nafasi nyingine kurekebisha hali tofauti na wanaume.

Wapo ambao hawafuati mfumo huu lakini ni wachache mno. Mfano wapo mabinti wanaotumia ujana wao kujijenga na hata kupata pesa, ajira n.k. Hawa ni wachache na tena wengi wao hupata waume ambao ni matom boy. Vijana wanaotafuta kulelewa!! Pia wako vijana ambao wametoka maisha bora na nyota zao kung'aa kungali asubuhi, lakini hawa nao wana majuto yao baadaye.

---------------------------------------------------------------
---------------------------------------------------------------

UFAFANUZI ZAIDI

Mambo haya husemwa kwa mfano:
Mara nyingi kijana anayeanza maisha akipata utajiri wa ghafla asipokuwa na usimamizi mzuri (washauri)utajiri wote hutoweka kwa kasi ya ajabu. Hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko kwanza. Hii ni kwa sababu moyoni mwake hajawa na hazina ya ujuzi wa matumizi sahihi ya utajiri huo wa mali. Hivyo huongozwa kwa kuona kuliko kutoka rohoni. Huongozwa na mambo "mazuri" ya dunia kama ulevi, uzinzi, madawa ya kulevya nk.

Kwa kuwa moyo wake uko tupu, mambo haya huujaza na kuutiisha moyo. Ndio maana biashara nyingi zinazoanza juu moja kwa moja hufa kibudu, isipokuwa kama wataajiri wenye ujuzi wazisimamie.

Kwa lugha nyingine, biashara inayoanzia chini kabisa ina nafasi kubwa ya kustawi. Katika kipindi chote cha kupanda na kushuka (trial and errors) hujaza moyoni elimu sahihi kwa ustawi wa biashara. Safari huonekana kuwa ngumu na ndefu mno, lakini mwisho wake ni mtamu kama asali. Safari hii huhitaji kujinyima mambo mengi ya anasa ambayo jamii huyahesabu kuwa ndio kilele cha kusudi la maisha. Mtu atendaye haya "hakika anahesabika amekufa duniani" ingawa anaishi.

Ndipo tuelewe ni kwa nini mabenki hutoa kwa urahisi mikopo kwenye biashara zinazoendelea "hata kama ni ndogo" kuliko zinazotarajia kuanza baada ya mkopo!! Kijana aliyehitimu chuo kikuu akiomba mkopo benki itaangalia waliomzunguka, menejimenti. Mkopo utatolewa kwa imani kwamba waliomzunguka wana ujuzi wa kutosha kuweza kuzalisha pesa zile, sio kwa sababu ya degree ya kijana huyu.

Sasa mtazame mama ntilie, mwenye kujitambua, ana banda lake la biashara, huweka pesa zake kwenye benki mojawapo. Miezi michache baadaye mama huyu huanza kupata "usumbufu" kutoka mawakala wa benki kumshawishi achukue mkopo ili kuiboresha biashara yake. Tena wako ambao humpatia mbinu zaidi za namna ya kukuza na kuiendeleza biashara yake!! Umeona tofauti!!? Watu wa kale walisema pesa hufuata mkondo, sisi tukatafsiri kijuujuu tu. Tukajidanganya kuwa pesa huwafuata wenye nazo, SI KWELI. Pesa hufuata njia yake, yaani kama maji yafuatavyo mkondo. Sasa ukijiweka kwenye mkondo wa maji lazima upitiwe na mafuriko, ndivyo ilivyo kwa pesa. Jiweke kwenye njia yake, itakufuata.

