Hii kitu hatari jamani... Tujitahidi kuacha...

Hii kitu hatari jamani... Tujitahidi kuacha...

Watu wana zini mpaka ukipishana nao wananuka ngonongono ptuuuuuuuuu!!! Unzinzi umewajaa shenzy kabisa!!
 
kizazi cha nyoka kabisa hao,,,,,,mijitu na ndoa zao bado yanaenda kufakamiana mxuuuuuuuuuuuuuuuu

Sio hao tu Asnam.... mambo ya game za nje siku hizi yamekuwa kama kawaida, ndo maana inabidi tujitahidi sana kupunguza kama sio kuacha kabisa...
 
Nadhani huyo dada alikuwa na kimuhe muhe sana kwa ajili ya kutaka kumuonesha ufundi huyo rafiki yako. Akajikuta yuko under high pressure na kufikia kupoteza faham...ni mambo ya kawaida hasa mtu anapokuwa under high pressure plus strees kwa kuwa walikuwa wanafanya usasiliti so yakamkuta hayo!

mambo ya kukamia mechi mabaya sana..kwa uungwana unasema tu game yangu utaiona siku tuko uwanjani! Mambo ya sijui naenda round kumi mara sijui unakata kama feni ni ujinga tu na ndo inapelekea majanga hasa show inapokuwa chini ya kiwando ulichojitapa nacho.

BTW, Mleta mada umemwaga full details hapa kiasi kwamba hata wahusika wenyewe kama ni member hapa lazma imewatouch...siku nyingine jamaa hatakusimulia tena. USINZI NOMAAA

Mkuu kama ulijua vile, maana jamaa kanipigia punde anacheka eti niemuanika JF... Nikamwambia as lo as sijamtaja jina, sidhani kama iko shida...
 
Huyo jamaa kweli kapinda sijui kama ataacha ni mpaka yamkute zaidi ya hayo. Wanandoa wasio waamninifu waache UZINZI haufai laweza kukuta lolote hata kupoteza maisha sijui utakua mgeni wa nani huko.

Ndo maana inahitaji commitment ya hali ya juu na maombi, maana mtu akishazoea hii kitu kuacha noma... it is so addictive!!!
 
"Best" yangu hakuonekana kwenye kijiwe (baa) cha mpira Jumamosi iliyopita, kama nilivyotegemea. Nilipompigia simu akaniambia kuna 'kazi' anafanya jioni ile, muda si mrefu angeni-join. Kwa kuwa namuelewa, aliposema 'kazi' nilijua anamaanisha nini, kiufupi alikuwa anaisaliti ndoa yake somewhere. Sikushangaa kwa sababu nimemzoea...


Takribani masaa mawili badaye kaja, wakati huo mechi ya Man U na WBA ikifikia ukingoni. Kwa kuwa yeye ni mpinzani mkubwa wa Man U na tena timu yake ilitokea kushinda muda mfupi uliokuwa umepita, nilimtarajia kabisa angekuwa na furaha na kelele kibao... Lakini hali ilikuwa tofauti, kwani alipokaa, ingawa macho yalikuwa kideoni, lakini niliona kabisa akili yake ilizama kwenye dimbwi la mawazo!!!

"Vipi Mzee, swalama huko?"... nikamuuliza... Mwanzoni alikwepakwepa lakini baadaye akanipa full mkanda...
Anasema jioni ile alikuwa anaiba na demu ambaye zamani alikuwa demu wake lakini wakaja kupotezana. Ingawa walikuja kukutana miaka ya karibuni, hawakuthubutu kugusia mambo ya mapenzi kwa sababu kwanza, kila mmoja alikuwa na ndoa, na pili zamani hizo walipokuwa kwenye mapenzi ya kiuanafunzi, hawakuwahi kuduu... hivyo hakukuwa na kitu wanakimiss kimapenzi baina yao kiviile...
Hata hivyo shetani ni shetani tu... baada ya kuchat hapa na pale, wakajikuta wamekubaliana wakaonje kile 'walichotunziana' zamani. Hivyo, hiyo Jumamosi ndiyo ilikuwa siku ya siku

