Nilipoona picha hii kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 10/02/2011 nilishindwa kujizuia kucheka kwa jinsi mwandishi alivyoiweka caption: 'TUKO PAMOJA: Mheshimiwa akifuatilia kwa makini mjadala bungeni...', it was hillarious indeed! Hata hivyo pamoja na hicho kuonekana kama kichekesho cha siku nikajikuta naboreka na kuchukizwa na tabia hii ya Waheshimiwa kuuchapa usingizi bungeni.
Kilichokuja kunimaliza zaidi ni response ya Mheshimiwa kuwa katika picha hiyo alikua 'amezama kwenye maombi mazito ya kuliombea bunge' na wala hakulala kama ilivyodhaniwa. Nchi hii ina vituko jamani, hivi kweli mtu mwenye mzigo wa uongozi kwa watu wake utapataje usingizi kirahisi hata chumbani kwako??... sembuse bungeni!!?
Mh. Regia Mtema alitoa kuwa kuwa bungeni ni sawa tudigrii moja au tatu ni sawa tu hata asiye kuwa nayo mwazo sawa maanake wengi hawaelewi wamekwenda mle kufanya nini
Hawa wabunge wanatufanya sisi wajinga,nani ambae hajui usingizi wa kulala na wa kuzama kimaombi!!!Unaliombea bunge wewe kama nani??Bungeni kuna muda wa kuomba dua kwa nini usiombe muda huo!!!Pole kwa waliompa KULA/KURA
Uliyetuma picha hii naomba tujulishe hii ni ya Bunge lililopita au la sasa... Kama ni sasa lazima tuwasiliane na wabunge waangalie uwezekano wa kutoa adhabu kwa watu kama hawa.... Sisi tunakufa njaa watu wanakula pesa kwa kulala bungeni... It is not fair
We geo uko wapi?Hii picha ni ktk bunge hili lililoanza juzi!!!eti anajitetea kuwa hakulala ila alizama ktk maombi-awadanganye hao wafuasi wake!!sisi tuko macho.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.