Turudi kwenye mada:
Mabinti huanza kama kijana aliyepata pesa bila kuwa na maandalizi. Akili zao bado hazijawa na uelewa kuhusu tamu na chungu ya maisha. Ni kipindi ambacho wanachagua mambo ya kuujaza moyo, mambo ambayo ndio yatakuwa mwongozo wa maisha yao siku za usoni. Sasa kwa kuwa bado mioyo yao ni mitupu, ni rahisi mno kwao kuongozwa kutoka nje, kwa kuwatazama wanawake wenye mifano mibaya, na pia kwa kusikiliza ushawishi wa wanaume walioharibika akili wakitafuta waule ujana wao. Akiruhusu haya, maisha yake huanzia juu kwa kutumikia anasa huku akishushwa chini kwa kasi ya ajabu mno!! Hiki ni kipindi ambacho wazazi wenye busara huchukua uongozi wa binti huyu. Wazazi ama walezi hufanya maamuzi kwa niaba yake, huku binti akijifunza namna ya kufanya maamuzi sahihi kwa kuwatazama wao.

Kijana mume yeye huanzia chini. Hujifunza kwa wazazi ama walezi jinsi ya kuchagua na kusimamia lengo lake. Kisha hujibidiisha kulifikia lengo hilo huku akikwepa milima na mabonde. Hujipatia taratibu ujuzi ambao baadaye utakuwa wenye manufaa makubwa kwake na jamii nzima kwa ujumla. Kijana huyu hufananishwa na mfanyabiashara aliyejiweka kwenye mkondo wa pesa hata mafuriko yanapotokea humkumba. Ni kijana ambaye baada ya dhiki na mateso mengi hukubalika na kuhesabiwa kuwa shujaa na jamii nzima kwa hiyo huchukua chochote atakacho, haombi!!

Funzo muhimu:

>> Kile unachokijaza moyoni ndicho kitakachokuongoza siku za usoni. Kijana anaongozwa toka nje (anasa n.k.) kama hakufundishwa jinsi ya kujizuia. Maongozi haya ni kwa sababu moyo uko tupu unatafuta namna ya kujaza gap. Binti ana nafasi kubwa kuingia kwenye huu mtego kwa sababu kiasili huanzia juu daima. Kijana mume atategemea mazingira yake, mfano kama anatoka familia tajiri n.k.

>> Kumzuia mtoto wa kike awe chini sio kutaka aishi kama mwanamume, bali ni kuruhusu UFAHAMU wake ukomae ili kwamba aweze kupambanua mema na mabaya. Awapo hivyo hugeuka kuwa bidhaa adimu sokoni.

>> Wanaonishambulia hakika wanajifanya vipofu, wanaona lakini wamekataa kuukubali ukweli. Hai nai wana sehemu yao katika jamii!!

Samcezar, Femur, Boeing 757, I LOVE U
Azarel, Prince Mhando

Wanaume walioharibika akili

Jinsi vijana wa sasa wanavyopoteza majira yao

Jinsi wazazi tunavyowaharibu watoto wetu wenyewe

------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------

Dah huyu Jamaa, Kazi ipo!

Naheshimu sana unachosimamia. Pia naheshimu sana unachoamini. Lakini pamoja na hadithi zako na marejeo ya neno unalosimamia, embu jaribu kutafakari vitu vifuatavyo;

Unaamini kuwa Ndoa ni Jambo la lazima, sawa. Na unaonekana kuwa ni muumini wa Christianity. Kwa navyofahamu katika imani yako hairuhusiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja. Lakini pia katika age level yoyote kwa hapa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani, idadi ya wanawake huwa ni kubwa sana kulinganisha na idadi ya wanaume. So even if kila mwanaume akioa mke mmoja, still kuna uwezekano wa idadi ya wanawake kadhaa kukosa wanaume wa kuwaoa. Je hao unawazungumziaje??

Iko wapi hadithi hapo? Jadili mada kuliko kuweka kejeli. Hapo naongelea maisha na yamewalenga mabinti wanaoinukia.

Kuhusu suala la idadi kwangu hakuna mashiko, ukiwa na binti yako humfunzi kwamba kuna idadi kubwa ya wanawake hivyo unaweza usiolewe. Mzazi mwema humlea binti yake kana kwamba atapata mume.

