Bonny
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 13,369
- 30,009
ahaa wap na mkipewa pesa mtasikia mnaanza huyu ana kithothej natafuta mwenye mguududu?????? hata machizi wanayo pesa kwanza
ahaa wap na mkipewa pesa mtasikia mnaanza huyu ana kithothej natafuta mwenye mguududu?????? hata machizi wanayo pesa kwanza
Si vibaya lakini vilevile si sheria...
Wema haupaswi kuzidi uwezo...
Kama mwanamke huyo aliweza kuhudumiwa na hao wazazi wenye uwezo duni hadi kufikia umri huo, iweje baada ya kumpata mwanaume mtazamo huo ubadilike?
Kwa kuwa umetaja neno kusaidia, najua watambua kuwa msaada haulazimishwi wala kushurutishwa bali hutegemea utayari na uwezo wa mtoaji...
Mtu asipokusaidia hata kama ana taarifa hupaswi kumuhukumu...
Dalili ya mvua kuambatana na mawingu haina uhusiano wowote na walichosema wahenga, it's a scientific fact...
Hivi kujali katika mahusiano hupimwa na urefu au ufupi wa mkono pekee?
Si dalili mbaya na wala msaada si deni...
Mwanamke ambaye ana mawazo tegemezi haswa ya kiuchumi ni mzigo kwa mwanaume...
Si jambo jema maana wanayafanya hayo kabla ya wakati...ni kama dereva anayeovateki kwenye kona...
pesa my dear! dyudyu hata kama haitoshelezi neck massager zitasaidia in mange's voice! ni shidaaaaaa!
Blue G Kuna maswali mengi na logic nyingi ambazo zinapelekea mwanaume kuamua kumuhudumia mwanamke na sio tu kuwa kwenye mahusiano ndio iwe sababu ya kuhudumia. Nitakupa mfano mmoja, kama huyo mpenzi wangu ameniomba credit kwenye simu yake na nikamtumia lakini kwangu mimi anaishia kunibip au kunitumia please call me, do I have to do anything to her again? Sisemi sipigwi mizinga, napigwa sana tu but kama ni mizinga ya kipuuzi huwa sitoi na kama mwanamke anaona kwasababu sipigwi mizinga ya kipuuzi then sifai then na aende tu kwakweli.
Mi sjuagi wanapendaga nin hawa watu kwa kwel btn cash and ze dudu
Unachanganya habari kueleweka ngumu hivi mtoa mada umeoa au ni wale ambao ndo mnaanza mapenzi? Kwenye issue ya mke na mume hakuna hiyo kitu ya kupigana mizinga. Vibiriti ngoma ndo wanaopiga mizinga!
hapo kwenye red mkuusi vibaya lakini si sheria ni kweli ila kuna umuhimu wake katika kufanya hivyo,hata nyakati za kale yakobo alimfanyia babamkwe wake kazi kwa miaka mingi ili aweze kumpata raheli kama mke wake jambo ambalo lingefananishwa na msaada wa hali kuelekea baba na mke waka mtarajiwa pia.
ila tu imetokea binti kapata mume mwenye kujiweza asite kuomba msaada kwa kuchelea mtazamo wake kutiliwa shaka kuwa umebadilika na hofu ya maswali amelelewaje mpaka wakati huo?
kwani kuna mtu ambaye hapendi kusaidiwa?nafikiri hakuna ila tu watu hubaki bila msaada kwa kuwa hakuna aliyejitokeza kuwasadia lakini vipi akijitokeza?
katika hii thread yangu kamwe sijamshurutisha mwanaume amsaidie mwanamke,ila nimeonesha kuwa mwanaume hapaswai kulalamika kwa kuwa tu anaombwa msaada na mchumbake
au kuona jukumu la kumtunza mkewe kuwa ni kubwa sana kiasi cha kuanza kulalamika,au kutaka wagaane majukumu yakifedha nyumbani.
kwenye hivyo firebrick colour naomba tu nikwambie mkuu ukweli,hakuna mwanamke ambaye hapendi kutunzwa na mume wake awe na kazi asiwe nayo,kila mwanamke hujihisi anapendwa na kuthaminiwa ikiwa mume ataona kuitunza familia kutia ndani na mke wake kuwa ni jukumu lake na si vinginevyo,huo ndo ukweli mkuu na tamaa hiyo haimaanishi ni utegemezi ila ni taamaa ya asili ambayo nina amini asilimia kubwa ya wanawake wanayo kama wapo wasiokuwa nayo ni ndogo sana mkuu.