Sasa stori yenyewe...
Jamaa anasema yaliyomkuta humo ndani siku hiyo yamemfanya awaze sana huku akimshukuru Mungu wake kumnusuru na balaa. Anasema walianza tu mdogo mdogo na kwa kuwa kwenye kuchat before kila mmoja alikuwa anajisifiaga kuwa yuko fiti, basi hapo ilikuwa kama wanataka kuonyeshana ufundi. Jamaa alikuwa anasoma mchezo, akijitahidi kwanza demu achoke flani, ndipo aanza 'kumpelekesha'... Mapema tu demu aliomba wabadili staili ili awe juu, jamaa akamwambia hakuna shida, panda. Ndani ya dakika ambazo hazikuzidi 5, jamaa anasema aliona demu akihema kwa kasi sana, akadhani ndo anakaribia 'kibo', hivyo kimoyomoyo akajisifu kuwa mshindi, maana wakati ule yeye ndo alikuwa kwanza baado... akajisemea kuwa baada ya hapo angepiga kazi hadi demu aduwae...
Ila jamaa anasema demu ghafla alistopisha move alizokuwa anafanya, akajidondosha kifuani pake, kisha akajidondosha pembeni. Wakati jamaa anaanza kushangaa, demu akasema kwa sauti ya mbali "Nipepee, moyo unaenda mbio"... Jamaa akataharuki, demu akawa anasema kwa sauti ya mbaali... 'moyo'.. moyo... alafu baadae akawa kimya. Demu alikuwa anatiririka jasho vibaya na alipolala paliloa...
Jamaa kwa kuchanganyikiwa, akakurupuka akitaka kukimbia nje, alipofika mlangoni akakumbuka hajavaa, akarui kuvaa, akapata wazo ampepee kidogo akafanya hivyo na nguo zake. Hata hivyo akaona haina maana kwani mle ndani kulikuwa na baridi kali ya AC.
Alipomaliza kuvaa, huku demu akiendelea kutweta vibaya, jamaa akataka tena kutoka, lakini alipofika mlangoni akaona atakuwa ameacha ushahidi, akarudi akachukua simu ya demu (maana waliwasiliana kwa sms kabla). Hata hivyo alipotaka kutoka akaona ni upuuzi tu maana isingekuwa kazi ngumu kugundua ni yeye alikuwa nae, ikizingatiwa details za mawasiliano zingepatikana huko mitandaoni, na funger prints alizoacha mle ndani ni za kutosha, akarudi.
Baada ya kama dakika 20, demu alitulia, akarudiwa na nguvu akaweza kujigeuza na akawa anaongea kidogo kidogo... baadae akapata nguvu zaidi... Hata hivyo jamaa alinichekesha kwani anasema pale walikubaliana gemu iahirishwe, lakini walipoenda bafuni kuoga, mizuka ilimrudia akajikuta akimshawishi demu wakamaliza mle mle...

Jamaa aliwaza mambo mengi sana... mke wake, mme wa yule dada, kazi yake, jela, fedheha, umasikini nk... Tulishauriana mengi sana, kubwa ni kuwa haya mambo ni hatari jamani, kwa ambao hawajaacha, wajitahidi waache...

Mkuu Tuko , nakusalimu, Uchunguzi wangu binafsi unasema kuwa, huyu rafiki wako ndio wewe. Pole na Mkasa uliokukuta!
 
Last edited by a moderator:
Kwa hali hiyo ya utata wa huo demu lakini jamaa bado akatamani kupiga tena mzigo? Kweli tunajitakia makubwa sana. Aise, akirudiwa nguvu na fahamu natoka nduki na inakuwa ni mwiko tena kumtafuta.
 
Kweli yatupasa kuishi katika maisha yaukamilifu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Aise hatari sana hii..magonjwa ya moyo na kisukari pia huwa ni chanzo..kama mtu. Ana presha na magonjwa ya moyo,.ngono ni hatari kwa maisha
 
Back
Top Bottom