Pili ni wazi kuwa si kila mwanamke amezaliwa kwa ajili ya kuwa mke. Wako waliozaliwa kwa ajili ya kuwa makahaba, kuishi peke yao nk. Mimi naongelea MAFUNZO KWA MABINTI ili walio na hekima ya kuwa wake, wataisikia sauti hii. Sasa hao wasio na matarajio ya kuwa wake wanaweza kukusikiliza wewe pia. Wapo na wadada wengine hapo juu wametoa matusi mengi sana wakivutia upande wao.

Unahimiza kuwa mtoto wa kike akilelewa vizuri akawa na sifa njema basi inamrahisishia kuja kuolewa kwa sababu sifa njema kwake zinamuongezea thamani kwa Mwanaume. Sawa .. lakini tafakari;

Unadhani wanawake wote ambao hawajaolewa au single mothers ni kwa sababu wamelelewa vibaya? Au ni kwa sababu wana sifa mbaya? Vipi kuhusu sifa mbaya na tabia chafu za wanaume wanaowarubuni wanawake wenye tabia nzuri kwa manufaa yao binafsi? Sijaona ukilizungumzia hili..!!

1. Si kweli kwamba wanawake wote ambao hawajaolewa wana sifa mbaya, ama single mothers wote walikuwa na tabia mbaya. Hii ni very poor way of reasoning . Ni sawa na kusema "ni kweli kwamba kila mwanamke aliyeolewa ana sifa nzuri. Please tusilete fallacy tukapotosha watu. Zingatia nimesema ana nafasi kubwa ya kuja kuolewa kulinganisha na hao unaowapigania.

Lakini pia, ni kwa vipi tuwashauri vijana wajibidiishe katika kusoma ili waje kuishi kwa raha mbeleni wakati kuna wasomi chungu nzima wanazidiwa hata na mama ntilie? Kwa logic yako utataka tusiwakazanie watoto wetu kufanya bidii kwenye masomo kwani wanaweza kupoteza muda bure, heri tuwatume kuuza pipi na maji barabarani watuletee vijisenti!! Amua mwenyewe.

2. Kuhusu hao wanaume - binti akilelewa kwenye maadili ana nafasi kubwa ya kuwaepuka wanaorubuni, huo hasa ndio muktadha wa mada hii. Nashindwa kuelewa umepotea wapi au unatetea nini hasa. Mada hii imeongelea fika madhara ya kuwasikiliza wanaume hao baradhuli ili binti avuke ujana wake salama ila wewe unapinga huku ukikubali.

Umeshawahi kutafakari kuwa waharibifu wakubwa kwenye mahusiano huwa ni sisi wanaume? Most women were truly in love and pretty ready to get married with their first Men, but guess what happened? Men screwed up like we always do!! Saivi kibao kimeanza kugeuka, na sisi tunaumizwa na hao wanawake tuliowafundisha unyang'au then you came up here with maadili, Damn, Come On! Stop playing around, sisi ndio chanzo cha haya yote.

Are you effeminate!? Now you just came clean. Ni kwa vipi wanaume ni chanzo cha wanawake kuharibika? That's very poor reasoning. Ngoja nikusaidie neno:

Uzi huu umelenga mabinti na "wazazi" wao. Anayeharibu maadili ya mtoto si kijana wanayekutana beach, ama mzee anayevizia vitoto vidogo. Mharibifu namba moja ni WAZAZI. Huu utamaduni mpya wa baba mfanyakazi na mama mfanyakazi ndio matokeo yake hayo. Unawezaje kuzaa watoto na kuwa dump kwa house girl? Nani anayewalea watoto na kuhakiki kila hatua zao wanapotoka nyumbani? Familia zetu zimegeuka kama GUEST HOUSES, watu wanakutana usiku wanajamiiana, asubuhi kila mmoja anashika njia zake, tuko bize. Watoto ambao ndio MATUNDA ya ndoa tumewatupa, hatuwajali tena. Tumeajiri vitoto vyenzao tunaviita vi-house girl ili viwafundishe malezi na adabu njema. Hivyo vibinti ambavyo vimewashinda wa kwao kwa tabia mbovu wakaamua kuvisukuma "utumwani" kwa jina kifichi "house girl" ili vikajifunze adabu na uhalisia wa maisha labda vitabadilika. Vikifika majumbani mwetu tunavikabidhi jukumu kubwa zaidi la ndoa, malezi ya watoto, utadhani vimetoka chuo cha malezi ya familia. Yaana tumepoteza hata maana ya ndoa!!