Blue G Mapenzi ni maelewano na kuaminiana, mnapoanza mahusiano mara nyingi huwa mnaulizana vitu mnavyovipenda na kuvichukia, mnaelezana kuhusu familia zenu na background zenu. Hii yote ni kuelezana ili kila mmoja amjue mwenzie kwa undani lakini kikubwa ni kutengeneza mazingira ya kuaminiana. Kama mazingira ya kuaminiana yatajengwa kuanzia awali then kama atakuja kuniambia chochote nitakuwa tayari kumsaidia kwa namna yoyote ile. Nitakupa mfano, niliwahi kuwa na mpenzi wangu mmoja ambaye pamoja na kuishi mikoa tofauti lakini nilikuwa na uhakika kwamba "this is my girlfriend" alikuwa akiniambia tatizo then linakuwa genuine na nilikuwa nikimwambia inakuwa genuine kwasababu tuliyajenga haya from the beginning. Lakini tatizo la mapenzi ya siku hizi ni ujanja ujanja mwingi sana kiasi kwamba hakuna anyemuaini mwenzie na hapo ndipo hata anapokuja mpenzi wako ana shida Fulani unahisi ni mizinga hata kama huenda ikawa shida genuine.umeongelea jambo hili so smartly na mfano ulioutoa nimeuelewa sana,ndo maana hata mimi pale mwishoni nilimalizia kwa kusema sirifai kwa madada walio magold digger nazungumzia mpenzi wako ambaye una future naye ana shida fulani ya pesa na labda anakuomba mara nyingi na hata wewe unajua kabisa kuwa kwao uwezo wao ni duni,tena wakati mwingine anaona aibu mpaka anakwambia naomba uniazime kiasi fulani cha pesa nitakurudhishia unafanyaje hapo mkuu?je utaona anakupiga mizinga kwa kuwa imekuwa ni kawaida yake kukuomba pesa?utalalamika kuwa anakupiga mizinga au amekugeuza baba yake?au unafanyaje mkuu M'Jr?japo as for me nashindwa kwa kweli kuomba omba napenda mtu anipe kitu yeye mwenyewe kwa kupenda lakini sasa kuna hali zinamlazimu mtu aombe hata kinyume na matakwa yake.
Mkuu sidhani kama Yakobo alikubali kutumika kwa nia ya kutoa msaada na wala alichokifanya huwezi kukifananisha na msaada...
Alichokifanya Yakobo ni kuonesha nia ya kwamba yule binti anayemuhitaji yu na thamani kwake na ndio maana laikubali kutumika...
Hilo halina utofauti na mahari itolewayo na mwanaume kwa nia ya kumfanya binti awe chini ya himaya yake, kwa kifupi Yakobo alikuwa anatimiza wajibu.
Nilidhani mjadala wetu umejikita kwenye suala la uchumba na upenzi na si ndoa....!!!
Ni ngumu kuwa na jibu la moja kwa moja kuwa watu wote wanapenda kusaidiwa, la hasha kusingelikuwa na maneno kama mchapakazi, hodari, jasiri n.k
Msaada mara nyingi una gharama zake, ni rahisi kuchekelea unapopata mtu wa kukusaidia lakini ujiulize kama kuna ulazima huo?
Ni ngumu kujua kuwa umetoa shurti karibu katika maelezo yako yote...
Kutumia tungo kama "hapaswi" maana yake unajaribu kutia ushawishi au shurti kwa kutumia tu lugha laini...
Kwa kifupi tayari unakuwa umeshachagua upande ambao kwao wajionesha kuwa u muumini wake...
Hili la mke sina kipingamizi nalo kwa kuwa ni sheria tena ni shurti kwa mume kumtunza mke na ndio maana ulikubali kumtoa toka himaya ya wazazi au walezi wake...
Once again utatoka nje ya context ambayo mimi na wewe tumekubaliana tujengee hoja...
Tokea awali nimeshajieleza kuwa sina shida na mahusiano ya kindoa maana hayo tayari ni mkataba...
Concern yangu kubwa ni haya mahusiano mengine ya kimapenzi ambayo hayana kibali chochote cha kindoa...
Blue G Mapenzi ni maelewano na kuaminiana, mnapoanza mahusiano mara nyingi huwa mnaulizana vitu mnavyovipenda na kuvichukia, mnaelezana kuhusu familia zenu na background zenu. Hii yote ni kuelezana ili kila mmoja amjue mwenzie kwa undani lakini kikubwa ni kutengeneza mazingira ya kuaminiana. Kama mazingira ya kuaminiana yatajengwa kuanzia awali then kama atakuja kuniambia chochote nitakuwa tayari kumsaidia kwa namna yoyote ile. Nitakupa mfano, niliwahi kuwa na mpenzi wangu mmoja ambaye pamoja na kuishi mikoa tofauti lakini nilikuwa na uhakika kwamba "this is my girlfriend" alikuwa akiniambia tatizo then linakuwa genuine na nilikuwa nikimwambia inakuwa genuine kwasababu tuliyajenga haya from the beginning. Lakini tatizo la mapenzi ya siku hizi ni ujanja ujanja mwingi sana kiasi kwamba hakuna anyemuaini mwenzie na hapo ndipo hata anapokuja mpenzi wako ana shida Fulani unahisi ni mizinga hata kama huenda ikawa shida genuine.
unaweza kunisaidia katika hilo mkuu?
Mwanaume pesa.... dushe mbwembwe tu... utasikia namkuna vizuri awezi niacha nani kasema nikipata wakunipa nakuacha ,
Mmmmmhh!! Hiyo kali
nmekuseoma mkuu inategemea zaid na status ya masisha na mahtaj zaid enheewanapendaga vyote mkuu kwani bado hujajuaga tu dudu wanapenda treat zako wanapenda pia kama tu na wewe unavyopenda kipochi manyoya na spoil zao nyingine nyingine upo hapo mkuu?