Hii inapendeza sana kwa wapenzi

Nilipomuongelea mama magufuli nilimuweka kwenye kundi la wanawake walioanzia chini na waume zao,unaweza usiuone mchango wake kwa muono wako kwasababu unataka kumlinganisha na mwingine lkn mchango wake anaujua mumewe. Kumbuka mke ni image ya mumewe kwahiyo michelle alikuwa image ya Obama, unapomsifia Michelle hauwezi ukaacha kumsifia Obama maana asingekuwa na Obama maybe asingekuwa Michelle tunaemfahamu.

Kuhusu wanawake wenye kipato kikubwa kuliko waume zao mie nawashuhudia wengi tu huku mitaani na maisha yanasonga vizuri tu.

Hao wanaotafuta waume kwa vigezo vya rangi hata wanaume wanachagua hivyo nashangaa kwanini umeegemea upande wa wanawake tu,maybe wanawake hawapaswi kuwa na choices bali anayekuja ye ajibebee tu, mtu anakuwa na yule aliyemridhia kama ambavyo michelle alimridhia obama maana alikidhi vigezo vyake.

Hii ya wanawake wa sasa kuangalia mwanaume ambae ana unafuu wa maisha ni kwakuwa maisha yamebadilika mpendwa,sio kama zamani mkikosa mboga utakwenda kuchuma hata kwenye shamba la jirani. hakuna anaependa shida ndio maana angalia hata thread za wanaume wanaotafuta wachumba utaona anahitaji alojiajiri au aloajiriwa,wengine mwenye elimu fulani,kwakuwa birds of the same feadhers flies together.

Vigezo vyako vinaweza visiwe vya yule, kwahiyo heshimu tu vigezo vya mwenzio. Hata wanaume wa sasa walio wengi hauwezi kuwalingalisha na baba/babu zetu kuna vingi wanakosa.

Itoshe kusema nyakati zimebadilika and alot hv changed, usitegemee mwanamke awe wa 50s wakati we ni wa 80s. Ila wanawake wema na wanaume wema still wapo wengi tu ni vile wewe unavyochanga karata zako kuwapata.
 
Hakuna kitu hapo alifanya usanii tu, inaonekana huwajui vizuri wazungu
Hebu wakati mwingine muwe positive jamani, mbona hamna jema. Au ndio ile mtu akiona kwake kunaungua basi anaamini na kwa wenzie ni vivyo hivyo na kama sio hivyo basi wanapretend!!!
 
[emoji3] [emoji3] hilarious comment
 

House of cards ntaanza kuiangalia week ijayo. Nmeshaiweka kwenye list
 
Mnafiki tu huyo analia na Mengi akiwaza jinsi alivyoikuta Libya na jinsi alivyoiacha, mauaji na ubaguzi wa waziwazi kwa wamarekani weusi kwanini chozi lisimtoke?
 
Hakika wametoka mbali Lizarazu.
Sana...

Vipi lakin mkuu we wako hamjatoka nae mbali?

mimi wangu nilikutana nae la nne baada ya mimi kurudia darasa na ndio alinisaidia sana kuvuka kwenda la tano, huwezi amini hadi leo hii niko nae.
 
Sana...

Vipi lakin mkuu we wako hamjatoka nae mbali?

mimi wangu nilikutana nae la nne baada ya mimi kurudia darasa na ndio alinisaidia sana kuvuka kwenda la tano, huwezi amini hadi leo hii niko nae.
Una bahati sana mkuu. Hapana ni hukuhuku juu.
 
Ni kweli. Kuna shida mahali. Wanaume wengi wanatembea peke yao kwenye ndoto zao.
Shida inaanzia kwa wazazi, ukimwambia ndoto anakusimanga na kukukatisha tamaa wengi wao wanasema dhahiri, wewe fulani huwezi labda uwe mwalimu,n.k huwezi kuwa raisi,n.k. Itakuaje kwa mwanamke uliyekutana nae atakuelewa vipi?

Personally ninaushuhuda wa rafiki yangu, alimuuza mchumba wake kama yeye akiwa mtu mwenye nyadhifa au umaarufu mjini ataweza stress za magezetini na vyombo vya habari? Dada kafunguka, yeye hawezi kabisa...atapendelea kama wataishi maisha ya chini, watoto wasome shule nzuri, chakula kiwepo nyumbani, aweze kuvaa vizuri basi.

