Hii inaweza kumfanya mtoto ashindwe kuongea?

Habari wakuu,
Mvurugo wangu ni huu hapa...Hivi mfano ikatokea mtoto amefikisha umri wa mwaka mmoja toka kuzaliwa eneo fulani labda tuseme Dar (Ubungo) kisha ukamuamisha ukampeleka Mara(Majita) ndani ndani huko ambapo lugha wanayozungumza ni tofauti na ile ya Dar,nako huko akae mwaka mmoja.Baada ya hapo unamuamisha unampeleka Mbeya(Umalila) ndani ndani kabisa ambapo wanazungumza lugha yao nako huko akae mwaka mmoja.Baadae unampeleka Arusha(Umasaini) alafu akae miezi mitatu alafu unampeleka Dodoma(ndani ndani huko) n.k...
Je,kwa mvurugo huo mtoto anaweza kufika miaka 7 au zaidi hajui kuongea kwa sababu ya kumuhamishahamisha?
Siyo tu kuwa hatajua kusema ila hatajua chochote(growth restrictions) kwa sababu hatazoea chochote/yeyote,hatakuwa na furaha na atakata tamaa kujifunza. Hata watu atawaogopa na kuwachukia. Ushahidi ni pale unapobadilsha mlezi wa mtoto.
 
Huyo mtoto anasafiri na wazazi wake obviously wanaozungumza lugha moja, na huyo mtoto hatoki sana ndani kwa sababu ni mdogo, hivyo haina athari kwenye lugha maana atajifunza lugha ya baba na mama.
 
Huyo mtoto anasafiri na wazazi wake obviously wanaozungumza lugha moja, na huyo mtoto hatoki sana ndani kwa sababu ni mdogo, hivyo haina athari kwenye lugha maana atajifunza lugha ya baba na mama.
vipi kama kila anapotoka eneo moja hadi lingine anakua na mlezi mpya tofauti?
 
Back
Top Bottom