Hii imekaaje ya kuja kulipia daraja la Kigamboni?

Serikali yako mbovu imeshindwa jenga hilo daraja, waliojenga (NSSF nk) ndo lazima walipishe ili hela yao irudi. Ni kawaisa sana kulipia barabara nchi nyingi kama unataka kwenda fast
 
Labda mimi sielewi!

Sijawahi kusikia dunia hii kuna nchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaidi ya kodi, fines. Hii ya daraja la Kigamboni kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwani kodi tunazolipa zinafanya nini? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gani?

Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana JF naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia?

Na nini maana ya public goods?

Nawasilisha

Mkuu,
hao Watangazaji wa media kubwa ni wanafiki tu. They always portray bad image kwa Nchi zetu zinazoendelea,usishangae tafadhali hizo charges zipo mahala pote.

[h=1]Prices - private customers[/h] All prices are per single trip and including 25 percent VAT. Currency is euro (EUR).
Car up to 6 metres
SmutTur[SUP]4[/SUP]
BroPas[SUP]1[/SUP]14,0022.00
Cash payment 47.00
EasyGo 45.00
10-trip card (the card costs 354.00 [SUP]2[/SUP]) 35,40

Mobile home over 6 meters, car up to 6 metres with trailer/caravan
or car 6-9 metres[SUP]3[/SUP]
SmutTur[SUP]4[/SUP]
BroPas[SUP]1[/SUP]28,00 44.00
Cash payment 94.00
EasyGo 94.00
10-trip card (the card costs 354.00[SUP]2[/SUP]) 70.80

Motorcycle
SmutTur[SUP]4[/SUP]
BroPas[SUP]1[/SUP]7,0010.00
Cash payment 25.00
EasyGo 25.00
10-trip card (the card costs 195.00[SUP]2[/SUP]) 19.50

1) The BroPass agreement includes an ongoing annual subscription of 39.00 EUR.

2) When you purchase a 10-trip card you pay for all 10 trips, e.g. 354/195 EUR. The card is valid for one year. Should you not use all 10 trips within that year, our Customer Service will refund the price of the card minus the cash price of the number of trips you have used plus a fee of 50 DKK.

3) If the car is over 6 meters and the total length of car and trailer/caravan is over 9 meters, the price is according to length - please see our Business prices

4) The short break price "SmutTur" applies for outward journeys made between 5 pm and midnight, Monday to Friday, and all day on weekends and holidays. Whenever you travel, you must use a ØresundBizz® transponder and make the return journey within six hours of departure.

Huo ni mfumo wa malipo kwa Daraja moja tu la Oresund ambalo niliwahi liwekea thread huko nyuma. Kwahiyo malipo yapo tu sema unafiki wao tu.
 
Kazi mojawapo ya hili jukwaa iwe kuelimishana.Huyu anafahamu hiki yule anafahamu kile nk.SIyo kila mmoja anafanya kazi serikalini.Mleta mada angefahamishwa tu kwa lugha nzuri kuliko kufahamishwa na kupewa kejeli.Nashukuru sana kwa waliompa elimu kwa lugha ya staha.

Mtoa mada-Hicho unachokisema ni kitu kipo duniani kote zinaitwa TOLL ROAD (barabara za kulipia),ndiyo kwanza mambo haya yanaingia Tanzania.Tanroads wako kwemye mpango wa kujenga barabara ya kulipia ya njia sita (3 go/3 return) kutoka Mbagala rangi tatu hadi Chalinze.Kama hutaki foleni za Ubungo unachepuka huko unakimbiza gari 120KM/hr.Hii miradi inaitwa kwa kizungu Public private partnerships (PPP.Kampuni binafsi zinaijengea serikali miundo mbinu halafu zinarudisha fedha zao kwa kukusanya mapato.Mfano mwingine ni huo wa mabasi yanendayo kasi (BRT) Daresalaam.

Miradi hii ni ile tu inayotoa huduma kwa wananchi ambapo huduma hizo zilitakiwa kutolewe na serikali.Miradi mizuri sana.

hapo kunasababu gan yakuwa na serikari isiyokuwa na manufaa kwa watu wake
 
Jana akijinasibu kwa wakazi wa Kigamboni Magufuli alisema akichaguliwa wakazi hao watapia daraja la Kigamboni bure! Lakini akasema wenye magari binafsi lazima walipie hiyo uduma, sasa najiuliza hao wananchi watapitaje bure kwa kutembea au?, na kama watapanda daladala si watakuwa washalipa nauli kwenye vituo vya daladala? Sasa hiyo ni bure ama ndo changa la macho. Labda ziwekwe daladala za serikali alafu zitoe huduma hiyo bure lakini kwa daladala za watu binafsi hilo HALIWEZEKANI!!!! 25-OCT 2015 thinks will be harder!!
 