Ukimkuta baba ambaye anaelewa ndoa ni nini, house girl anayeonyesha upendo mkubwa kwa watoto na kuwalea kwa uangalifu hupendwa na baba wa mji. Mwishowe hujikuta akiishia kitandani kwa sababu kaugusa moyo wa baba. Sasa kama unatarajia hose girl ndio amfundishe mwanao kutokimbilia mabinti hovyo ama kutodanganywa na mashuga dadi, umepotea mno. Utanyoosha vodole sana ili wanawake humu wakusifie kwa kuwaunga mkono, lakini wenye hekima watagundua huo mtego!!

Nisiandike sana, lakini kama unataka kutetea unachoamini. Basi gusia pande zote mbili. Sifa Njema ziwe kwa wanawake na wanaume PIA.

At the end of the day, huyo Mwanamke hata awe na sifa njema kiasi gani, kama anazungukwa na wanaume wapuuzi, ataishia kuwa kwenye mahusiano ya kipuuzi tu.

All Love.

Sitafuti sifa, nasimamia nachokiamini. Nakushauri andika uzi unaohusu wanaume tutakusikiliza. Hitimisho lako limedhihirisha mtazamo wako, nakushauri soma uzi humu unaitwa wanaume walioharibika akili. Unaweza kupata mambo mawili matatu. Huko uliko umepotea.

Wanaume walioharibika akili

Jinsi wazazi tunavyowaharibu watoto wetu wenyewe

Jinsi vijana wa sasa wanavyopoteza majira yao
 
Hii nadharia inarefect ukweli wa maisha. Ni kweli prime ya mwanamke huanza akiwa mdogo na decline huanza anavyoanza kuingia age ya utu uzima. Kwa wanaume decline huanza wakiwa wadogo na huelekea prime yao wanavyokuwa watu wazima.
Maisha ukiamua...yanaweza yakawa tofauti..hayana formula moja muda wote

If this theory was true basi mabinti wabichi wote wasingevuka 25 yrs bila wenza...si ndo wabichi wako sokoni?


Usisahau hao walio 30 na 35 leo walikua 25 at some point.
 
Maisha ukiamua...yanaweza yakawa tofauti..hayana formula moja muda wote

If this theory was true basi mabinti wabichi wote wasingevuka 25 yrs bila wenza...si ndo wabichi wako sokoni?


Usisahau hao walio 30 na 35 leo walikua 25 at some point.
So unataka kusema mabinti wote wanafanana mienendo ya tabia au nikueleweje mpenzi?!
 
Unamjua Meghan Markle? Ameolewa na nani na akiwa na umri gani?.
Usitumie mfano wa m'moja kuwakilisha wengi utachemka! Kilichomkuta huyo dada kimezungukwa na hali zisizo za kawaida nyingi kiasi kwamba its enough kusema, Megan amebahatisha.....

But usikwepe ukweli kinachotokea mtaank unaona lakini.....
 
Ehee ur coming now...hawafanani mienendo...life cant treat them the same...NEVER
So unataka kunambia binti ambaye amejitunza hadi miaka 25 na kuendelea akawa na bikra ya yake ni sawa na binti ambaye ameanza kuliwa akiwa na miaka 17 hadi anafika umri wa miaka 30 anamsururu wa boyfriends sijui wangapi....hawa hawawezi kuwa na mwisho unaofanana.
 
Back
Top Bottom