Hii itakuwa nini jamani!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii itakuwa nini jamani!!!

Discussion in 'JF Doctor' started by 4X4byfar, Mar 3, 2012.

 1. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za leo wa ndungu;

  Nimekuwa nikikojoa mkojo naunapo karibia kuishia naumwa sana ukeni? Then baada ya ya kupangusa naona vijidamu kidogo kwenye tissue. Najisikia vibaridi jioni nakukosa hamu ya kula. Leo nisiku ya tatu kusikia hayo maumivu yalianza juzi jioni. Ila leo kutwa damu haijatoka imebakia maumivu tuu. Hospitali kwa mtaalamu mpaka j,3. Msaada plz nini hii jamani.
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  As unasubiri kwenda hospitali kupima damu na mengine kunywa maji mengi, una dalili zote za advanced urinal infection (I am not a Doctor lakini).
   
 3. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Inawezekana ni urinary tract Infection, STD au medication allergy. subiria jumatatu ukapate ka dozi kako for the time being tafuna ka kitunguu saumu tembe moja au mbili (sio kitunguu kizima) kwa siku (wanasemaga haka kakitunguu ni natural antibiotic) na avoid sex.

  N:B. Nina F ya baioloji form 4
   
 4. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Zote dalili ulizotaja hapo nafikiri utakuwa na urinary tract infection ambayo huenda ikawa ni simple cystitis au pyelonephritis kwa hiyo cha muhimu nenda hospitari ukachukue vipimo, pili hakikisha unatumia juice na chakula ambazo zina sukari kidogo kupunguza kuzaliana kwa bacteria . Tatu kunywa maji ya kutosha 8 glass ili kufurashi bacteria .Nne fanya mazoezi kuanzia dakika 30 siku tano kwa kila wiki moja . Avoid sex kama klorockwini alivokuelekeza wakati wa dose.
   
 5. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani asanteni sana sana tena sana, maana nilianza kupata ka presha kwa kuwa toka kuzaliwa sijawahi kupata damu kutoka kwenye mkojo. Kwa kweli hata hamu ya kula imepungua kwa sana tuu alafu vitu vya sukari hamu imekatika ghafla tuu. Ngoja ifike hio j3 nikapime mweee! Thanks once again kwa majibu yenu.
   
 6. k

  kamili JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Choo kidogo kuchanganyika na damu mwishoni yawezekana kuwa UTI, na kichocho.
   
 7. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tafuta systemic alkaliser. Ama mist potassium citrate au disodium citrate. Yonyesha hunywi maji ya kutosha. Umepata a case of bladder calculii na UTI. Kuna vijiwe vidogo unavikojoa na vinakupa maumivu na vina sababisha infection.

  Nunuwa CITAL LIQUID na utumie 15mls kwenye glasi ya maji x 3 kwa siku. Hii ni best. GOOD LUCK.
   
 8. korino

  korino JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 492
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  le dada angu! kesho ukamwone dr. ila inaelekea hunywi maji yakutosha ww! kunywa maji mengi atlist hata lita 2 na nusus per day
   
 9. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wapendwa waliosema sinywi maji ni kweli kabisa kwa siku naweza kupitiliza bila kunywa maji kabisa! Yani ndivyo nilivyo na sina kiu kabisa. Ila kwa sasa nimejifunza somo zuri sana. Mnajua nini kabla ya haya matatizo kunipata nilianza kunywa maji ya vuguvugu yaliochangwanywa na asali ya 1tbs(hii receipt niliipata humu jf) kuwa inasaidia nadhani ku detoxify mwili! sasa baada ya kama siku 5 hivi ndo nikaanza kujisikia hivyo. Kwa uoga nikaachana na hio receipt kabisa. Sasa sijui ndo iliofanya hayo mawe (kama doctorz) alivyosema? Ila nimeweka appointment na nimepewa mda wa kuchekiwa, though hata wao hospitali wamesema ntakuwa na Urinary infection.

  Jamani nawashukuru sana wana jf you made me feel good kwa umoja wenu kwa kweli, mbarikiwe sana wapendwa.
   
Loading...