Mimi nadhani kila daraja lina umuhimu wake fikiria tu pale mto wami si inabidi kiwepo kizuizi ili wenye magari walipe kama ni utaratibu kuwa hata kwa wenzetu waliendelea ulipaji wa aina hii upo sioni kama hili la kigamboni lina umuhimu tofauti..Na je nini maana ya ile road license??au kunatakiwa kuwepo na bridge license kuepusha usumbufu?teh,teh...
 
Kama NSSF hufanya biashara kwa nini fedha za Wafanyakazi hazilipwi na RIBA? Pamoja na kugharamia uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.Dr wambie CCM walipe madeni yetu na riba.
 
Labda mimi sielewi!

Sijawahi kusikia dunia hii kuna nchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaidi ya kodi, fines. Hii ya daraja la Kigamboni kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwani kodi tunazolipa zinafanya nini? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gani?

Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana JF naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia?

Na nini maana ya public goods?

Nawasilisha

Utasikiaje dunia nzima na ww unakaa manzese unabwata ? Dunia nzima kuna barabara za kulipia hata madaraja !
 
Mkuu hata mimi nimeshangaa sana kumsikia John Pombe Magufuli akitamka kwenye kampeni huko kigamboni (alikowaambia wapige mbizi) kuwa waenda kwa miguu hawatalipia nauli ila magari yatalipa nauli. Nikajiuliza mbona madaraja mengine hatulipi nauli iweje hili la kigamboni tulilipie? Huyo ndiyo John Pombe Magufuli raisi anayeomba kura za wananchi!!!!
Labda mimi sielewi!

Sijawahi kusikia dunia hii kuna nchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaidi ya kodi, fines. Hii ya daraja la Kigamboni kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwani kodi tunazolipa zinafanya nini? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gani?

Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana JF naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia?

Na nini maana ya public goods?

Nawasilisha
 
Mbona madaraja mengine hatulipii? Hili lina nini? Daraja refu la mto rufiji mbona tunapita bure? Kwa vile wamejenga NSSF ndiyo tulilipie? Serikali itumie kodi zetu kuilipa NSSF. Nashukuru sikai huko!!!!
Usipende vya bure.........daraja linajengwa na NSSF sasa michango yetu unataka irudi vipi?
 
Duh!!! Magufuli style!!!! Nchi hii hatujafikia hapo eti tulipie gharama ambazo serikali yetu inaweza kugharamia. Kwanza wananchi wengi kipato ni kidogo. Pili wenye magari wengi ni mikopo ya benki siyo kwamba wana pesa. Kuwalipisha mtakuwa mnawaonea. Kusanyeni kodi za kutosha ili mpate fedha. Kwani mnategemea kukusanya shilingi ngapi na mmepanga kuzifanyia nini???
Huyo mtangazaji wa BBC kama kashangaa kweli basi itakuwa kwa sababu nyengine, sio kwa kuwa hajawahi kusikia ama kuona ama kutumia barabara na madaraja ya kulipia. Uingereza barabara hizo zimejaa tele, pamoja na nchi nyengine zilizoendelea.

Katika nchi zinazoendelea zenye huduma kama hizo ni pamoja na China, Thailand,...

Asiyeweza kulipia daraja apande pantoni au apige mbizi :]
 
Na watu bado wanaishabikia serikali ya ccm!!!!
tanzania,tanzaniaaaaaaaa nakupenda kwa moyo woteeeeeeeeeee.......
nchi yangu tanzaniaaa jina lako ni tamu sanaaaaaaaaaaaaaa x2
nilalapo nakuwaza weweeeee.
niamkapo ni heri mama weeee.
tanzania tanzania jina lako ni tamu sanaaa...........

nikiukumbuka huu wimbo machozi yananitoka.
hawa viongozi walikuwa wanaomba mwalimu afe ili waiuze hii nchi?
je wanafikiri baada ya dhulma hizi dhidi ya wanyonge wao na familia zao wwatapona?

ee mungu nipe maisha marefu ili niushudie mwisho wao.
 
Labda mimi sielewi!

Sijawahi kusikia dunia hii kuna nchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaidi ya kodi, fines. Hii ya daraja la Kigamboni kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwani kodi tunazolipa zinafanya nini? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gani?

Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana JF naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia?

Na nini maana ya public goods?

Nawasilisha

Daraja pia linahitaji ukarabati wa mara kwa mara, hivyo lazima watumiaji walipie.
 
Back
Top Bottom