Shida ipo kwenye jamii. Wahindi an ideal husband ni yule mwenye mabavu na uwezo wa kupambana na "social evils" ambazo huwakumba wanawake wa India kwa sehemu kubwa. Ila hapa kwetu wanawake wanapenda wanaume wenye pesa maana jamii yetu janga kubwa ni umasikini. Tunaamini ukiwa na pesa kila kitu kitakua sawa, kiasi kwamba wengi huamini ugomvi wa wazazi waliokuwa wakiuona walipokua wadogo chanzo ni pesa. Hivyo mume akiwa na pesa hakuna shida tena.
 
Katika kupenda naamini ni vema kuanza kumpenda mtu kwa asilimia 100 halafu zitabaki au kupungua kutokana na mtu atakapolipokea na kulienzi pendo lako kwake.

Kuliko kuanza na asilimia 0 ukitegemea penzi liongezeke kadri mtu atakavyokuwa anakujali na kukuenzi. Hili ni pendo la kinafiki na bahati mbaya wengi wapo kwenye aina hii ya kupenda.
 
Sawa mkuu. Acha tutafute pesa kwa bidii tutimize ndoto zao.
 
Inaizidi hata couple ya jay z na beyonce ?
Hao nao wana historia nayo,kwa kumbu kumbu nilizo nazo jigga & be wanaishi kwa utii fulan,coz ata ukiangalia age zao jigga mkubw kwa 12 ivi ...bt michele & obama only 3 yrs ivi ndo mana kuna greit respect 1 anothr,ata scandal zao sio kama za kina jay & beyonc ni zile za muda,readily undercorrection....still hawafiki obama & michelle....kinda lyk dem nd ar ril greit[emoji119]
 
Unajua ni kwa nini alilia? Analia sababu anajua mwisho wa ndoa yake umefikia. Inasemekana, "eti", Michelle alikuwa anataka kumwaga Obama siku nyingi tu lakini kwa sababu ya Urais akaona atachafua hali ya hewa, hivyo akaamua kusubiria jamaa amalize muda wake ndio amteme. Kama hizi tetesi zinaukweli basi itajulikana muda sio mrefu.
 
Hujawai kutana na matapeli wa mapenzi, jamii inabadilika kutokana na makosa ya jana. Mtu anakwambia anakupenda na wewe unampa hizo 100% baada ya 2 months ikatokea una mimba anakukana, na hamjafahamiana kiasi hicho kwamba inamjua kaka, dada au kwao. Wewe utafanya nini?
 
Du! Hii bado sijaipata.
 
Navyosema kumpenda mtu kwa asilimia 100 haina maana niwe mjinga. Mtu kuniambia ananipenda haimaanishi ananipenda kweli, inawezekana amenitamani tu.
Na hakuna upendo wa maneno, upendo ni matendo...nukta

Na kwa hiyo scenario yako hivi mtu hata simjui vizuri na wala hatujakubaliana tuzae, naanzaje kubeba mimba???? Siwezi
 

Naheshimu sana mawazo mpendwa na bila shaka tunaelewana vizuri. Nakubali kuwa mke ni image ya mumewe na ndio maana hata pengine mkanganyiko uliomo kwenye familia ya mkuluu yaani yeye na mke wake umechangia aonekane mtu wa ajabu ajabu tu kila leo amekosa mpaka huruma kwa familia nyingi za kitanzania hadi kufikia hatua kutuambia tufe na njaa.

Hiyo ya wanawake wenye nguvu kiuchumi na elimu kubwa kuolewa na wanaume wenye nguvu ndogo kiuchumi na elimu ndogo asee labda utakuwa unaziona huko mtaani unakoishi ila kwa ndoa nyingi nnazoziona mimi it is absolutely opposite na huko mtaani kwako.

Alafu nimelezea zaidi kwa kuegemea wanawake kulingana na topic yenyewe nilivyoikuta lakini pamoja na hivyo kuna mahali nime admit kuwa hata sisi wanaume tunatakiwa kuwa responsible coz we all have fair share in current situations, kuhusu kuwa na machaguo sikatai ila kuwa na vigezo vilivyopitiliza bila hata kufikiria kwa kina kuhusu vigezo hivyo huo ni upuuzi mkubwa. Bila shaka wewe mwenyewe unajua ni jinsia gani hasa inayokujaga na vigezo vingi.

Point kubwa hapo labda ni nyakati kubadilika kiuchumi na hii ndio imefanya huu uharibifu wote uwepo kiasi cha mapenzi kugeuka biashara na geniune love imekuwa replaced na vitu vingi ndio ile mtu anakupenda baada ya kuona una huakika wa kumlisha. Hivyo hatuna budi kucopy uhalisia uliopo.
 
Hahaha
Hii nayo habari mpya sijawahi skia
Landa ntafuatilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…